Stephen J.J. Owawa: Naomba kujibu baadhi ya hoja zilizotolewa juu yangu hapa JF

owawajr

Member
Jul 30, 2009
46
36
Wapendwa wana JF kuna post iliyoomba CV yangu kwa madai kuwa alikuwa katika utafiti katika wilaya yetu ya Rorya na kuzua baadhi ya maswali na majibu ya ukweli kutoka kwa watu tunaofamhamiana katika harakati,Nashukuru kwa wale walionipigia simu na wale wote waliotoa majibu ya ukweli kwa kile wananchokijua juu yangu,Bado nadhani kuna baadhi ya mambo humu yanahitaji majibu kutoka kwangu au kusema ukweli ili ukweli utuweke huru japo kuna ya kujibu hasa yale ya msingi ila siyo kujibu ya uongo.Naomba kujibu haya:


  1. Jina: Stephen Juma Johnson Owawa
  2. Nilipo: Bukoba-Kagera
  3. Kazi:Mkaguzi (Auditor) ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
  4. Elimu: Primary-Ratia primary School-Rorya,Sekondary-Arwing secondary School-DSM,A-Level-SHYCOM shinyanga-ECA,Chuo,University of Dar es Salaam (B.COM-Accounting)
  5. Kuhusu kumaliza Chuo:Nimemaliza UDSM 2010 baada ya kufukuzwa mara nyingi kutokana na kupinga sera ya elimu ya juu hasa mfumo dhania ya uchangiaji
  6. Kushiririki uchaguzi jimbo la Rorya 2010: Nilishiriki katika uchaguzi kupitia CHADEMA kama mratibu wa kampeni wa Mgombea Ubunge Martin Ochola Ndira kuanzia kuhame kwake NCCR kuja CHADEMA na kushiriki kwa mwezi moja kwenye kampeni
  7. Kugombea Ubunge Rorya: Ni haki ya kikatiba kwa mtu yeyote ili mradi atimize matakwa ya sheria

Wana JF kama kuna maswali ya msingi na ya Ukweli yanayostahili kujibiwa nitayajibu kwa maana ya ukweli wake nilionao na uhalisia wake kutoka kwangu.

Naomba kuwasilisha.
 
Nimeambiwa kwamba 2015 CCM watamsimamisha Mama Gaudensia Kabaka (Waziri wa Ajira na Vijana) baada Lameck kairo kusema hatagombea. Vipi huo ubavu wa Mama Kabaka utaumudu?
 
Kwa nini unataka kuacha kazi ya ukaguzi ili uwe mbunge? Nijibu swali hili halafu nikuulize kuhusu Rorya
 
Hakuna sehemu niliyosema kuwa naacha kazi kugombea ubunge ila kama kugombea ubunge au udiwani ni njia bora zaidi kuchangia maendeleo kuliko kazi vyote vinaweza kupimwa

Wewe timiza ndoto yako. Ila baba yangu safari ni safari alitaka ujibu kuwa kule Bungeni kuna poshoz nzuri ukilinganisha na unakofanya. Pia mwambie hata mwalimu Diamond Gangwe ( Shycom) aliacha Ualimu akawa refa!!!
 
Hakuna sehemu niliyosema kuwa naacha kazi kugombea ubunge ila kama kugombea ubunge au udiwani ni njia bora zaidi kuchangia maendeleo kuliko kazi vyote vinaweza kupimwa

sikiliza kaka,ukiamua kugombea ubunge ina maana unapoteza kazi yako ya sasa hivi,jibu lile swali pale juu
 
Owawa,wewe sio makini,nimesoma na wewe darasa moja.Unakumbuka wewe ulianzisha mgomo baadae ukahongwa na kina mkandala ukataka kuusitisha.Lakini wapambanaji wa ukweli akina Silinde wakaendeleza moto_Owawa,your true color is not known.
 
Kaazi kwelikweli.......Unaajianzishia thread unajiomba CV yako mwenyewe,Unajijibu........Dah,haya bana jifanyie promo

Kwani wewe umekatazwa kujianzishia thread yako? kasema jana kuna mtu alianzisha thread kutaka kujua CV yake, so leo kaja mwenyewe kueleza kwa ufasaha.
 
Back
Top Bottom