Wasalaam wanasheria wa jf,naomba msaada wa kisheria kuhusu stahili zangu ambazo natakiwa nizidai kwa mwajiri wangu. Mi ni mwalim ambaye kwa sasa nipo chuo kikuu nikisoma shahada ya kwanza. Barua ya ruhusa kutoka kwa mwajiri kwenda kusoma inaeleza kwamba nijigharimie. Swali langu ni kwamba kwa barua hiyo sina tena haki ya kumwomba mwajiri anilipie chochote katika masomo yangu?