Sura za hawa watu hazifanani na kutungua helikopta

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,058
"Nitawashughulikia hata maaskari wanaobambikia watu kesi hovyo hovyo hakika sitawaangusha. Kama niliweza kusimamia sheria nikiwa waziri tu, sasa niwe rais kabisa...hiiiiiiiiii...(vicheko vya wananchi wa Mara vilisikika)."
Hiyo ilikuwa ni kauli ya Mhe.

Magufuli alipokuwa katika moja ya mikutano yake mkoani Mara. Sasa juzi juzi hapo kumekuwa na tukio la kutunguliwa kwa ndege ya doria huko Maswa jambo lililozua utata mkubwa sana na huzuni kuu kwa Watanzania na Waingereza kwa kuwa rubani huyo alikuwa raia wa Uingereza.

Kuanzia siku ya juzi kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusiana na kukamatwa kwa walioitwa watuhumiwa wa ujangili na utunguaji wa ndege hiyo. Nimejaribu kuperuzi na kufanya mawasiliano ya kina kutoka kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi na nimepata taarifa kuwa kulikuwa na upekuzi wa nyumba baada ya nyumba ikiwemo vitisho vya hapa na pale kwa wananchi kusudi wawataje watu wanaowahisi kuwa majangili au wamiliki wa silaha kinyume cha sheria.

Hofu yangu kuhusiana na waliokamatwa ni kwamba, isijekuwa ni FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE ya jeshi la polisi kwa lengo la kutaka waonekane wanafanya kazi kwa kukamata kamata hata wanyonge wasiokuwa na hatia. Ukitazama vema sura za waliokamatwa hazifanani kabisa na uwezo, maarifa na ujuzi wa kutungua ndege japokuwa yawezekana mmoja au watatu kati yao walishiriki.

Ikiwa wana makosa mengineyo sawa lakini si vema kumhusisha kila raia anayekaa na hifadhi na suala la utunguaji wa ndege.Natoa rai kwa jeshi la polisi kuchunguza kwa umakini jambo hili na kuhakikisha wanakamatwa majangili wa kweli na siyo wanyonge wanaowinda nguruwe pori kwa ajili ya kitoweo.
watunguaji-jpg.322518
 
Attachments

  • WATUNGUAJI.JPG
    WATUNGUAJI.JPG
    104.5 KB · Views: 294
"Nitawashughulikia hata maaskari wanaobambikia watu kesi hovyo hovyo....hakika sitawaangusha. Kama niliweza kusimamia sheria nikiwa waziri tu, sasa niwe rais kabisa...hiiiiiiiiii...(vicheko vya wananchi wa Mara vilisikika)."
Hiyo ilikuwa ni kauli ya Mhe. Magufuli alipokuwa katika moja ya mikutano yake mkoani Mara. Sasa juzi juzi hapo kumekuwa na tukio la kutunguliwa kwa ndege ya doria huko Maswa jambo lililozua utata mkubwa sana na huzuni kuu kwa Watanzania na Waingereza kwa kuwa rubani huyo alikuwa raia wa Uingereza.
Kuanzia siku ya juzi kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusiana na kukamatwa kwa walioitwa watuhumiwa wa ujangili na utunguaji wa ndege hiyo. Nimejaribu kuperuzi na kufanya mawasiliano ya kina kutoka kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi na nimepata taarifa kuwa kulikuwa na upekuzi wa nyumba baada ya nyumba ikiwemo vitisho vya hapa na pale kwa wananchi kusudi wawataje watu wanaowahisi kuwa majangili au wamiliki wa silaha kinyume cha sheria. Hofu yangu kuhusiana na waliokamatwa ni kwamba, isijekuwa ni FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE ya jeshi la polisi kwa lengo la kutaka waonekane wanafanya kazi kwa kukamata kamata hata wanyonge wasiokuwa na hatia. Ukitazama vema sura za waliokamatwa hazifanani kabisa na uwezo, maarifa na ujuzi wa kutungua ndege japokuwa yawezekana mmoja au watatu kati yao walishiriki. Ikiwa wana makosa mengineyo sawa lakini si vema kumhusisha kila raia anayekaa na hifadhi na suala la utunguaji wa ndege.
Natoa rai kwa jeshi la polisi kuchunguza kwa umakini jambo hili na kuhakikisha wanakamatwa majangili wa kweli na siyo wanyonge wanaowinda nguruwe pori kwa ajili ya kitoweo.
Kwani sura za watunguaji helicopter zinafananaje mkuu???...
 
Si kila mmoja aweza kuitumia lugha ya mwili kujenga nadharia fulani, kwa kuwa nina uzoefu wa kukaa karibu na mbuga nina experience ya kuona maofisa wa wanyamapori kwa kushirikiana na jeshi la polisi wakitumia nguvu kubwa kuwashurutisha wananchi wanaokaa karibu na hifadhi au mbuga kutoa taarifa hata kama hawanazo.
Ndege ilikuwa inafanya doria na hakuna maelezo ya awali kwamba ati hao watu walikuwa wanawindwa wakamatwe na waendesha doria. Laiti kama kungekuwa na zoezi la kurushiana risasi angalau ingeleta mantiki fulani. Mimi ninaona kama kuna siri iliyofichika nyuma ya pazia. Pamoja na hayo bado ninabaki na swali la ilikuwaje rubani mwingereza na siyo Mtanzania?
 
Kama huyo mwenye shati la urujuani??Hapo wahusika wapo kitaa walala hoi ndio wanakamatwa...Ujangiri wa tembo haufanywi na watu masikini
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Ukweli utajulikana tu, Tafadhali tuwaachie polisi na vyombo vinavyohusika vifanye kazi zake bila kuingiliwa kwani uharifu uliofanyika ni mbaya sana kwa nchi yetu
 
Nasikia watu wanajiita wahifadhi wa mazingira,walinzi wa wanyama,kumbe ni mbinu tu za kwenda kwenye mbuga za wanyama,kuanzisha terrorist camps to destabilze neighbouring countries. Ndege inadaiwa kutunguliwa na mfanyakazi wa Ngorongoro,maybe those people know something that we don,t know kuhusu hawa watu wanaosema wanataka kuwalinda wanyama. World Wildlife Fund na T.I.,Transparency International zote ni kazi ya Prince Philip,zimeanzishwa James Wolfenson alipokuwa rais wa World Bank,nazo hazikuanzishwa kwa aababu zinazofikiriwa. World Bank na IMF walikuwa wanatafuta scapegoat kuelezea kwa nini nchi za Afrika hazipati maendeleo. Ikaamuliwa kwa viongozi ""mafisadi"" ndio wanaozuia maendeleo Afrika,kwa sababu wanazichukua hela zote za msaada.Kumbe matatizo ni riba za World Bank na IMF. Kwa hiyo wameanzisha TI,pia they are preoccupied with preserving forests and protecting animals,kwa sababu they have a depopulation agenda,they strongly believe that the population of the world should never hsve been permitted to go beyond half a billion. Hey,hapa naona activity sana ya ndege za ngerengere,tokea siku ile Magufuli aliposema uchaguzi urudiwe Zanzibar. Nadhani hizi ndege zote zinaenda Pemba.
 
UncleBen: Wengine walihukumiwa kabla ya hakimu kutoa hukumu rasmi hivyo waligaragazwa chini ipasavyo. Bila shaka wengine walichukuliwa mashambani wakipalilia mihogo!
Nimekuelewa vizuri mkuu ,ngoja tuone mwisho wake utakuaje
 
"Nitawashughulikia hata maaskari wanaobambikia watu kesi hovyo hovyo....hakika sitawaangusha. Kama niliweza kusimamia sheria nikiwa waziri tu, sasa niwe rais kabisa...hiiiiiiiiii...(vicheko vya wananchi wa Mara vilisikika)."
Hiyo ilikuwa ni kauli ya Mhe. Magufuli alipokuwa katika moja ya mikutano yake mkoani Mara. Sasa juzi juzi hapo kumekuwa na tukio la kutunguliwa kwa ndege ya doria huko Maswa jambo lililozua utata mkubwa sana na huzuni kuu kwa Watanzania na Waingereza kwa kuwa rubani huyo alikuwa raia wa Uingereza.
Kuanzia siku ya juzi kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusiana na kukamatwa kwa walioitwa watuhumiwa wa ujangili na utunguaji wa ndege hiyo. Nimejaribu kuperuzi na kufanya mawasiliano ya kina kutoka kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi na nimepata taarifa kuwa kulikuwa na upekuzi wa nyumba baada ya nyumba ikiwemo vitisho vya hapa na pale kwa wananchi kusudi wawataje watu wanaowahisi kuwa majangili au wamiliki wa silaha kinyume cha sheria. Hofu yangu kuhusiana na waliokamatwa ni kwamba, isijekuwa ni FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE ya jeshi la polisi kwa lengo la kutaka waonekane wanafanya kazi kwa kukamata kamata hata wanyonge wasiokuwa na hatia. Ukitazama vema sura za waliokamatwa hazifanani kabisa na uwezo, maarifa na ujuzi wa kutungua ndege japokuwa yawezekana mmoja au watatu kati yao walishiriki. Ikiwa wana makosa mengineyo sawa lakini si vema kumhusisha kila raia anayekaa na hifadhi na suala la utunguaji wa ndege.
Natoa rai kwa jeshi la polisi kuchunguza kwa umakini jambo hili na kuhakikisha wanakamatwa majangili wa kweli na siyo wanyonge wanaowinda nguruwe pori kwa ajili ya kitoweo.
Mkuu inayotungua helicopter ni Mikono kaka, sio sura.
 
Nasikia watu wanajiita wahifadhi wa mazingira,walinzi wa wanyama,kumbe ni mbinu tu za kwenda kwenye mbuga za wanyama,kuanzisha terrorist camps to destabilze neighbouring countries. Ndege inadaiwa kutunguliwa na mfanyakazi wa Ngorongoro,maybe those people know something that we don,t know kuhusu hawa watu wanaosema wanataka kuwalinda wanyama. World Wildlife Fund na T.I.,Transparency International zote ni kazi ya Prince Philip,zimeanzishwa James Wolfenson alipokuwa rais wa World Bank,nazo hazikuanzishwa kwa aababu zinazofikiriwa. World Bank na IMF walikuwa wanatafuta scapegoat kuelezea kwa nini nchi za Afrika hazipati maendeleo. Ikaamuliwa kwa viongozi ""mafisadi"" ndio wanaozuia maendeleo Afrika,kwa sababu wanazichukua hela zote za msaada.Kumbe matatizo ni riba za World Bank na IMF.
mkuu kwani ulikuwa unataka kuongelea nini hasa?

Riba au?

Ugaidi ?

Uhifadhi wa mazingira?

Alafu bro nilikuuliza swali hujanijibu...Umewahi kuvuta sigara ya aina yoyote..hasa sigara kali aina ya Bhange?
 
Back
Top Bottom