Swali kwa Waziri wa Mazingira, Dkt Suleiman Jaffo: Watumishi wa umma 333 wamefuata nini kwenye mkutano wa COP28 huko Dubai?

Mtoto wa Samia, Abdul - Halim Hafidh Ameir ameandikwa ni National delegate.

Swali la kujiuliza huyu mtu ni National delegate kutoka taasisi ipi?

Hii ni serious state capture.
Hapo president office hujaona mkuu....acheni watumishi nao wale mema ya nchi ingawaje sijaona hapo wizara ya elimu ikimaanisha kwamba walimu wamewekwa kando kwenye huu ulaji.​
 
Kama walitenga bajeti au kama uhusiano wao mzuri na Dubai umewasaidia kupeleka watu wengi COP28 hilo ni jambo la kupongeza!
Climate Change is a serious threat to humanity. And global conferences the right spot to negotiate and deliberate on the matter.
Mama Amon ungetuletea pia event schedules ili tujue je kwa idadi ya watu walioenda COP28 EXPO CITY wanaweza kuhudhuria kila major event na side events??
Hata hivyo tujenge interest ya kuhudhuria matukio ya kimataifa yenye relevance kubwa kwetu!
 
View attachment 2835179

Mheshimiwa Dkt. Suleiman Jaffo,
Waziri wa Mazingira,

Mkutano wa kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi unafanyika huko Dubai, kwa siku 14, tangu tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba 2023.

Lakini ukubwa wa ujumbe wa Tanzania umeibua utata miongoni mwa Watanzania wanaotaka serikali ibane matumizi.

Tanzania imewakilishwa na watu 764. Watu wapatao 391 kati yao ni watumishi wa umma. Watu baki wametoka sekta binafsi.

Jedwali lifuatalo hapa chini linaonyesha mchanganuo wa wajumbe wa Tanzania. Na faili kamili la MS Excel limeambatanishwa hapa chini kwa ufafanuzi zaidi.

View attachment 2835194

Kwa wale wanaotaka ulinganisho mpana, pia tumeambatanisha Jedwali kamili ya wajumbe wote duniani waliohudhuria COP28.

Kwa mujibu wa Jedwali hili, Kidunia nchi zenye wajumbe wengi ni UAE (4,409), Brazil (3,081), China (1,411), Nigeria (1,411), Indonesia (1,229), Japan (1,067) na Turkey (1,045).

Na kwa upande mwingine, kidunia nchi zenye wajumbe wachache ni North Korea (2), Nicaragua (6), Eritrea (7), Liechtenstein (8) na Moldova (8).

Katika Bara la Afrika, nchi ya kwanza kwa wajumbe wengi ni Nigeria(1411), Ya pili ni Morocco (823), Ya tatu ni Kenya (765), Ya nne ni Tanzania (764), Ya tano ni Ghana (618), ya sita ni Uganda (606). Zingine ni DR Congo (590), Rwanda (223), Burundi (172), na South Sudan (158).

Tunaelewa kwamba kila Taifa linayo Kamati yake ya kupima, Kuripoti na kuthibitisha taarifa juu ya mabadiliko ya tabianchi.

Yaani, "National Measurement, Reporting, and Verification Framework" au "National MRV Framework" kwa kifupi.

View attachment 2835261

Kamati hii ya MRV katika ngazi ya kitaifa ndiyo huripoti kwenye mkutano wa COP28. Ukubwa wa timu ya wawakilishi wake unategemea nguvu za kiuchumi za nchi husika.

Swali ni kwamba, Kamati ya MRV ya Tanzania inao wajumbe 330, ambayo ni idadi sawa na Bunge zima la Tanzania? Watanzania wengi wanauliza swali hili, na ni muhimu kwa serikali kulijibu.

Vinginevyo mikutano ya COP sasa itaonekana kama ziara binafsi za kuwapa wajumbe "exposure" ya kimataifa kwa kutumia fedha za umma pasipo ajenda yoyote ya maana kwa Taifa.

Tusisahau yale ya Mkutano wa Rio de Janeiro mwaka 1992 ambapo ziara ya Tanzania ilihusisha watoto wa shule, akiwemo mwanafunzi mmoja aliyejulikana kama Bi Mkubwa Rajab, binti yake Mzee Kitwana Kondo.

Binti huyu alimletea shida Rais Mwinyi wakati ule. Vijiweni Dar es Salaam kulizuka kejeli kuwa Rais Mwinyi alikweda kwa Mzee Kitwana Kondo kuchumbia akitumia maneno haya: "Bi Mkubwa anifaa sana, maana anayo miaka yoye ya CCM na mitano juu."

Uvumi ulizagaa. Ilifika hatua mpaka Rais akaitisha mkutano wa hadhara Mnazi Mmoja kukanusha uvumi.

Taarifa zinasema kuwa, siku hiyo Rais Mwinyi aliwauliza mabinti wa shhule ya Jangwani, "Eti Mie Nimemwoa mwenzenu?"

Tunayoyasema kuhusu Tanzania yanazihusu nchi zingine pia. Mikutano ya COP haipaswi kuwa sababu ya kufuja fedha za umma pasipo ajenda ya umma inayoeleweka.

Taarifa hizi zimechakatwa na:

Mama Amon
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
SLP P/Bag
"Sumbawanga Town"
Sumbawanga
Mwisho wa mwaka huu, ni muda wa watu kutoana out baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa na visirani vya kukwaruzana na mabosi.
Swali ni je, hao wote wamelipiwa na serikali? Bila shaka jibu ni hapana.
 
Wachache sana hao, ilitakiwa kila watu 1000 angalau wawakilishwe na mtu mmoja.
 
Per diem za kutosha
Hebu tupige hesabu kidogo:
Kwa maafisa wa serikali (na hasa wale wanaokwenda kwenye COP huwa ni Principal Officers and above) = USD (420+incidental 84) = 504/day x 14 days = 7,056, hapo bado ticket na kwa wale wakurugenzi, makatibu wakuu na mawaziri ongeza na enterterinment allowance (?). Tickets kwa PS na wajuu ni kuanzia Business class.

Hesabu yangu ya darasa la saba imekomea hapo.
 
Sahivi ndiyo ana-connection zote za maza ajili ya kupiga pesa za umma za wajinga wabara
WhatsApp Image 2023-08-13 at 11.04.24.jpeg

Miezi michache iliyopita alienda Uganda na kuonana na Museveni kwenye delegation ya serikali kujadili masuala ya nishati ila hatuambiwi kwenye hiyo delegation alienda kama nani.
 
Hapo president office hujaona mkuu....acheni watumishi nao wale mema ya nchi ingawaje sijaona hapo wizara ya elimu ikimaanisha kwamba walimu wamewekwa kando kwenye huu ulaji.​
Watu wamebeba hadi vimada wao!

Marehemu Bob Marley alisema ni rahisi kudanganya watu wote , ila sio rahisi kudanganya watu wote kwa wakati wote .
 
View attachment 2835179

Mheshimiwa Dkt. Suleiman Jaffo,
Waziri wa Mazingira,

Mkutano wa kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi unafanyika huko Dubai, kwa siku 14, tangu tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba 2023.

Lakini ukubwa wa ujumbe wa Tanzania umeibua utata miongoni mwa Watanzania wanaotaka serikali ibane matumizi.

Tanzania imewakilishwa na watu 764. Watu wapatao 391 kati yao ni watumishi wa umma. Watu baki wametoka sekta binafsi.

Jedwali lifuatalo hapa chini linaonyesha mchanganuo wa wajumbe wa Tanzania. Na faili kamili la MS Excel limeambatanishwa hapa chini kwa ufafanuzi zaidi.

View attachment 2835194

Kwa wale wanaotaka ulinganisho mpana, pia tumeambatanisha Jedwali kamili ya wajumbe wote duniani waliohudhuria COP28.

Kwa mujibu wa Jedwali hili, Kidunia nchi zenye wajumbe wengi ni UAE (4,409), Brazil (3,081), China (1,411), Nigeria (1,411), Indonesia (1,229), Japan (1,067) na Turkey (1,045).

Na kwa upande mwingine, kidunia nchi zenye wajumbe wachache ni North Korea (2), Nicaragua (6), Eritrea (7), Liechtenstein (8) na Moldova (8).

Katika Bara la Afrika, nchi ya kwanza kwa wajumbe wengi ni Nigeria(1411), Ya pili ni Morocco (823), Ya tatu ni Kenya (765), Ya nne ni Tanzania (764), Ya tano ni Ghana (618), ya sita ni Uganda (606). Zingine ni DR Congo (590), Rwanda (223), Burundi (172), na South Sudan (158).

Tunaelewa kwamba kila Taifa linayo Kamati yake ya kupima, Kuripoti na kuthibitisha taarifa juu ya mabadiliko ya tabianchi.

Yaani, "National Measurement, Reporting, and Verification Framework" au "National MRV Framework" kwa kifupi.

View attachment 2835261

Kamati hii ya MRV katika ngazi ya kitaifa ndiyo huripoti kwenye mkutano wa COP28. Ukubwa wa timu ya wawakilishi wake unategemea nguvu za kiuchumi za nchi husika.

Swali ni kwamba, Kamati ya MRV ya Tanzania inao wajumbe 330, ambayo ni idadi sawa na Bunge zima la Tanzania? Watanzania wengi wanauliza swali hili, na ni muhimu kwa serikali kulijibu.

Vinginevyo mikutano ya COP sasa itaonekana kama ziara binafsi za kuwapa wajumbe "exposure" ya kimataifa kwa kutumia fedha za umma pasipo ajenda yoyote ya maana kwa Taifa.

Tusisahau yale ya Mkutano wa Rio de Janeiro mwaka 1992 ambapo ziara ya Tanzania ilihusisha watoto wa shule, akiwemo mwanafunzi mmoja aliyejulikana kama Bi Mkubwa Rajab, binti yake Mzee Kitwana Kondo.

Binti huyu alimletea shida Rais Mwinyi wakati ule. Vijiweni Dar es Salaam kulizuka kejeli kuwa Rais Mwinyi alikweda kwa Mzee Kitwana Kondo kuchumbia akitumia maneno haya: "Bi Mkubwa anifaa sana, maana anayo miaka yoye ya CCM na mitano juu."

Uvumi ulizagaa. Ilifika hatua mpaka Rais akaitisha mkutano wa hadhara Mnazi Mmoja kukanusha uvumi.

Taarifa zinasema kuwa, siku hiyo Rais Mwinyi aliwauliza mabinti wa shhule ya Jangwani, "Eti Mie Nimemwoa mwenzenu?"

Tunayoyasema kuhusu Tanzania yanazihusu nchi zingine pia. Mikutano ya COP haipaswi kuwa sababu ya kufuja fedha za umma pasipo ajenda ya umma inayoeleweka.

Taarifa hizi zimechakatwa na:

Mama Amon
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
SLP P/Bag
"Sumbawanga Town"
Sumbawanga
Hao ni watu wa "State Capture." Ikumbukwe kuwa Climate Change is a falsified agenda ya NWO,kwa hiyo agents wa NWO lazima wahudhurie kwa wingi ili ionekane kwamba inaungwa mkono.
 
Wanafanya hayo huku barabara Jiji la Dar tu ni mahandaki kila kona.

Nenda hospital yaani facilities ni chakavu mpaka inatia huruma.

Ipo haja wahusika wajiuzulu nafasi zao.

Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
Ccm ni ile ile oh ni ile ile
 
Hivi tuna uhakika kuwa hawa viongozi ni binadamu wenzetu kweli?
Idije ikawa tunawaona binadamu kwa macho ya kawaida kumbe sio binadamu wa kweli!
 
Hao ni watu wa "State Capture." Ikumbukwe kuwa Climate Change is a falsified agenda ya NWO,kwa hiyo agents wa NWO lazima wahudhurie kwa wingi ili ionekane kwamba inaungwa mkono.
Yaa naona hizi ishu za climate change, pandemic (covid), cyberattack wale jamaa wa agenda 2030 wanazichukulia kama agenda zao za kutaka kuleta mabadiliko mbalimbali kwenye mifumo ikiwemo kutoa utambulisho kwa kila mwanadamu (unique ID), wanasema 'you will own nothing and be happy' na kwamba watu watakuwa wanakula wadudu.......hatari sana hawa watu.​
 
Back
Top Bottom