Steven Wassira adai hakubaliani na ushindi wa Easther Bulaya

Mzee Wasira, hivi kweli wewe ndio mtu wa kulalamika wakati wewe ndio umekuwa ukikebehi jitihada za wapinzani kuhusu marekebisho ya tume ya uchaguzi? Ulidhani hayo tunayolalamikia hayakuhusu? Umekanyaga rasimu ya katiba iliyokuwa inaweka mazingira mazuri ya tume ya uchaguzi, unasema Rais hana juisi ya kuwapa wapinzani hivyo wasiende ikulu? Umesahau vipindi vyako vya dakika 45 za ITV kuhusu mchakato wa katiba? yaani katika watu ambao kilasiku nilikuwa naenda kanisani kumuomba Mungu washindwe katika uchaguzi wakwanza ni wewe. Umekanyaga haki za watanzania sasa Mungu amekuonyesha, halafu umekanyagwa na komandoo wa UKAWA wa jinsia ya KE, hiyo ndiyo size yako. Sasa unaenda Star TV kulalamika, kwani hujui mahakama ilipo? Unadhani sisi ndio tumeumbwa kuwa raia wa kawaida tu wewe Ubunge na Uwaziri? Muda uliotumikia serikali unatosha. Acha vijana warejee rasimu ya katiba, wewe ukirudi utatuharibia, kaa pemebeni, Kula pensheni, subiri kupiga kura ya maoni ya katiba pendekezwa, Yaani wewe umeiharibu Tanzania, nina hasira na wewe. Hili sio tusi ni mtazamo wangu kwako. Tanzania Bila Wasira Inawezekana. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeee!

Pawaaaaaaaaaaaaaa...........mzee anatia aibu kweli huyu.........yeye nani mpaka awe kiongozi siku zote........
hili liwe fundisho kwa wengine.......pale unapokuwa kiongozi......halafu una dharau wananchi......hii ndio adhabu yao........
 
Kwanza huwa anauchapa tu usingizi ,anang'ang'ania kwenda bungeni kufanya nini na uzee wote huo.Apumzike tu na wajukuu sasa.Naamini hajaonewa kabisa.Bulaya is good.
SABABU;
- Uchaguzi haukuwa huru na haki.
- Kura zilizopigwa ni zaidi ya waliojiandikisha

Source.
MAHOJIANO NA ITV.
 
bora Makinda aliyesoma alama za nyakati akaamua asigombee kulinda heshima yake... huyu mzee naye angefanya hivyo
 
pic+wasira.jpg
 
Bulayo umenifurahisha sana Dada yangu kwa kumtoa MTU aliyejiona na majigambo mengi kuitetea ccm asante bulayo Mungu akubariki
 
Wapiga kura: Mzee Wassira wananchi wako tuna shida ya maji. Tukikuchagua tuletee maji

Stephen Wassira: Kwani dawa mnamezea nini?!
 
Naomba msaada, Kura zilishapigwa, matokeo yakatoka, na mbunge wa zamani kashindwa, kwa nini bado tumuite mheshimiwa? Je ipo siku maalumu tunayotakiwa ku-drop hili jina la Mheshimiwa. kwa mantiki hii huyu Ndugu Wasira nadhnai si mheshimiwa tena au siyo?
 
Back
Top Bottom