Spika Sitta agawa matrekta 12 jimboni kwake

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Spika Sitta agawa matrekta 12 jimboni kwake

Na Tausi Mbowe, Urambo Tabora

SPIKA wa Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta amesema wakati wa malumbano umeisha na sasa ni wakati wa viogozi na wabunge kushirikiana na wananchi katika kuwaletea maendeleo kwa lengo la kupunguza umasikini katika kaya zao.


Spika Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki alisema hayo mjini hapa jana wakati wa hafla ya kuwakabidhi matreta aina ya 'power tiller' kwa ajili ya kilimo katika kata 12 za jimbo hilo yenye thamani ya zaidi ya Sh 100 milioni.


Akizungumza huku akishangiliwa na umati wa watu, Spika Sitta alisema kazi hiyo ni muhimu katika maisha ya wana Urambo kwa kuwa sasa wanachohitaji ni maendeleo na si suala lingine.


“Ndugu wana Urambo wenzangu tunaweza kila siku kuzungumza bila mafanikio, wananchi sasa wamechoka na wanachotaka kutoka kwa viongozi wao si maneno tu wanahitaji tuwape maendeleo ili waweze kujikwamua katika lindi la umasikini walionalo na si vinginevyo,”alisema Spika Sitta.


“Hivi wananchi hata kama tunaweza kujenga barabara, kuboresha miundombinu , lakini bila kipato ni kazi bure,”alisisitiza Spika Sitta huku akishangiliwa na umati huo.


Kauli ya Mbunge huyo inaweza kuwa mwiba kwa wapinzani wake na baadhi ya viongozi na wabunge ambao kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakilumbana badala ya kufanya kazi waliyotumwa na wananchi waliwachagua.


Wabunge sasa wamekuwa wakinyoosheana vidole wenyewe kwa wenyewe katika hoja ambazo si za msingi na kufikia kukashifiana huku wengine wakiwatuhumu wenzao kwa kufadhiliwa na kundi la mafisadi katika mambo yao binafsi kama harusi na hata katika kampeni zao za kutafuta nafasi za ubunge.


Akizungumzaia kuhusu matrekta hayo, Sitta alisema matreta hayo yametolewa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark na kwamba yatagaiwa kwa vikundi vya wanawake 38 ambapo vyenye kaya 800 zitakazonufaika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo.


Akifafanua zaidi Sitta alisema, mara baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza, balozi wa Dermak atakuja kukagua mradi huo na endapo ataridhika serikali yake itatoa tena matrekta mengine kwa ajili ya awamu ya pili ambapo zaidi ya kaya 1,600 ikiwa ni mara dufu ya awamu ya kwanza zitanufaika.


“Kama tunavyojua sasa kipindi cha kilimo cha alizeti kimeisha, nimeagiza matrekta haya yatumike katika shughuli nyingine za maendeleo badala ya kusubiri kilimo cha alizeti na karanga pekee,” aliongeza.


Alisema matrekta hayo yana uwezo wa kufungwa pampu na pia yana uwezo wa kutumika katika kilimo cha umwagiliaji hivyo kusaidia mpango wa serikali wa kilimo kwanza kwa vitendo.


Awali, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Urambo, Dewji alimpigia debe mbunge huyo na kusema kuwa haoni sababu ya jimbo hilo kuchukuliwa na wapinzani katika uchaguzi ujao kutokana na ukweli kwamba CCM imeweza kujizatiti na kwamba katika uchaguzi huo anauhakikika jimbo hilo watashinda kwa kishindo.


Dewji alisema hali hiyo imejidhihirisha wazi katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji ambapo CCM iliweza kuibuka kidedea kwa kunyakua viti vyote vya serikali za mitaa na kupoteza kijiji kimoja tu.
 
hahahaaaaa, waheshimiwa naona muda huu wanaumiza vichwa sana kuhusu 2010!!!.
kila la heri waheshimiwa, ila mjue mwakani hatuangalii uzuri wala sura, piga chini tu kudadadeeeki.
 
Back
Top Bottom