Suruali Imeniaibisha Kwenye Daladala.....!!

Dah! hii kitu inaboa sana aisee, kuna siku nilikuwa ukweni, sasa katika kujifanya kuwaimpress wakwe nikajifanya nimesomea karate, kumbe bamkwe na yeye alipitia hako kakozi lakini ananichora tu. Mara akaniambia nipige side kick aone, mzembe ile kuruka nikafyetuka na suruali ikakwapuka na mbaya zaidi nikateguka shingo. Yule mamkwe ili kunipa moyo nisijiskie nishai akajidai, "Kumbe tukivamiwa na wizi tukupigie simu wewe tu bamkwe wala hatuna haja ya kuwahi polisi".

klorokwini bwana...aha ha ha ha..
 
Last edited by a moderator:
Hivi mchina hakuleta sarawili za kiume stretch able? Manake sie tunavyobanwaga, kusingekuwa na stretch materials tungetoka damu ama vidonda, mweh!
 
za buku mbili Karume then unaenda kuipunguza kwa fundi wako sh 400. Polen cna
 
Leo asubuhi nawahi zangu kwenye majukumu ya kila siku nimekumbwa na balaa.
Nilipokuwa napanda katika daladala ghafla suruali ikaachia(ikatatuka) kuanzia usawa wa maungio ya miguu mpaka usawa zip inapoanzia. Mbaya zaidi nilikuwa nimechomekea, sikushuka hadi kituo cha mwisho konda aliponiazima sare yake nikavaa kwa muda wakati fundi akinirekebishia hii iliyotatuka
Hata ofisini sikuenda tena.....

Una umri gani?Usije kuwa na old skuli afu unatuiga vijana kupiga model!!! Haha zina wenyewe modo ndugu yangu usizivamie zitakuumbua hahah
Pole lakini my brother..
 
pole sana kaka! Ishamtokea rafiki yangu ofisini alipoinama kuokota karatasi ni soo! Mbele kulikuwa na wateja
 
Duh! Hii ni balaa, pole sana mkuu kwa yaliyokukuta. Umenikumbusha siku niliyotumbukia kwenye mtaro wa maji machafu maeneo ya soko kuu wakati nikishangaa wowowo la mwanadada mrembo aliyekuwa akikatiza barabarani.
 
Una umri gani?Usije kuwa na old skuli afu unatuiga vijana kupiga model!!! Haha zina wenyewe modo ndugu yangu usizivamie zitakuumbua hahah
Pole lakini my brother..
Ha ha ha aaah!! Mtundu Kisu sikuweka manjonjo yoyote katika kuvaa nia ajali tu ya kawaida.
 
Last edited by a moderator:
kwani hyo iliyochanika sh. Ngap? Na itakuwa fundi aliye ipunguza kaibana sana. Bt pole cna kwa dhahma
Loy MX sio ya buku mbili, sijaivaa tena baada ya kurudi nyumbani natafuta mtu wa kumkabidhi...
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom