Sumaye Kung'oka CCM leo?

Status
Not open for further replies.

Watu

JF-Expert Member
May 12, 2008
3,231
1,470
Kukutana na waandishi wa habari leo saa 5.00 asubuhi katika hotel ya courtyard Hotel jijini dar es salaam

Source: Tanzania daima
 
hawezi kung'oka ccm hata iweje....anaendeleza tu nipasho yao na uvccm
 
WALA SI SUMAYE TU BALI KAJIULIZENI TU KWAMBA NI LINI WATU WAZURI WATAWAONDOKENI CHAMANI

Wewe kwa mtaji wa hizi zengwe, fitina na uchuro wa Lowassa kwa wenzie wenye kuona mbali na nchi hii bado unafikiri tu mtu kubaki humo kwenye ajizi nyumba ya njaa CCM???

Cha msingi jiulize tu kwamba watu wazuri na wenye upeo wa hali ya juu kama Wazee Sinde Warioba, John Malecela, Salim Ahmed Salim na wengine wengi tu lini wanakiondoka hicho chama kilichoingiliwa na Mchwa ikulayo hadi chuma kwa maana ya JK, Rostam Aziz pamoja na Edward Lowassa.
 
Doh safi sana! i new Edward Lowassa is not the only candidate,

MHHH??SIDHANI KAMA SUMAYE ANATAKA URAISI ILA NAFIKIRI NI MMOJA YA WATU MAKINI WALIOBAKI CCM AKITANGAZA KUONDOKA NITAFURAHI SANA
aje CDM ananafasi na bado ana nguvu
 
Tusubiri azungumze hiyo saa tano wala siyo mbali.lakini lililo la uhakika sana ni kwamba hawezi kuondoka CCM!
 
Nadhani anataka kujibu hoja za uvccm. Hv hawa uvccm n kina nani? Mbona wanasiasa za 1947? Umbea tu umewajaa!
 
MHHH??SIDHANI KAMA SUMAYE ANATAKA URAISI ILA NAFIKIRI NI MMOJA YA WATU MAKINI WALIOBAKI CCM AKITANGAZA KUONDOKA NITAFURAHI SANA
aje CDM ananafasi na bado ana nguvu

Watu wakini?
Hivi sio huyu nilisikia enzi hizo alivo maliza mda wake kuwa ana trilion11 ambazo haijulikani zilipo?
Leo msafi au kwa kuwa alikaa kimya mda mrefu?

Ngoja arudi tena,niliambiwa hata kama huwajui wazazi wako ingia kwenye siasa,watu wanajua kila kitu kuhusu wewe na utakisikia!!!!
 
Hakuna kitu hapo,

Ni usanii tu, tena wa kiwango cha chini kabisa. Inatia kichefuchefu!
 
MHHH??SIDHANI KAMA SUMAYE ANATAKA URAISI ILA NAFIKIRI NI MMOJA YA WATU MAKINI WALIOBAKI CCM AKITANGAZA KUONDOKA NITAFURAHI SANA
aje CDM ananafasi na bado ana nguvu

Kweli ukipenda hata chongo huoni, leo hii Sumaye amekuwa mtu mzuri. EPA ilianzia kipindi cha Sumaye, Kiwira mzee BWM alijiuzia kipindi cha sumaye, ubadhirifu mkubwa wa fedha za STABEX kwa ajili ya kilimo kilifanyika kipindi cha Sumaye ( refer skendo la Waziri Keenja wakati ni waziri wa kilimo)
 
sumaye nae mchafu tu,mi simuoni msafi hapo,acheni kumpigia chapuo!kwani wakulima wa mvomero waliporwa mashamba na nan?
 
Kweli ukipenda hata chongo huoni, leo hii Sumaye amekuwa mtu mzuri. EPA ilianzia kipindi cha Sumaye, Kiwira mzee BWM alijiuzia kipindi cha sumaye, ubadhirifu mkubwa wa fedha za STABEX kwa ajili ya kilimo kilifanyika kipindi cha Sumaye ( refer skendo la Waziri Keenja wakati ni waziri wa kilimo)

Sitashangaa Lowasa 2015 akiitwa malaika na chaguo la Mungu!

Watanzania wanakipaji cha kukumbuka mambo ndani ya week moja tu,wakidanganywa na vikauli vya kuonesha mafisadi wapo pamoja nao wanasahau haraka sana!
 
hasa huu mradi wake wa Loliondo unamjenga sana kisiasa. Ndo maana Mtanzania na magazeti mengine uchwara hayaishi kuhubiri ya Loliondo. Wenye akili, macho na masikio tunafuatilia kwa makini, tunaona na kusikia vema.

tunasubiri tu siku ya loliondo yatakapoanza kutumika kama turufu ya kisiasa. time will always tell
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom