Swali kwa pesa za nssf

Unaweza kabisa kuchukua mafao yako ya NSSF hata kama hujaacha kazi, cha msingi tu kama sehemu unayofanyia kazi wafanyakazi wapo NSSF na wengine PPF wewe omba kubadilisha mfuko wa hifadhi kutoka NSSF kwenda PPF ukishafanya hivo hela zako za NSSF unachukua bila tatizo sisi hapa kazini ndo mtindo unaotumika hapa kazini though sijafahamu kama unapewa hela yako kabla ya miezi sita au baada ya miezi sita lakni uwezekano wa kuchukua ela yako kabla ya kustaafu, kuresign au kuachishwa kazi upo ndugu yangu

Ok unaweza kubadili mfuko lakini kubadilisha mfuko sio sawa na kuzichukua pesa zako, najua labda mnasema kuwa mnabadili lakini hamfanyi hivyo nawashauri muwe waangalifu kwenye hilo maana kuna element za fraud hapo, pia nadhani utakuwa umevunja ule mda ambao unatakiwa uwe umechangia mfuko ili kupata mafao unapostaafu, ila kama hautakuja kuyataka hayo mafao wakati wa kustaafu hili labda sio tatizo.
 
sorry Kang hivi kuna mtu ambaye anataka apewe milioni 1 - 10 leo au baada ya miaka tuseme 40 ijayo? kweli unaona thamani italingana? na kwanini hawaipi interest hii hela yetu wakati wao wanajengea maghorofa na kupangisha na kujilipa mamishahara makuubwa. tatu kuna ubaguzi sana wanakopesha nadhani watu wengine ila sio sisi wanyonge. Mradi ni akiba tu nimeamua mwenyewe niitumie sasa au la sioni kama ni fraud.
 
Edit: Wewe ndo hujui, soma sheria nimeiweka chini, PYUMBAVVVV...

Mwalimu wako anapata tabu sana kukuelewesha,kama haujui ni vyema kukaa kimya na sio kupotosha,
nani aliokwambia hauwezi kujitoa nssf mpaka umri wa kustaafu ufike? Jipange wewe kila•za
 
Ninavyoelewa NSSF hauwezi kujitoa, na hauipati hiyo hela hata kama kukiacha/kuachishwa kazi ni mpaka ufikie umri wa kustaafu ndipo utaanza kupata malipo kwa mpango details zaidi zipo kwenye website yao.
Ungekuwa unaweza kujitoa ingepoteza maana yote ya NSSF, kwa sababu inategemea mchango wako kuwalipa wastaafu wa sasa na wewe ukistaafu utalipwa na mchango wa vizazi vijavyo (unless mpango mzima u-collapse huko mbeleni :A S-cry: ).

Weh! usiombee hii kitu icollapse huko mbele, tutacollapse wengi maana kuna chenji yetu nyingi sana kule, hapa nilipo nasubiri nifikishe miaka yangu 55 nistaafu nivute chenji yangu.

Halafu mkuu uloanzisha mada, watu wanapewa chenji yao ukishaacha au kuachishwa kazi ila inabidi usubiri baada ya mienzi sita. au labda tu kama unaondoka nchini kabisa hurudi au unaenda kusoma unaweza kupewa chap chap ! mambo mengine tembelea ofisi zao watakujuza zaidi.
 
Mwalimu wako anapata tabu sana kukuelewesha,kama haujui ni vyema kukaa kimya na sio kupotosha,
nani aliokwambia hauwezi kujitoa nssf mpaka umri wa kustaafu ufike? Jipange wewe kila•za

Kweli wewe tube-light! yaani na sheria umewekewa bado unabisha? Ignorance is bliss!!
 
sorry Kang hivi kuna mtu ambaye anataka apewe milioni 1 - 10 leo au baada ya miaka tuseme 40 ijayo? kweli unaona thamani italingana? na kwanini hawaipi interest hii hela yetu wakati wao wanajengea maghorofa na kupangisha na kujilipa mamishahara makuubwa. tatu kuna ubaguzi sana wanakopesha nadhani watu wengine ila sio sisi wanyonge. Mradi ni akiba tu nimeamua mwenyewe niitumie sasa au la sioni kama ni fraud.

Yote unayosema yana ukweli, hasa hilo la interest maana social security za nchi nyingi zinakusanya interest, lakini sheria ndo inaamua nini ni fraud.
 
Back
Top Bottom