thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Ndugu Dr Tulia Ackson Mwansasu,spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na uongozi mzima wa bunge letu,kichwa cha habari kimejieleza vyema.
Ripoti ya CAG imejaa madudu mengi sana kuhusiana na ubadhirifu wa fedha za umma ndani ya serikali, hii haikubaliki hata kidogo, kwasababu ubadhirifu huo unadumaza nchi na wananchi kwa ujumla,kadhalika ubadhirifu huo unafanya wananchi wakose imani kwa rais Samia na CCM kupoteza mvuto.
Kwakua serikali inasiku ishirini na moja kujibu hoja hizo za CAG tusubiri, japokuwa muda wa kutosha serikali ilikuwa nao hata kabla CAG hajaiweka hadharani ripoti hiyo ya ukaguzi, ,kwangu mimi binafsi sidhani kama wanamajibu ya kutosha kuhusiana na tuhuma hizo , kudumisha utawala bora acha tusubiri kuona jipya.
Ndugu Spika wananchi wanalalamikia ubadhirifu huo kwa uchungu mkubwa sana, wapo ambao wanakata tamaa ya kulipa kodi,wakiamini watalipa ili zikatafunwe na wajanja wachache serikalini.ikumbukwe serikali inajiendesha kwa kodi mbalimbali.kukosekana kwa kodi hakuna ambacho serikali itafanya.
Nikuombe ndugu Spika, japo bunge limejaa wabunge wengi wa ccm, lakini kuna wabunge ambao hawakubaliani na ubadhirifu huo ,wape nafasi waisimamie serikali kisawasawa, kufanya hivyo utamsaidia rais Samia, chama chako,. nchi, na wananchi kwa ujumla, si watumishi wote wa serikali wanahusika na ubadhirifu huo ,bali kuna wahuni wachache ndani ya serikali wanaichafua serikali nzima kwa tamaa zao,hawa toa nafasi kwa bunge lishughulike nao,na ndio wajibu wake,pasiwepo na biashara ya kulindana,ikumbukwe tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu 2025,ni vyema kufika serikali na chama vikiwa visafi.
Na kama hoja za serikali zitakuwa dhaifu kama CAG alivyoripoti ni vyema ikaundwa kamati teule ya bunge yenye wazalendo na wanaogopa mungu wachunguze tuhuma hizo,ili kuleta tumaini kwa watanzania.
Nawsilisha