Swali la Kizushi; Bangi ikikamatwa inachomwa, Cocaine Inakwenda wapi???

Kwa nini bangi ikikamatwa yachomwa mbele ya waandishi wa habari na makamera na mapolisi n.k n.k.
Lakini kwa upande wa sembe(Ngada) hawafanyi hivyo?
 
Nimeona niulize hili swali kwani Mara nyingi nimekua nikiwaona TFDA wakiteketeza Bidhaa feki (vyakula na dawa) Mara wanapozikamata.

Nimeona Askari wakiteketeza Silaha/ Bunduki zinazomilikiwa kinyume na sheria kule Kigoma kwa kuzichoma.

Ila sijawahi kusikia Askari wameteketeza Kiasi Fulani cha dawa za kulevya , Je zikikamatwa hupelekwa wapi? Ukizingatia ni vitu vya thamani sana.
 
Tanzania Portland cement company Ltd. Huwa wanaleta hapa kuzichoma kwenye mtambo maalumu.

Wanakuja na escort ya hali ya juu utazani kuna vita lakini wataalam wanakuambia unga khalisi umeechwa sehemu.
 
Tanzania Portland cement company Ltd. Huwa wanaleta hapa kuzichoma kwenye mtambo maalumu.

Wanakuja na escort ya hali ya juu utazani kuna vita lakini wataalam wanakuambia unga khalisi umeechwa sehemu.

Naomba majina yako halisi makonda anakuulizia mkuu
 
Nimeona niulize hili swali kwani Mara nyingi nimekua nikiwaona TFDA wakiteketeza Bidhaa feki (vyakula na dawa) Mara wanapozikamata.

Nimeona Askari wakiteketeza Silaha/ Bunduki zinazomilikiwa kinyume na sheria kule Kigoma kwa kuzichoma.

Ila sijawahi kusikia Askari wameteketeza Kiasi Fulani cha dawa za kulevya , Je zikikamatwa hupelekwa wapi? Ukizingatia ni vitu vya thamani sana.
Jibu lipo mkuu kuna usanii mkubwa sana unaoendelea vingine ni vema kukaa kimya ili kuinusuru nafsi yako
 
Nimeona niulize hili swali kwani Mara nyingi nimekua nikiwaona TFDA wakiteketeza Bidhaa feki (vyakula na dawa) Mara wanapozikamata.

Nimeona Askari wakiteketeza Silaha/ Bunduki zinazomilikiwa kinyume na sheria kule Kigoma kwa kuzichoma.

Ila sijawahi kusikia Askari wameteketeza Kiasi Fulani cha dawa za kulevya , Je zikikamatwa hupelekwa wapi? Ukizingatia ni vitu vya thamani sana.
Madawa huwa yanateketezwa kwenye kiwanda chochote chenye tanuru la moto, kwa DAR ni kiwanda cha cement cha Wazo kwa kuchomwa moto kwenye tanuru la moto mkali na kugeuka hewa.

Tatizo yanapokamatwa huwa ni Mkemia Mkuu huwa anathibitisha ni madawa kweli, ila kinachoteketezwa huwa ni unga wa sembe, ndio maana huitwa sembe!, wala mkemia huwa haitwi kuthibitisha tena, tangu yakikamatwa na kuhifadhiwa kama ushahidi, kuna mazingaombwe hutokea, madawa yale hugeuka unga wa sembe!.

Mtuhumiwa Mkenya Nurdin Akasha alipokamatwa na tani za madawa, kwenye semi tella tatu na madawa yakahifadhiwa strong room za polisi, kesi ilipoanza, mahakama ilipokweda kushuhudia ushahidi, wakathibitisha ni unga, akahukumiwa jela miaka 10, kabla hajatumikia kifungo, akaugua ghafla na kulazwa ICU Muhimbili, kwa vile alikuwa mahututi akipumulia mashine, alipangiwa kulindwa na askari magereza wa kike, asubuhi yake walikuta shuka tuu, Akasha ali vanish into thin air!, walipofuatilia ule mzigo ili ukateketezwe Wazo, wakakuta ni unga wa sembe!.

JIJI LA MBEYA LATEKETEZA MADAWA YA KULEVYA YA SH 1.8 BILIONI.
Juma Mtanda 7:11 PM

DSC00302.JPG

Madawa ya kulevya yenye thamani ya sh 1.8 Bilioni yakiteketezwa kwa kumbukizwa katika tanuru la moto mkali ili kuweza kuyuka chini ya ulinzi mkali wa askari wa jeshi la polisi mkoani Mbeya. Dawa hizo ni zile ambayo zilikamatwa mpaka mwa Tunduma mwaka 2010 washukiwa wakiwa ni raia wawili wa Afrika kusini, Vuyo Jack na mkewe Anastazia Cloete.
DSC00212.JPG
Dawa hizo za kulevya zateketezwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
DSC00296.JPG

DSC00246.JPG
DSC00254.JPG

DSC00317.JPG

DSC00277.JPG

IMG_3182322421696.jpeg

Raia wawili wa Afrika kusini, Vuyo Jack, na mkewe Anastazia Cloete.
Paskali
 
Acha madawa kuna siku zilikamatwa gunia 200 za bangi kutoka Arusha sijui zilipotelea wapi mpaka Leo......

Zilikamatiwa maeneo ya manyara kwenye maroli ya mizigo 4 .......
 
Umesahau nyavu bandia zikikamatwa zinachomwa moto huku media kibao zikimulika
 
Nimetafakari nikaona tushirikishane,Vipo vitu haramu vinateketezwa mara nyingi.
1.Silaha haramu.Tumeona
2.Madawa feki.Tumeona
3.Bangi.Tumeona
4.Mirungi.Tumeona
N.k.
Vipi madawa ya kulevyia?"Unga"Mbona sijawahi kuona ukiteketezwa?Si umekamatwa mara nyingi na kwenye Tv tukaona hayo makete?Zinapelekwa wapi?
Karibuni!
 
Nimekaaa nikatafakari sana baada ya leo kusikia kuwa eti ni siku ya Kupiga vita madawa ya kulevya; nikamsikiliza na Lukuzi nae, mmmmhhhh nikajiuliza hivi, kila siku tunaona madawa mbali mbali yakikamatwa ikiwa ni pamoja na Bangi, Cocaine na mengineyo; Juzi hapa wakakamata bangi kilo mia nne, shamba la bangi Korogwe likachomwa moto na kwingineko.

Je, Cocaine na madawa ambayo yako imported huwa yanapelekwa wapi? Yamehifadhiwa wapi na kwa ajili gani?

HUKUMSIKIA MAKONDA, ALIBAINISHWA NA KUSEMA KWAMBA ASKARI WAKIKAMATA COCAINE, WEWE ULIYEKAMATWA UNATAKIWA UTAJE WATEJA WAKO ILI WAKAUZE, NA MMOJA WA ASKARI AMEPAMBANA HADI AMENUNUA NYUMBA KIGAMBONI....ULE MZIGO WA LINDI ULIOKAMATWA, JPM MWENYEWE JANA KAGWAYA, ETI UMEMKAMATA MTU NA NGADA HALAFU UPELELEZI UNAENDELEA...USIFANYE MCHEZO NA WAUZA NGADA, WAPO TAYARI KUUUA UKOO WENU WOTE, ILI WASIJULIKANE MISHE ZAO...OGOPA SANA HAWA WATU, KINA AKASHA WA MOMBASA KENYA, WANARITHISHANA TU HII BIASHARA NA HAWAKAMATWI NA DUNIA NZIMA INAWAJUA...HATARI SANA MKUU!
 
We ulishaona wapi pesa inachomwa?? Huwa wanachoma bangi, nyavu za kokoro, vyakula na vipodozi vibovu waonekane wanakerwa na vitu hivyo, unga ukikamatwa nadhani huwa unarudi sokoni. Vinginevyo watuoneshe wanavyouteketeza kama wanavyotuonesha bidhaa nyingine. Hapo najua watatoa kisingizio cha ushahidi mahakamani ndii maana hawachomi, Je hivyo vinavyochomwa vyenyewe sio ushahidi????!
 
Back
Top Bottom