Swali la kizushi but important

SI unit

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
1,953
766
Hi ladies and gentlemen. Siku za hivi karibuni, mikasa ya usaliti na kukosa uaminifu kwenye mapenzi imekua inaongezeka kwa kasi. Sababu zipo nyingi na thread zenye hizo sababu naamini zilishaanzishwa mara nyingi humu MMU. Ninachojiuliza, kati ya upendo (kupenda) na tamaa (kutamani) kipi kina nguvu. (Of the two which is more powerful and leads the other).
Your coments plz.
 
Uzushi hauwezi kuwa muhimu.

Kutamani kunachuja haraka, vinavyotamaniwa mara nyingi vikikosekana ndio basi tena, tamaa haivumilii, tamaa haijali wala tamaa haina huruma. Mapenzi on the other hand kama yapo ya kweli utafaidi maana hata pale utakapokua una mapungufu mwenzio anaweza akayavumilia, ukimhitaji atakuwepo, ukianguka atakusaidia uinuke tena n.k

Sasa chagua mwenyewe hapo kipi kina nguvu.
 
Kupenda ni moto wa mkaa wa mti wa mgunga. Ni moto uwakao taratibu hivyo kuendelea kuwaka kwa muda mrefu sana lakini tamaa ni moto wa kifuu
 
.
What are the components of tamaa. Sura/mwonekano wa kuvutia or valuable material things? For what i guess (not sure) tamaa ndio inaanza na upendo ni baada ya tamaa kuota mizizi. Inawezekana kumpenda mtu ambaye hajakuvutia?
 
Kupenda ni moto wa mkaa wa mti wa mgunga. Ni moto uwakao taratibu hivyo kuendelea kuwaka kwa muda mrefu sana lakini tamaa ni moto wa kifuu
.
Kwa hiyo unanikubalia tamaa is the leader au sio? Coz moto wa kifuu unawashwa the same way kama huo moto wa mkaa wa mti wa mgunga..
 
.
What are the components of tamaa. Sura/mwonekano wa kuvutia or valuable material things? For what i guess (not sure) tamaa ndio inaanza na upendo ni baada ya tamaa kuota mizizi. Inawezekana kumpenda mtu ambaye hajakuvutia?

Kwani ukivutiwa na kitu lazima ukitamani? Kuna kuvutiwa kunakozaa kupenda hicho kitu na sio kutamani.

Kuhusu components za kutamani, nadhani ungekuja nazo wewe mwenye swali ili tuelewe nini haswa unachoongelea.
 
Tamaa ni kukidhi hamu ya muda mfupi (unaweza kujizuia, kusahau au kutokujiweka kwenye mazingira ya vishawishi)

Kupenda comes from within (ni vigumu kujizuia wala kusahau hata ukiwa mbali still unaweza ukakumbuka na kuumia) upendo ukisalitiwa, ukiukosa can lead to broken heart ukiupata na kurudishiwa furaha yake you can't compare (concequences zake ni kubwa)

In short duniani hakuna a strong force kama upendo, you can even destroy enemies with upendo, kama tungekuwa na upendo wa kutosha sidhani kama hata kungekuwa na vita...,
 
Hivi unaweza kupenda bila kutamani kweli au Unaweza tamani bila kupenda? Nijuavyo mimi vinavyo tamaniwa na vinavyopendwa vyote ni vizuri so what's the difference? Tofauti inakuja kuwa kwenye Upendo tamaa inadumu na kuendelea i think.
 
Hivi unaweza kupenda bila kutamani kweli au Unaweza tamani bila kupenda?
ofcourse unaweza kumtamani yule dada kwa maumbile yake, lakini simpendi, pia naweza kumpenda mke wangu ingawa sasa kapata ajali na umbo lake halipendezi ila bado nampenda, au ingawa physically simtamani ila nampendea character yake.

Nijuavyo mimi vinavyo tamaniwa na vinavyopendwa vyote ni vizuri so what's the difference? Tofauti inakuja kuwa kwenye Upendo tamaa inadumu na kuendelea i think.

Mkuu tamaa mbaya haina uzuri wowote na mara nyingi tamaa haina kikomo ukipata ukitakacho bado utataka zaidi na zaidi
 
Mi nauliza, unajuaje kama umependa au umetamani? Kuna mtu sijui nampenda, sijui namtani! Msaaaada plzzzz.
 
Mi nauliza, unajuaje kama umependa au umetamani? Kuna mtu sijui nampenda, sijui namtani! Msaaaada plzzzz.
unaweza ukapenda na kutamani pia ila kutamani sio kupenda, kupenda ni zaidi ya kitu unachopata (au hamu uliyonayo) nikimaanisha kwamba ukipenda hata hicho ulichotamani mwanzo kikiondoka uwezekano mkubwa bado utaendelea kupenda tofauti na tamaa (ukikidhi haja yako tamaa inakwisha) yaani kama ukishakula mua unavyotupa lile ganda (utamu umekwisha !)
 
ahsante ila bado sijaelewa, kutamani ni nini na kupenda ni nini?
 
ahsante ila bado sijaelewa, kutamani ni nini na kupenda ni nini?
Nakutamani sijakuona siku nyingi natamani kusikia story zako natamani company yako tukiangalia movies, natamani kusikia kicheko chako na tabasamu lako..., lakini nakupenda kwa roho moja sitaacha kukupenda kamwe hata pale ukibadilisha mood yako ukaacha kutabasamu, kunipa company n.k.
 
ukisema unatamani unamaanisha nini?
 
ukisema unatamani unamaanisha nini?
hamu, kiu, shauku, curiosity n.k. naweza nikawa natamani company ya msichana ambayo kwenye bar yoyote ya karibu nitakidhi hamu yangu.., ila upendo kama ni kwa Hus basi Asha au Mwajuma hawawezi nitimizia..., and don't get me wrong huenda tamaa yangu ni ya kumpata Asha pekee basi hadi siku takapompata Asha tamaa haitaisha na huenda ninatamani kile alichonacho Asha hivyo mara kwa mara huenda nikawa namtafuta Asha kukidhi hamu..., kwahio upendo is a package ambayo kutamani ni ingredient ya hio package (subset).

Kutamani pekee does not mean umependa ila kupenda means unatamani pia
 
Back
Top Bottom