DOKEZO Stendi ya Daladala ya Mbezi Mwisho inanuka mkojo tupu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Kabwelavoice

New Member
Mar 30, 2023
1
3
Habari Wadau,

Ukweli hii ni kero ambayo mwisho wa siku itakuja kuzaa magonjwa ya mlipuko. Stendi ya Mbezi mwisho ya daladala ambayo hata magari ya Mwendokasi yanapaki pale, kuna kero ya watu kukojoa hovyo ndani ya stendi huku walinzi na migambo wa jiji wakifukuzana na wamachinga tu lakini wanaokojoa wanawaangalia tu.

Kujihakikishia fika Mbezi mwisho asubuhi, simama lile eneo ambalo abiria wanapanga foleni kusubiri mwendokasi, mkojo unatiririka na unatoa harufu kali kwelikweli. Lakini Mamlaka zipo tu. Hii stendi wakati mwingine hata taa unakuta haziwaki ni giza tu, kilichobaki pale ni watu kuanza kujisaidia haja kubwa tu.

Kwa mtindo wa usimamizi huu, uongozi wa Manipaa ya Ubungo nachelea kusema ni useless kwasababu ni zaidi ya mwaka hali ni hiyohiyo tu kila siku.

daldala mbezi mwisho.jpg

Pia soma:
 
Aaaah bwanae tunakula Daku sie bana....usitutie kichefuchefu sie. Kwani hakuna Serekali ya Mtaa huko? Unataka Mama SAMIA aje adeki hiyo mikojo? Aaah sio kweli bhana! Mnazingua!!!!
 
Maeneo kama hayo huduma ya choo ilitakiwa iwe bure. Stand inaingiza pesa ndiyo ingegharamia huduma hiyo. Tatizo tena ukiweka bure ndani ya wiki vyoo vinakuwa haviingiliki.
 
Hii ndiyo namna ngozi nyeusi ilivyo. Hatuwezi jiongoza hata siku moja. Si watu wa chini, si viongozi wetu wa juu.
 
Back
Top Bottom