Star tv yageuka kero kwa watazamaji

Baba Tina

Senior Member
Dec 22, 2010
131
2
Thursday, February 03, 2011
Wana jamvi napenda kutumia muda huu kuelezea masikitiko yangu kuhusiana na suala la tatizo la sauti ambalo sasa linaelekea kuota mizizi na kua kero kwa watazamaji wake wanaofuatilia vipindi mbalimbali hasa vipindi vya tuongee asubuhi na taarifa za habari.

Kitu kinachosikitisha zaidi ni pale tatizo hilo la sauti linapotokea na watangazaji wa vipindi husika wakiendelea kuendesha vipindi na kuwaacha watazamaji wakiangalia picha ya muendesha kipindi bila kusikia sauti ya kile kinachozungumzwa. Tatizo hili si geni star tv lakini sasa imefika wakati watazamaji tumechoka na inabidi tuondoe dukuduku letu.

Natambua kuwa matatizo ya kiufundi wakati mwingine haya epukiki na yanakua nje ya uwezo na yamekua yakitokea hata katika vituo vingine vya televisheni lakini tumeshuhudia matukio hayo yanapotokea katika vituo vingine vya televisheni mafundi wanawahi kuondoa picha hiyo na kuweka matangazo wakati wakiendelea kurekebisha mitambo na mambo yakiwa sawa wanaendelea na kipindi. Suala hili na nadra sana kutokea star tv.

Kitu ninachojiuliza ni kwamba inakuwaje tatizo hilo linapotokea STAR TV mafundi wanashindwa kufanya marekebisho na kuacha watazamaji wakiendelea kuangalia picha ya muendesha kipindi bila kusikia maneno yanayo zungumzwa?? Au star tv haina mafundi wa sauti, au pengine mafundi wao wana uwezo duni. Jibu wanalo star tv wenyewe.

Kinachosikitisha zaidi mara nyingi tatizo la sauti linapotokea mwendesha kipindi huendelea na kipindi kama vile hakuna tatizo lililotokea. Kwa mfano, kama taarifa ya habari inasomwa na tatizo la sauti likatokea basi habari hiyo itaendelea bila sauti na ikimalizika habari hiyo mtangazaji anaendelea na habari nyingine bila maelezo yoyote! Ina maana mtangazaji huyo anakua hajui kama sauti haitoki???

Kwa wale walioangalia kipindi cha tuongee asubuhi leo alhamisi ambapo viongozi wa chama cha walimu Tanzania (CWT) walialikwa wameshuhudia jinsi Rymondi Nyamhula alivyokua akizungumza kwa muda mrefu bila yeye wala mafundi kujua kwamba sauti haitoki mpaka pale watangazaji waliokua Dar es Salaam walipoligundua tatizo na wao kuendelea na mjadala na kumuondoa hewani. Walau kwa leo waliomba radhi japokua bado waliiacha picha hewani kwa muda mrefu.

Taarifa ya habari ya leo usiku pia ilikua inaboa kwa sababu sehemu kubwa ya habari iliyosomwa leo sa mbili usiku haikua na sauti. Wale walioangalia habari leo usiku wameshuhudia msoma habari Jacob Marcus akiendelea kusoma habari japokuwa mara nyingi sauti yake au ya reporter ilikua haisikiki kabisa. Kila alipomaliza kusoma habari moja aliendelea kusoma habari nyingine kimyakimya na kutuacha watazamaji hewani.

Naamini star tv ni moja kati ya vituo vya televisheni ambavyo vimejijengea heshima kubwa hapa nchini kwa kua na vipindi bora na mijadala mizito yenye tija kwa taifa lakini wanapoendelea kufumbia macho tatizo hili la sauti wanajivunjia heshima waliyojijengea kwa watazamaji.

Nawashauri star tv wafanye hima kushughulikia tatizo hilo kwani sasa limekua kero kubwa kwa watazamaji. Star tv wawakumbushe mafundi wao wanaohusika na sauti waamke usingizini na watimize wajibu wao ipasavyo ili kuendelea kukijengea heshima kituo hicho cha televisheni. Wawe makini kurekebisha tatizo linapotokea mapema na sio kutuachia picha isiyokua na sauti.

Nawasilisha:
 
Sio kawaida kuwahi kurudi nyumbani sasa leo kwa shauku kubwa nikanasubiri taarifa ya habari star TV nikao Wanapiga musiki kuja kuangalia muda saa 2 30 then tarifa haina sauti mh real bad
 
Hata upande wa RFA kuna tatizo la kiufundi. Sijui kwa nini!! Dialo aangalie biashara yake isije ikakimbiwa na wateja.
 
Kinachosikitisha zaidi sio kukatika kwa sauti bali ni pale sauti inapokata hala jamaa wanaendelea kutuachi picha zisizokua na sauti kwa muda mrefu tu na mafundi wanatulia tu.
 
Mbona nyingi tu ambazo sio za siasa zinawekwa kwenye jukwaa la siasa? Ukweli ni kwamba jukwaa la siasa lina wapenzi wengi sana kuliko majukwaa mengine.
 
Nimefurahia unavyohitimisha, ni wazi wewe ni mtumishi wa umma!
 
ni kweli star wasipoliangalia hili na kulitufutia ufumbuzi fasta sie wadau tutakula kona muda si mrefu! bt kwa shingo upande coz kiukweli star wapo juu kutupa vitu really, Wajitahidi kutatua!
 
Kweli jana walichemsha,kwanza taarifa ya habari walichelewa kusoma kimbembe cha pili ukosekanaji wa sauti.
 
Basi mode uweke hii habari kwenye jukwaa la habari mchanganyiko
 
Back
Top Bottom