Spika Makinda Afafanua mvurugano kwenye mjadala wa Sheria ya Mchakato wa Katiba

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,547
113,727
Wanabodi,
Watch Live on TBC-
Spika wa Bunge, Mhe. Anna Makinda, ameliahirisha Bunge asubuhi hii, baada ya kipindi cha maswali na majibu ili kupata fursa ya kushiriki Public Hearing.

Pia Mhe. Makinda, anafafanua Kilichotokea Jana katika kupokea maoni ya muswada wa kamati ya kukusanya maoni ya katiba kwa vituo vya Dar es Salaam na Dodoma.

Mhe. Makinda avishutumu vyama vinavyotumia zoezi hili kama mtaji wa kisiasa! (makofi..)

Endelea kufuatilia.
 
Anadai wanaofanya vurugu wanahamasishwa na wanasiasa wenye kuwa na malengo mabaya kwa taifa? Natarajia kauli kama hii
 
Bado hajaahirisha, Pasco, mbona haraka.

Bado anaendelea kuwapaka viongozi anaodai wanachochea vurugu kuhusiana na Muswada ya Mabadiliko ya Katiba, kufuatia yaliyotokea Dodoma na Dar.

Wabunge wa CCM wanamshangilia kwa nguvu.
 
Makinda alaani zomea zomea.
Asisitiza muswada sio sheria,
asisitiza kuchangia kwa amani.
 
Bado hajaahirisha, Pasco, mbona haraka.

Bado anaendelea kuwapaka viongozi anaodai wanachochea vurugu kuhusiana na Muswada ya Mabadiliko ya Katiba, kufuatia yaliyotokea Dodoma na Dar.

Wabunge wa CCM wanamshangilia kwa nguvu.

Niko, alitangulia na tamko la kuliahirisha bunge ndipo ukafuatia ufafanuzi.
 
anapolaani zomea zomea, sisi tunalaani muswada wenyewe.

so we are even.

mpaka kielelweke.
Ng'wanangwa, amesisitiza huo muswada sio sheria, unarekebishika ndio maana unajadiliwa, wapinzani wa muswadi huo, wametakiwa kutoa maoni ili itakaundwa sheria, ndio iwe na hayo maoni ya wadau.
 
Anadai wanaofanya vurugu wanahamasishwa na wanasiasa wenye kuwa na malengo mabaya kwa taifa? Natarajia kauli kama hii
Invisible, sisi kama wana jf, tutafute namna ya kuwasaidia wenzetu hawa ambao sasa hawatajwi tena kwa majina, bali wana kuwa labed kama 'wafanya vurugu', hali hii ikiachiwa kuendelea hivi hivi, itafikia wakati ita register kwenye mind ya Watanzania kuwa kina 'fulani' ni wafanya vurugu!.
 
Kuna mwelekeo wa kupanga kuhusisha ukosoaji wa mswada huu na Chadema. Serikali na ccm wanatumia mbinu hii kukwepa hoja zinazokosoa mswada huo.

Jana mkuu wa mkoa wa Dodoma alidai waliozuiwa nje ya bunge walikuwa ni wanafunzi wa udom ambao waliletwa na Chadema. Lakini siyo wote walikuwa wanafunzi na wanachama wa Chadema. Tambwe hiza alizomewa Karimjee wakadai ni Chadema. Lakini hata ccm walimzomea!

Kama nia ya serikali na ccm ni kuupitisha huo mswada ulivyo basi watatumia kisingizio hicho cha kijinga kuupitisha, wakidhani wanakomoa Chadema. Wakifanya hivyo watahatarisha Amani.

Kwanaza ni kweli kwamba huo mswada umekaa vibaya na mapungufu mengi mno. Pili, ni dharau kubwa sana kwa watz ambao siyo Chadema kuwaona kwamba hawana akili ya kuona yaliyomo kwenye huu mswada.

Tatu, basi hata kama mko sahihi kwamba ni wanachama wa Chadema pekee wenye akili na uwezo wa kuchambua uzuri na ubaya wa huu mswada, wao pia ni watz hivyo wana haki ya kusikilizwa.

Nne, kukataa hoja kwa sababu humpendi mtoa hoja ni kusokota sayansi mantiki. Shuhulikia hoja usimshuhulikie mtoa hoja!
 
tutawazomea mpk kieleweke. Wamezoea vya kunyonga, mwaka huu watakula vya kuchinja. 2nashukuru, endlea ku2habarisha, mungu akutangulie.
asante mwanamama mtamu (sweetlady), habari yenyewe ya kuhabarishwa imeishapita!, hapa tunazungumzia tuu, yatokanayo.
 
nafikiri spika na ccm ndo wafanya fujo. wanavuruga "public hearing" ya mswada huo. wao wanataka waingize watu wenye kukubaliana na utumbo waliouandaa. tz ya leo siyo ya 1950s. ubaya wao wa kusababisha fujo, wanataka waupelekee kwa wengine??? ajabu-'kweli nyani hajioni kundule'!!!!!!!!!!!!!
 
Wanabodi,
Watch Live on TBC-
Spika wa Bunge, Mhe. Anna Makinda, ameliahirisha Bunge asubuhi hii, baada ya kipindi cha maswali na majibu ili kupata fursa ya kushiriki Public Hearing.

Pia Mhe. Makinda, anafafanua Kilichotokea Jana katika kupokea masoni kwa vituo vya Dar es Salaam na Dodoma.

Mhe. Makinda avishutumu vyama vinavyotumia zoezi hili kama mtaji wa kisiasa! (makofi..)

Endelea kufuatilia.

Ni ukosefu wa hekima kutafuta visingizio kwa kila kitu kinachotokea dhidi ya serikali kuwa kinasababishwa na vyama vya upinzani bila kuangalia kwanza serikali yenyewe inawajibaka vipi kwa wananchi wake.

Muswada ni mbovu, majibu yanayotolewa na wawakilishi wa ccm ni hovyo, bunge halikuwa tayari kuhudumia idadi ya waliojitokeza. Kwa maoni yangu lawama zilitakiwa zipelekwe serikalini na kwa kamati husika kwa kutoweka mazingira shirikishi zaidi kwenye suala hili nyeti badala ya kutafuta mchawi
 
Ng'wanangwa, amesisitiza huo muswada sio sheria, unarekebishika ndio maana unajadiliwa, wapinzani wa muswadi huo, wametakiwa kutoa maoni ili itakaundwa sheria, ndio iwe na hayo maoni ya wadau.

Kuna uhuni unafanyika katika kukusanya hayo maoni. Mfano Dodoma jana walipeleka wanafunzi wa City Secondary ya huko pamoja na akina mama nadhani wa Manyoni ambao kiukweli hawana upeo wa kudadavua lugha ngumu namna ile ya kisheria. Sasa watu wenye weledi wanapotaka kupata haki yao wao wanaita fujo. Kama hawataki kusikiliza watu wafanye nini?
 
Invisible, sisi kama wana jf, tutafute namna ya kuwasaidia wenzetu hawa ambao sasa hawatajwi tena kwa majina, bali wana kuwa labed kama 'wafanya vurugu', hali hii ikiachiwa kuendelea hivi hivi, itafikia wakati ita register kwenye mind ya Watanzania kuwa kina 'fulani' ni wafanya vurugu!.

Which happens to be the truth, good morning...
 
Je alipoahirisha amesema kama na ukumbi nao umebadirishwa? au ni kale kale kaukumbi kiduchu? kama vipi waweke ngoma uwanjani, au serikali itangaze mapumziko wiki nzima midahalo hiyo ifanyike nchi nzima kila watu mkoani kwao, kisha yakusanywe yaliyojadiliwa na wananchi, ili wapate input za watu wote siyo dom tu na dar.
 
kwani huyu anaihusisha chadema kwa namna yoyote ile kwamba wanatafuta mtaji wa kisiasa???au ni vyama gani vinavyojihusisha kwenye zoezo hili la public hearing???coz nina hofu kama wabunge wa CCM wanashangilia kwa kupiga makofi huenda CHADEMA ndio kimewekwa kiti motpo hapo........
 
Back
Top Bottom