Sugu ndani ya mjadala wa katiba

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
MBUNGE wa Mbeya Mjini,
Joseph Mbilinyi (CHADEMA), amesema sheria ya uchaguzi katika nafasi za mameya na wenyeviti wa halmashauri nchini ina kasoro hivyo haipaswi kupewa nafasi katika Katiba mpya.

Alisema kitendo cha kundi la watu wachache (madiwani) kuwa na uwezo wa kisheria kumsimamisha kiongozi anayeenda kutetea maslahi ya watu wote hata wasio na vyama hakipaswi kupewa nafasi katika Katiba mpya ambayo moto wa kuidai kuandikwa upya umepamba moto kila kona ya nchi
 
Sikubaliani na Sugu katika hili.

Madiwani ni wawakilishi wa wananchi wa kata zilizopo kwenye wilaya husika, hivyo sio vibaya kwao kumchagua Meya au Mwenyekiti miongoni miongoni mwao kwa niaba ya wananchi waliowachagua.

Lakini sikubaliani kabisa na utaratibu wa sasa wa kuwaruhusu Wabunge wa Viti Maalumu kushiriki kwenye uchaguzi huo, huku ni kuwanyang'anya wananchi sauti ya uwakilishi wao walioufanya kupitia uchaguzi, hili ndilo linalopaswa kufanyiwa kazi.
 
Haipaswi kupewa nafasi au ionapaswa kupewa nafasi na marekebisho??????haijakaa sawa hiyo haya ni maneno ya Sugu au ya kwako Speaker?rekebisha hiyo haieleweki
 
Hapo kwenye RED kama upeo wako wa kufikiri ni finyu kiasi hicho, je unaonaje na rais akichaguliwa na wabunge kwa niaba yetu? maana kumbuka wabunge ni wawakilishi wa majimbo yetu.
 
SOS Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo,kinachoongelewa hapo ni kuwa sheria iliyopo ya uchaguzi wa mameya ina kasoro na haipaswi kupewa nafasi katika katiba mpya.Maana yake sheria hii haifai na irekebishwe ili iendane na katiba mpya.
 
MBUNGE wa Mbeya Mjini,
Joseph Mbilinyi (CHADEMA), amesema sheria ya uchaguzi katika nafasi za mameya na wenyeviti wa halmashauri nchini ina kasoro hivyo haipaswi kupewa nafasi katika Katiba mpya.

Alisema kitendo cha kundi la watu wachache (madiwani) kuwa na uwezo wa kisheria kumsimamisha kiongozi anayeenda kutetea maslahi ya watu wote hata wasio na vyama hakipaswi kupewa nafasi katika Katiba mpya ambayo moto wa kuidai kuandikwa upya umepamba moto kila kona ya nchi

sawa na safi sana sugu sio hiyo tu hata nafasi za wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wawe ni waajiliwa wa serikali sio wawe viongozi wa kisiasa au ziwe ni nafasi za kuomba au parliamentary confirmation posts tunahitaji tuwe na wasomi kama wakurugenzi katika wilaya zetu
 
Haileweki vizuri, nitauungana na mh. Sugu iwapo atasema hivi mfumo kuwa kuchagua meya ubadilishwe ili mameya wachaguliwe na ili wawajibike zaidi kwa wananchi. Huu mfumo wa kuwaachia madiwani wachague mameya ndiyo chanzo cha matatizo mengi yanayaozikabili halmashauri za miji.
 
Hapo kwenye RED kama upeo wako wa kufikiri ni finyu kiasi hicho, je unaonaje na rais akichaguliwa na wabunge kwa niaba yetu? maana kumbuka wabunge ni wawakilishi wa majimbo yetu.

Kama u mtu mwenye fikra yenye "dimension-moja" bila ya shaka una haki ya kuona hivyo, keep it up!!
 
mbunge wa mbeya mjini,
joseph mbilinyi (chadema), amesema sheria ya uchaguzi katika nafasi za mameya na wenyeviti wa halmashauri nchini ina kasoro hivyo haipaswi kupewa nafasi katika katiba mpya.

Alisema kitendo cha kundi la watu wachache (madiwani) kuwa na uwezo wa kisheria kumsimamisha kiongozi anayeenda kutetea maslahi ya watu wote hata wasio na vyama hakipaswi kupewa nafasi katika katiba mpya ambayo moto wa kuidai kuandikwa upya umepamba moto kila kona ya nchi

nafikiri kama madai haya kweli yalitolewa na sugu basi asome zaidi sheria za serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na kazi za baraza la madiwani sambamba na bunge kwa serikali kuu
 
Back
Top Bottom