Spika Tulia: Wanaojitolea kwenye kazi wapewe kipaumbele wakati wa kuajiriwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ameshauri Serikali kuweka utaratibu maalumu wa kuwazingatia kwanza Watumishi wanaofanya kazi za kujitolea wakati Serikali ikiendelea kufanya maboresho ya Sheria ya Ajira ili kuwasaidia kupata ajira bila kikwazo pindi zinapotangazwa.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Kiteto (CCM), Edward Olelekaita alihoji ni lini Serikali itapeleka Bungeni marekebisho ya Sheria ya Ajira ya Utumishi wa Umma ili kuongeza kigezo cha kujitolea katika kupata ajira ambapo Naibu Waziri wa Utumishi, Ridhiwan Kikwete amesema Serikali inafanya mapitio ya Sheria ya Utumishi wa Umma sura 298, sera ya menejimenti na ajira katika utumishi wa umma.

Kwa upande wake Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene amesema “Haipendezi kuona Daktari akilima Matikiti wakati sisi tunauhitaji wa Madaktari au Walimu, tunakuja na mpango mkakati wa kumaliza tatizo hilo,”

============

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameiagiza Serikali kuja na utaratibu maalumu kwa wanaofanya kazi za kujitolea kabla ya kuwa na sheria ya kuwasaidia kupata ajira bila kikwazo zinapotolea.

Spika ametoa mapendekezo hayo leo Jumatatu Septemba 4, 2023 wakati wabunge wengi walipouliza kuhusu nafasi ya watu wanaojitolea kutopata kipaumbele kwenye ajira mpya.

“Mheshimiwa Waziri, pamoja na kuwa hamjaleta sheria lakini ni vyema mkaangalia na kuwepa mpango maalumu kwa wanaofanya kazi za kujitolea ili inapotokea nafasi za ajira wapate moja kwa moja,” amesema Dk Tulia.

Katika swali la msingi Mbunge wa Kiteto (CCM), Edward Olelekaita alihoji ni lini Serikali itapeleka bungeni marekebisho ya Sheria ya Ajira ya Utumishi wa Umma kuongeza kigezo cha kujitolea ili kutoa fursa kwa wanaojitolea.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete amesema amesema kwa sasa Serikali inafanya mapitio ya Sheria ya Utumishi wa Umma sura 298, sera ya menejimenti na ajira katika utumishi wa umma.

Amesema lengo ni kuhakikisha Serikali inaongozwa na utaalamu na weledi “meritocracy” na usawa wa fursa za ajira kwa Watanzania wote.

Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene amesema Serikali haitakuwa tayari kuona mtumishi anayehitajika akibaki mtaani wakati kuna upungufu.

“Haipendezi kuona daktari akilima matikiti wakati sisi tunauhitaji wa madaktari au walimu kuzagaa mtaani wakati wamesomeshwa kwa rasilimali za nchi, tunakuja na mpango mkakati wa kumaliza tatizo hilo,” amesema Simbachawene.

MWANANCHI
 
Una familiaa ukajitolee utailisha nini familiaa? Aliyeshiba hamjali mwenye njaa
 
Back
Top Bottom