Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,021
- 2,481
Mheshimiwa Dkt. Suleiman Jaffo,
Waziri wa Mazingira,
Mkutano wa kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi unafanyika huko Dubai, kwa siku 14, tangu tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba 2023.
Lakini ukubwa wa ujumbe wa Tanzania umeibua utata miongoni mwa Watanzania wanaotaka serikali ibane matumizi.
Tanzania imewakilishwa na watu 764. Watu wapatao 391 kati yao ni watumishi wa umma. Watu baki wametoka sekta binafsi.
Jedwali lifuatalo hapa chini linaonyesha mchanganuo wa wajumbe wa Tanzania. Na faili kamili la MS Excel limeambatanishwa hapa chini kwa ufafanuzi zaidi.
Kwa wale wanaotaka ulinganisho mpana, pia tumeambatanisha Jedwali kamili ya wajumbe wote duniani waliohudhuria COP28.
Kwa mujibu wa Jedwali hili, Kidunia nchi zenye wajumbe wengi ni UAE (4,409), Brazil (3,081), China (1,411), Nigeria (1,411), Indonesia (1,229), Japan (1,067) na Turkey (1,045).
Na kwa upande mwingine, kidunia nchi zenye wajumbe wachache ni North Korea (2), Nicaragua (6), Eritrea (7), Liechtenstein (8) na Moldova (8).
Katika Bara la Afrika, nchi ya kwanza kwa wajumbe wengi ni Nigeria(1411), Ya pili ni Morocco (823), Ya tatu ni Kenya (765), Ya nne ni Tanzania (764), Ya tano ni Ghana (618), ya sita ni Uganda (606). Zingine ni DR Congo (590), Rwanda (223), Burundi (172), na South Sudan (158).
Tunaelewa kwamba kila Taifa linayo Kamati yake ya kupima, Kuripoti na kuthibitisha taarifa juu ya mabadiliko ya tabianchi.
Yaani, "National Measurement, Reporting, and Verification Framework" au "National MRV Framework" kwa kifupi. Mfano wa National MRV Framework" unaonyeshwa hapa chini katika picha.
Kamati hii ya MRV katika ngazi ya kitaifa ndiyo huripoti kwenye mkutano wa COP28. Ukubwa wa timu ya wawakilishi wake unategemea nguvu za kiuchumi za nchi husika. Maswali muhimu hapa ni haya:
- Je, kwa sasa "National MRV Framework" ya Tanzania inao watu wangapi?
- Je, Kama Kamati ya MRV ya Tanzania inao wajumbe pungufu ya watu 391, ambayo ni idadi sawa na Bunge zima la Tanzania, kwa nini Tanzania imewakilishwa na ujumbe mkubwa hivi?
- Je, wakati dunia ya leo inaendeshwa kwa kutumia kanuni za demokrasia ya uwakilishi vikao cya COP vinatumia kanuni za demokrasia ya moja kwa moja?
- Na je, ijapokuwa "COP’s Rules of Procedure" hazisemi kiwangocha chini cha wajumbe wa lazima kutoka nchi mwanachama wa Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Tabianchi, sisi kama Taifa tunapaswa kutumia vigezo gani kuamua juu ya suala hili, na vigezo hivi vimezingatiwa kwa kiasi gani?
Vinginevyo mikutano ya COP sasa itaonekana kama ziara binafsi za kuwapa wajumbe nafasi ya utalii binafsi wa kimataifa kwa kutumia fedha za umma pasipo ajenda yoyote ya maana kwa Taifa.
Tunapaswa kujifunza kutokana na sakata la Rais Mwinyi na Bi Mkubwa baada ya Earth Summit, yaani Mkutano wa Mazingira uliofanyika huko Rio de Janeiro mwaka 1992.
Katika ziara hiyo, Tanzania ilihusisha watoto wa shule, akiwemo mwanafunzi mmoja aliyejulikana kama Bi Mkubwa Rajab, binti yake Mzee Kitwana Kondo.
Binti huyu alimletea msukosuko Rais Mwinyi wakati ule. Vijiweni Dar es Salaam kulizuka kejeli kuwa Rais Mwinyi alikweda kwa Mzee Kitwana Kondo kuchumbia akitumia maneno haya: "Bi Mkubwa anifaa sana, maana anayo miaka yoye ya CCM na mitano juu."
Uvumi ulizagaa. Ilifika hatua mpaka Rais akaitisha mkutano wa hadhara Mnazi Mmoja kukanusha uvumi.
Taarifa zinasema kuwa, siku hiyo Rais Mwinyi aliwauliza mabinti wa shhule ya Jangwani, "Eti Mie Nimemwoa mwenzenu?"
Tunayoyasema kuhusu Tanzania yanazihusu nchi zingine pia. Mikutano ya COP haipaswi kuwa sababu ya kufuja fedha za umma pasipo ajenda ya umma inayoeleweka.
Taarifa hizi zimechakatwa na:
Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
SLP P/Bag
"Sumbawanga Town"
Sumbawanga