Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa

Violet ukweli upo palepale inawezekana mzazi wako mmoja au wote hawana msimamo kabisa wa dini yao/zao,
nasema hivyo kwa sababu hizi dini mbili ni tofauti kabisa, ni dini ambazo zinapingana sana, kwa hiyo mwenye imani yake thabiti ya dini hizo hawawezi kukaa pamoja

...hata kama wamependana kiukweli ukweli?

Naamini uwezekano wa interfaith marriages nikinukuu;

Believers, jews, sabaeans or Christians-whoever believe in god and the last day and does what is right-shall have nothing to fear or regret- Quran
 
mi sikubaliani na wewe hata kidogo,hizo ni hadithi tu za kufikirika,mi baba yangu ni muislam na mama yangu ni mkristo na ni mdini kweli kweli na wapo kwenye ndoa yao zaidi ya miaka 40....kwa ushahidi huu wa wazazi wangu unafikiri mi ntakuunga mkono?

Mtiti naomba nikuunge mkono...hatupaswi kurithishwa dini...ukweli mtu autafute mwenyewe. "independent investigation of the truth"! binafsi wazazi wangu walini expose kwa mafundisho ya dini 3 tofauti...nilipotimiza miaka 17 niliamua kuwa mfuasi wa dini ambayo nipo sasa. wazazi wangu walioana wakiwa ni waumini wa dini 2 tofauti.

mafundisho ya kiroho kwa dini zote ni sawa, kinachobadilika is the social teachings of a religion tu!
 
naona mletaji hoja ameangalia upande mmoja wa shilingi na kashindwa kujiuliza je wale ambao wameweza kutunza ndoa zao kama mfano wa violet wamewezaje? ndoa kwa watu wa dini mbili tofauti inawezekana kutokana na nyie wawili imani yenu hiko vipi katika dini zenu.mambo maovu mengi yametokea duniani pande za dini zote kupitia viongozi wao kiasi cha kwamba watu nao imani hipo lakini haina nguvu ya kuendesha maisha yao kama zamani.watu sasa hivi hawatenganishwi na dini hata siku moja kwenye swala la mapenzi.na je hizo ndoa za dini moja ambazo hazidumu mbona hamzichambui? ndoa nyingi zipo za dini tofauti na zimedumu mda mrefu fanya utafiti mleta hoja na utagundua hilo.
watu wote tuna amini ka jina la mungu na tuendelee kutenda mambo mema kwa watu wote lakini sio swala la kuanza kujitenganisha.wewe nenda kanisani na mwenzako ataenda msikitini mkirudi nyumbani fanyeni mambo yaliowaunganisha kindoa.
hapa narudi kule kule kwenye swali moja, kama wewe ndoa yako na muislamu/mkristo mwenzako haina doa na ni nzuri kwanini unajisumbua na ndoa za watu wengine wawe wa dini moja au dini tofauti?
 
mi sikubaliani na wewe hata kidogo,hizo ni hadithi tu za kufikirika,mi baba yangu ni muislam na mama yangu ni mkristo na ni mdini kweli kweli na wapo kwenye ndoa yao zaidi ya miaka 40....kwa ushahidi huu wa wazazi wangu unafikiri mi ntakuunga mkono?

Nakubaliana nawe kabisa kwenye hili. Nazifahamu ndoa za miaka chungu nzima za Waislamu na Wakristo ambao pamoja na tofauti zao za kidini wameishi vizuri tu katika ndoa zao na kuheshimu tofauti zao za kidini bila matatizo yoyote. Na watoto pia wanakuwa wanafuata dini ambazo wazazi wameamua baada ya kujadiliana. Hamjasikia usemi kwamba Love can move mountains!? Mapenzi ya kweli huondoa tofauti ndogo ndogo zilizopo kama dini n.k. na wana ndoa wakaishi kwa raha na mustarehe ukiondoa wale mafundamentalist ambao hutaka kuzikuza tofauti za kidini pamoja na kuwa Mungu anayeabudiwa na wote ni huyo huyo.
 
Wakati nahudhuria mafundisho ya ndoa,muelimishaji alisema ndoa asili yake ni MUNGU,KWANI MUNGU ALIKUWA NA UWEZO WA KUUMBA WANAWAKE WENGI NA WANAUME WENGI LAKINI ALIUMBA MMOJA TU ILI WAOANE.....hivyo ndoa ni ya mtu mume na mtu mke tu.
Aliendelea kusema kuwa kuna ndoa mseto yaani mtu wa dini moja na wa dini nyingine na ili ndoa hiyo ifungwe ni lazima mmoja au yote kati ya haya yawepo..
1.Hakuna au watu wa dini hiyo ni wachache ktk eneo hilo.
2.Mtu huyo wa dini nyingine hatomkwaza mwenzake ktk Imani yake.
3.Watoto watakao zaliwa wafundishwe na kulelewa ktk imani ya dini ya pale atakapofungia ndoa.
Ktk mafundisho hayo alisema kuwa binti hawezi kuruhusiwa kufunga ndoa ktk imani hiyo kama wanatofauti kubwa ya imani,akatoa mfano MLOKOLE NA MUISLAM AU MKATOLIKI NA MUISLAM.
Hivyo basi ndoa ya dini tofauti inaweza kuwepo ilmradi tu usimkwaze mwenzako ktk imani yake dhidi ya kwako.
 
Tunaye muabudu wooote ni mungu mmoja basi dini ni kitu gani basi mbela za haki? Ndoa hufungishwa na mungu ila mungu hamchagulii mwanadamu mke au mume kwani ukiangalia alimchagulia adam mke na matokeo yake adam akamlaumu mungu kwa kumpa mke.....sasa ieleweke kuwa mungu ametupa nafasi ya kuchagua tukisha chagua yeye anabariki......matatizo katika ndoa yapo hata kwa wale waliopo katika dini moja.....mfano uliotolewa hapa wa mbuzi na ng'ombe hauna uhalisia wowote ule naomba utafutwe mfano mwingine......
 
nakua makini sana na hili, na mara nyingi nikiwa nafikiria kumtafuta wangu wa ubani na wa maisha huwa kigezo namba moja ni dini, sitaki kuwa mnafiki kwa hili, maana pia sitaki kuwaudhi wazazi wangu walionilea katika maadiloi ya kidini na kunielewesha ni vigezo gani vya kuangalia wakati wa kutafuta wangu wa maisha
 
Dini tofauti hazina maafa yeyote kwenye ndoa kama aliyoanzisha thread anavyodai...wengi ni product of that (mimi nikiwemo), I made my own choice baada ya kumaliza form six!. Any way wazazi wangu ni wondeful mimi sijaona tatizo lolote wanadunda life mpaka leo...bottom line kumheshima binadamu mwenzako! Mahitaji yetu yanafanana ...na ni ya msingi ..love, respect, and kuvumilia.
 
Kwani hapa mnamaanisha dini sawa au imani sawa,kama mnazungumzia dini basi hapa mtakuwa mnakosea sana,sababu imani ni unachoamini,kama wote mnamwamini Mungu haijalishi mnamuamini kwa dini gani!!
 
Nimekupa thanks (pdidy) ila haimaanishi kuwa sikupingi. Ukiamini katika huo mfano utahofia kutoa changamoto. Kuna sababu ya kufungwa nira na mtu asiyenisisimua? Just b'se tuko dhehebu moja? Maisha yenyewe ni probability. Hatuishi ktk ndoa kwa lengo la kuzaa tu. Biblia inasema, kama utashindwa kujizuia basi oa! Vyanzo vya maafa ktk ndoa ni vingi ikiwapo nyumba ndogo ilhali mmefungwa nira moja. Ndoa ni sanaa wala si kanuni.
 
mi sikubaliani na wewe hata kidogo,hizo ni hadithi tu za kufikirika,mi baba yangu ni muislam na mama yangu ni mkristo na ni mdini kweli kweli na wapo kwenye ndoa yao zaidi ya miaka 40....kwa ushahidi huu wa wazazi wangu unafikiri mi ntakuunga mkono?

Bravo!
Ni mawazo mgando kufikiria kuwa ndoa nzuri au yenye amani na ya kudumu ni ya watu wenye imani moja tu. In fact zipo ndoa nyingi za watu wa namna hiyo (imani moja) ambazo zimejaa matatizo. Wakati huo huo, wachache tunaowafahamu ambao wameoana ndani ya imani tofauti, ndoa zao zimekuwa imara tu hasa kutokana na kujiweka karibu kwa wanandoa hao kwa sababu pande mbili za wazazi pamoja na jamii kwa ujumla zinakuwa kama zinawalaumu waliooana na kutegemea kuwa ndoa itavunjika. Wanandoa wanapojua hisia hizi, hujiweka karibu zaidi na ndoa inazidi kuwa imara.
 
Sure,

Dini tofauti zina matatizo yake katika ndoa.

Come to think of it, culture tofauti zina matatizo yake katika ndoa, kwa hiyo usioe tu mtu wa dini yako, bali hakikisha pia awe wa culture yako.

On the same token, hata political views tofauti zinaleta matatizo katika ndoa, kwa hiyo hakikisha si tu unaoa mtu wa dini na culture yako, bali pia awe wa political views zako.

When you examine things closely, hata income bracket za familia na background nazo zinaleta clash katika ndoa, utaoaje mtu ambaye haelewi dunia yako ilivyo, kwa hiyo hakikisha unaona katika income bracket na background yako pia, on top of dini, culture na political view.

Hey, you know what? I am sure there is a whole lot more incompatibility issues that could be raised in the same way, so why not cut to the chase. I will give you the best advise possible.

Why don't you skip the whole thing and marry yourself, surely there won't be any incompatibility issues between yourself and yourself, how about that huh?
 
lakini vipi Mlutheri na Mkatoliki kuna tatizo?
Hawa watu wanakaribiana sana, Lutherani na katoliki kuna mambo mengi tu ambayo yapo sawa, ijapo katoliki wanaamini ndoa ikifungwa kanisani kwao ndo ndoa, na ikifungiwa lutherani huamini kuwa si ndoa.

Hapo juu nilikuwa najaribu kukupa mwanga tu, ila muhimu ni kuliongelea suala la dini na mjue mtalichukulia je wakati wa stage za mwanzo kabisaa.

Katikati ya ndoa kugombana kisa dini haileti sense sabb kwani hukujua kama huyo uliyeko nae si dini yako labda useme tulikubaliana hivi then kanigeuka hapo kidogo logic inakuja bt otherwise umemchoka basi unatafuta nitoke vipi!
Ni hayo tu.
 
Tunaye muabudu wooote ni mungu mmoja basi dini ni kitu gani basi mbela za haki? Ndoa hufungishwa na mungu ila mungu hamchagulii mwanadamu mke au mume kwani ukiangalia alimchagulia adam mke na matokeo yake adam akamlaumu mungu kwa kumpa mke.....sasa ieleweke kuwa mungu ametupa nafasi ya kuchagua tukisha chagua yeye anabariki......matatizo katika ndoa yapo hata kwa wale waliopo katika dini moja.....mfano uliotolewa hapa wa mbuzi na ng'ombe hauna uhalisia wowote ule naomba utafutwe mfano mwingine......
I agree we all believe in one God but we don't believe in the same God.

Katika ndoa imani ina role sana wala hatuwezi kukataa, Kama wanandoa mnakua na dini moja inakua rahisi sana katika malezi ya watoto.

Tunajua kwamba chanzo ta taifa bora ni familia zilizo imara, chanzo cha kanisa bora ni familia zilizo bora na chanzo cha msikiti bora ni familia zilizo imara, huu ni ukweli ambao haupingiki. Mara nyingi tunasema watoto ni taifa la kesho lakini tunashindwa kuweka msingi imara kwa taifa hili.

Imani yenu ikiwa moja, inasaidia sana kuleta umoja na mshikamano katika malezi ya watoto.

Hili ni muhimu sana kwani mara watoto wanakua na reference moja wakijua nini kifanywe na nini kisifanywe. Dini zinapotofautiana watoto wanabaki kuchanganyikiwa kwa sababu baba anakua anakataza hili wakati mama analiruhusu or viceversa. Mchanganyiko huu hauwajengi watoto bali unakua unaleta shida na matokeo yake ni watoto wasio kua na msimamo katika dini yeyote.

Wengine wanasema watoto wengine watakua na dini moja na wengine nyingine. Hivi motto mmoja anapotoka madrasa na mwingine ametoka Sunday School inakuaje, kinaeleweka kweli katika hiyo nyumba? Watoto wanavyozidi kukua watakuja na maswali mengi tu sasa wanapokua na maswali kuhusu dini mnawajibu nini?

Just Imagine mkristo Mlokole na mwislamu wanaoana, hivi wanakaaje katika hiyo ndoa? Mwislamu anapotaka kuchoma Ubani na Kuzikiri, Huyu mkristo au Mlokole anakua amekaa wapi saa hizo, na Mlokole anapotaka kuimba pambio na kuomba mwislamu anakua amekaa wapi saa hizo. Haya siku Mkristo akipata hamu ya kutafuna kiti moto inakuaje katika hiyo nyumba? (Ingawa sio kitu muhimu sana kwa sababu anaweza kuacha kula kwa sababu ya ndoa).

Hivi vitu kwa kweli haviwezi kuchangamana kabisa, sijui Quran inasemaje katika hili lakini Biblia iko wazi na dhahiri kwamba Sahihi kufunga nira na mtu asieamini.

Unless nyie wanandoa ni watu msiojali habariza dini, Lakini ndoa za dini tofauti hazifai kwa malezi bora ya watoto.

Don't go into marriage just to satisfy yourself, think beyond that , think about the family you want to build, think about the legacy you want to leave behind. The decision is I your hand you can choose and make the right decision. Lakini kwa wale ambao tayari wako kwenye ndoa hizo mseto basi hakuna cha kufanya inabidi uendelee nayo ila kwa wale ambao hawajaingia, Please think twice.
 
Inategemea mnavyoendekeza hizo imani zenu za dini, lakini naona haina mpango wala nini. Mambo yanayofanyika katika ndoa hisia zake ni zilezile, uwe na dini hii au ile.

Watu ndio wanaooana, dini hazioani. Uamuzi wa namna ya kuendesha mambo yao mbalimbali ni wa walioko kwenye hiyo ndoa, na si wa dini.

Kuendekeza dini ni kuendekeza ujinga tu, mijitu haifanyi kazi inawadai muwalipe wao 10% ya mapato yenu ati wakampelekee mungu, mnakubali! Wajinga ndio waliwao! Hivi kama mungu kweli ndiye aliyeumba kila kitu, hiyo 10% ya mapato ya mmachinga anaihitaji ya nini? Yaani mungu aliumba kila kitu halafu akashindwa kujitengea mwenyewe 10%, mpaka 'mchungaji' akubembeleze au akutishie ukampelekee? Ujinga!
 
Inategemea mnavyoendekeza hizo imani zenu za dini, lakini naona haina mpango wala nini. Mambo yanayofanyika katika ndoa hisia zake ni zilezile, uwe na dini hii au ile.

Watu ndio wanaooana, dini hazioani. Uamuzi wa namna ya kuendesha mambo yao mbalimbali ni wa walioko kwenye hiyo ndoa, na si wa dini.

Kuendekeza dini ni kuendekeza ujinga tu, mijitu haifanyi kazi inawadai muwalipe wao 10% ya mapato yenu ati wakampelekee mungu, mnakubali! Wajinga ndio waliwao! Hivi kama mungu kweli ndiye aliyeumba kila kitu, hiyo 10% ya mapato ya mmachinga anaihitaji ya nini? Yaani mungu aliumba kila kitu halafu akashindwa kujitengea mwenyewe 10%, mpaka 'mchungaji' akubembeleze au akutishie ukampelekee? Ujinga!


Du Mshikaji inaonekana 10% inakukera sana, Kama huna mpango na dini kama ulivyosema mwenyewe si uachane na kutoa hiyo 10%.?
Inakusaidia nin kutoa 10% halafu ukilala usiku unaweweseka kukumbukia hela zako ulizotoa?

Nakubaliana na wewe kua hisia za yanayofanyika katika ndoa ni zilezile uwwe na dini au usiwe na dini. Lakini nu lazima ku-Balance mambo yote kwa sababu si muda wote mnakua mna DO, Muda mwingi wa maisha yenu unakua mnashughuka na mambo mengine ambayo si ku DO. Sasa Endapo hayo mambo mengine yatawafanya msielewane hata hiyo mood ya ku DO sijui itatoka wapi.

Ushauri wangu ni kwamba usijenge msingi wa ndoa yako kwenye ku DO peke yake. Lazima kubalance. Inakusaidia nini mwenzi wako ana score 100% kwenye ku Do lakini s/he is Lazy, Complain all the time, Ditry, Narow minded, Drunkard, Bad Language and the list goes on and on. Lazima ku balance mambo.



 
Mtimti, ebu chunguza vizuri maisha ya wazazi wako, itakuwa lazima kuna mmoja si muumini wa kweli yaani hayuko serious sana na dini, kama mmojawapo anazingatia imani yake.

Lakini kama wote ni waumini watiifu ki kweli kweli kwa dini zao, shida ipo sana tu!

Kutojali kwa mmojawapo wa wazazi wako ndo kumesaidia katika hilo!
ukichunguza sana hao wazazi utakuta ni wachapa kazi na watu walioelimika huwa dini inakuwa kigezo kwa watu wavivu na wenye IQ ndogo we angalia wafuasi wengi au wanaojiita wakereketwa wa dini wengi wao ni watu wavivu mf makanisa yetu haya ya kileo 85% mahubiri yao mtolee mungu mtolee mungu na makelele usk kucha,watu waache watu wapendane
 
Du Mshikaji inaonekana 10% inakukera sana, Kama huna mpango na dini kama ulivyosema mwenyewe si uachane na kutoa hiyo 10%.?
Inakusaidia nin kutoa 10% halafu ukilala usiku unaweweseka kukumbukia hela zako ulizotoa?

Nakubaliana na wewe kua hisia za yanayofanyika katika ndoa ni zilezile uwwe na dini au usiwe na dini. Lakini nu lazima ku-Balance mambo yote kwa sababu si muda wote mnakua mna DO, Muda mwingi wa maisha yenu unakua mnashughuka na mambo mengine ambayo si ku DO. Sasa Endapo hayo mambo mengine yatawafanya msielewane hata hiyo mood ya ku DO sijui itatoka wapi.

Ushauri wangu ni kwamba usijenge msingi wa ndoa yako kwenye ku DO peke yake. Lazima kubalance. Inakusaidia nini mwenzi wako ana score 100% kwenye ku Do lakini kwenye s/he is Lazy, Complain all the time, Ditry, Narow minded, Drunkard, Bad Language and the list goes on and on. Lazima ku balance mambo.




Wala sijasema msingi wa ndoa ni ngono pekee. Nasema ni mambo yote mnayoshea na kufurahia. Hayo wanandoa ndio wenye uamuzi nayo, sio dini zao. Ukiona watu wamekubaliana kuoana, ni kwamba wameshaona mambo yao hayo yanaendana sawa, habari ya dini pembeni.

Kuhusu 10% ya kulipa kwenye dini sitoagi maana najua ni upumbavu. Lakini huwa naenda kanisani maana kuna washkaji kibao halafu kuna mambo yananifurahisha na kunitoa upweke, kama zile nyimbo wanazoimbaga, wakati mwingine nainjoi mahubiri ya mchungaji kama ninavyoijoi mijadala hapa jamvini, lakini 10% hawapati ng'o! Huwa natoa kiasi fulani cha fedha kanisani kulipia gharama za kawaida, maana hata disco kuna kiingilio bana, kwa hiyo sh 500 hivi nikitoa, sio mbaya.
 
iNATEGEMEANA jinsi ulivyo-deep kwenye dini yako. kama wewe ni muumini wa kweli basi inawezekana DINI ikawa kikwazo kikubwa katika si ndoa ila kuanzisha mahusiano na mtu yeyote. Wapo watu huanza kwa kuuliza wewe dini gani na akipata uhakika si mlengwa wake basi hata ufanye nini humpati ng'oo.
 
Back
Top Bottom