Susy kafiwa na Dada yake leo asubuhi

Habari za Asubuhi,

Kwa wale watakaopenda kwenda kwenye msiba tafadhali wani PM kwa maelekezo zaidi.

Regards

DA
 
Nimepokea taarifa leo asubuhi kuwa member mwenzetu Susy amefiwa na Dada yake aliyekuwa akiishi Gongo la mboto.

Msiba huo umetokana na madhara ya mabomu yaliyotokea gongo la mboto.

Taarifa za msiba ulipo nitawafahamisha hapo baadae.

Bwana alitoa Bawana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.

DA
Manabii waliopata kuishi katika ii dunia wamepita,ili litimie lile neno lilitoka mbinguni,likisema ''kila nafsi iliyopata kuishi itaonja mauti". Imenibidi niyaseme hayo ili mwanajamvi mwenzetu ajue kufiwa sio jambo jipya bali ni jambo lililokuwepo tangu enzi na enzi za mababu na mabibi zetu.bwana ametoa na bwana ametWAA,MUNGU AILAZE ROHO YA MArehemu mahali peponi. na wote tuseme aamenii!!
 
My heartfelt condolences to you Susy!
Mungu wa Israel ndiye mfariji mkuu!
Endelea kumtumaini yeye!
Zaidi sana mpe yeye sifa!
 
pole susy na wote mnaohusika na msiba huo...mungu awape nguvu pia ya kuwadai fidia hao wanaojifanya nchi yao na wanaolinganisha thamani ya pesa na uhai wa mwanadamu
 
Samahani sana mpendwa
kwa kuchelewa kukupa pole
Pole sana dada Sussy
Munguawe pamoja nawe na familia
yako kwa wakati huu..Jua kwamba ameenda
mahali pazuri,pa amani kuliko hii dunia..
Kaenda nyumbani na ipo siku utamuona tu..
be strong we are all here for you my dear..

Sante sis kwa
taarifa ubarikiwe..
 
Pole sana Suzy kwa msiba uliopata ,Mungu awape faraja ya kweli wewe na familia yako,
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Libarikiwe
 
Poleni familia ya susy. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu. RIP dada yetu!
 
Yaani kuingia tu MMU nakutakana na habari mbaya, khaaaa!:disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed:
Pole sana dada Susy
 
Back
Top Bottom