Sugu aendelea Kutikisa Chunya, achambua Katiba kama Mhadhiri wa Chuo Kikuu. Wananchi waanza kumuelewa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,423
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema , Joseph Mbilinyi bado yuko Chunya kwa ziara ya kikazi, ambako ameendelea kuelimisha Wananchi kuhusu Umuhimu wa Katiba Mpya ambayo itazaa Tume huru ya Uchaguzi.

Sugu ambaye sasa anajulikana pia kama Jeshi la Mtu mmoja, anashangaza wengi kutokana na uwezo wake wa kuichambua Katiba ya Tanzania mithili ya Wahadhiri wakubwa wa Vyuo vikuu, hakika huyu jamaa ameiva.

Balaa zaidi ni uwezo wake wa kuuchambua Mkataba mbovu wa Bandari utadhani yeye ndio Mbarawa mwenyewe kutoka Kisiwandui.

Mambo yalikuwa hivi na hapa ni kata ya Lupa

Screenshot_2023-09-04-20-12-18-1.png

Screenshot_2023-09-04-20-12-22-1.png

Screenshot_2023-09-04-20-12-26-1.png

Wachambuzi wa Siasa wanaiona Chadema kama chama kilichoiva na kinachoaminiwa na wananchi kutokana na uwezo wa viongozi wake.

Bali kinachofahamika ni kwamba , hakuna kiongozi wa CCM au hata wabunge wake wanaoweza kuitisha mkutano wa hadhara ukahudhuriwa na umati bila msaada wa viongozi wa kitaifa.
 
Duh watu ni wengi knoma kwa haraka haraka wanaweza kufika 2k hapo, hakika chadema ni mpango wa mungu
 
Sugu moto chini.......... Aa aah..

Mkuu Erythrocyte, naona Huwa unaripoti Taarifa za CDM toka Kona mbali mbali za nchi. Wewe ndio afisa habari wa Sasa? Au una coordinate wapasha habari wasio rasmi?

All in all, imeshashauriwa humu,.CDM iwe na Media yake Sasa pamoja na Media people kama @erythrocite kwa ajili ya publicity. CDM ni taasisi haipaswi kuhabarika kwa style ya UDAKU
 
Unaposema udaku una maana huamini taarifa tunazozileta ? kwanza mimi si ofisa habari wa chadema , mdau tu wa siasa
 
Back
Top Bottom