A
Anonymous
Guest
Sisi tunaokaa Stendi ya Daladala ya Mbezi Luis kila siku tumelalamika vya kutosha kuhusu changamoto ya ulinzi unaofanywa na walinzi wa Suma JKT hapa.
Changamoto zao kubwa hazijulikani kwa mamlaka za juu, tatizo lipo hivi stendi hiyo ina watu wanaolinda yaani Suma JKT ambao wamekuwa wanawafukuza Wafanyabiashara humo ndani.
Kuna muda wanazima taa makusudi ili wawakamate Wafanyabiashara waliomo ndani ya kituo na wakiwakamata huwa Wanawanyanyasa na wakati mwingine kuwapora biadhaa zao wanazoziuza kisha kuzitumia wao, mfano Samaki au sigara na vitu kama hivyo.
Ukitaka kupata uhakika tembelea kituoni hapo mida ya mchana, kuna mtu wanamwita Msambaa, huyo jamaa ni hatari kwa kuwa ndio anaongoza ‘uhalifu’ huo unaofanywa kwa mgongo wa ulinzi.
Wanachofanyiwa Wananchi tena Watanzania wenzetu hiyo stendi ina mambo jamani.