iNATEGEMEANA jinsi ulivyo-deep kwenye dini yako. kama wewe ni muumini wa kweli basi inawezekana DINI ikawa kikwazo kikubwa katika si ndoa ila kuanzisha mahusiano na mtu yeyote. Wapo watu huanza kwa kuuliza wewe dini gani na akipata uhakika si mlengwa wake basi hata ufanye nini humpati ng'oo.
Wabaguzi tu hao. Hata kwenye group discussion ya kusoma wanabagua. Nikiwa sekondari kulikuwa na chama moja lilikuwa limejitenga kabisa, ati wasichanganyike na 'mataifa', sa bahati yao mbaya katika kundi hilo nondo zilikuwa hazipandi, wote waliishia na division za kuning'inia karibu na zero.