Spika Wa Bunge La Muungano awe toka chama cha upinzani

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,294
24,179
Ipo haja ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania atoke chama kikubwa cha upinzani baada kuangalia ufunguzi wa kikao cha Bunge la Muungano Februari 2011 mjini Dodoma na yaliyojitokeza.

Inaonekana ili Spika wa Bunge awe makini katika kufuata sheria, kanuni na busara basi hakuna shaka Spika atoke chama kikubwa cha upinzani. Ikiwa hivyo basi huyo spika wa bunge hatakuwa anafanya maamuzi ya kishabiki maana anajua wabunge wa chama tawala ambao watakuwa wengi watamburuza kumrudisha afuata taratibu, sheria na kanuni za Bunge.

Vyama vya upinzani pamoja na kutaka kusimamia kamati za Bunge, pia wapeleke muswada/hoja ya nafasi ya Spika wa Bunge iwe kiutaratibu inachukuliwa na chama cha upinzani chenye wabunge wengi. Nafasi ya Naibu Spika iende kwa chama tawala chenye wabunge wengi kinachoongoza serikali.

Maana kwa sasa inaonekana Bunge, wabunge na Spika badala ya kujikita kujadili miswada inayoweza kutatua kero zinazowasumbua wananchi kama umeme, miundo mbinu, huduma za afya, ufisadi n.k, Bunge sasa kwa kupitia CCM yenye wabunge wengi wanaangalia jinsi ya kuvuruga na kuvibana vyama vingine vya siasa.

Muundo huo mpya wa Spika wa Bunge awe toka chama cha upinzani utaleta ufanisi wa majukumu ya Bunge na wabunge, kwani Spika anajua akivurunda basi haitachukua muda mrefu kazi itamshinda na itabidi ajiuzulu kwa kupigiwa kura za kutokuwa na imani naye kutokana na sababu za msingi zenye mantiki na si za kishabiki.
 
Pole saana Ndg yangu, uwezekano huo haupo maana hiyo ruling party ndio wapiga kura bungeni kwa hiyo its next to impossible. Jibu hapa ni katiba mpya ya wananchi wenyewe wala si watawala waunde katiba ya kututawala!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom