Spika Makinda Afafanua mvurugano kwenye mjadala wa Sheria ya Mchakato wa Katiba

Kazi ipo kubwa sana spika yeye ni chadema tu ila kitu kiienda vibaya ni chadema... Ila yakienda vizuri ni ccm.. Sasa zamu hii mpaka kieleweka..

Hao waotaka katiba mpya siyo ccm wala cdm ni watanzania kwa hiyo walete huo muswada tuujadili hata huku mikoani...

Mapambano haya ni mpaka kieleweke....
 
Ule muswada nimeusoma, ni mbaya kiasi kwamba ukipita bungeni basi tujiandae kuingia katika matatizo makubwa, ni bora tubaki na katiba hii kuliko muswada huo kupitishwa kuwa sheria, kwa maana utazaa katiba mbaya kuliko hii tuliyonayo. Nashindwa kuelewa hawa walioandaa muswada huu kama ni wazalendo kweli au wana uraia wa nchi mbili, hivyo mambo yakiharibika hao wanaondoka na familia zao, sisi wengine tutakwenda wapi? maana uraia wetu wengine ni wa tz tu, tz ni alfa na omega.
 
Ule muswada nimeusoma, ni mbaya kiasi kwamba ukipita bungeni basi tujiandae kuingia katika matatizo makubwa, ni bora tubaki na katiba hii kuliko muswada huo kupitishwa kuwa sheria, kwa maana utazaa katiba mbaya kuliko hii tuliyonayo. Nashindwa kuelewa hawa walioandaa muswada huu kama ni wazalendo kweli au wana uraia wa nchi mbili, hivyo mambo yakiharibika hao wanaondoka na familia zao, sisi wengine tutakwenda wapi? maana uraia wetu wengine ni wa tz tu, tz ni alfa na omega.
GJ Mwanakatwe, japo tunashutumu sana, lazima tuwe fair na kuwa wakweli, huu sio muswada wa katiba mpya, ni muswada wa kukusanya maoni. Ukipita ndipo maoni yakusanywe na ni maoni hayo ndiyo yataamua katiba iweje, Sasa hata maoni bado hizi hoja za kupata katiba mbaya zaidi kuliko hii iliyopo zinatoka wapi?.
 
GJ Mwanakatwe, japo tunashutumu sana, lazima tuwe fair na kuwa wakweli, huu sio muswada wa katiba mpya, ni muswada wa kukusanya maoni. Ukipita ndipo maoni yakusanywe na ni maoni hayo ndiyo yataamua katiba iweje, Sasa hata maoni bado hizi hoja za kupata katiba mbaya zaidi kuliko hii iliyopo zinatoka wapi?.
Mkuu,
Nadhani Watanzania wengi wanachotaka ni katiba mpya na kwa hali yoyote ile miswada unapoletwa bungeni na kwa wananchi ni lazima ulenge azma hiyo..

JK aliwaahidi wananchi katiba mpya - kwa kauli yake mwenyewe na kasifiwa sana na vyombo vya ki ataifa.
Sasa sielewi huu Muswada unaozungumzia marekebisho ya katiba zaidi badala yakutunga katiba mpya, kuna maana gani zaidi ya kuwachanganya wananchi kwani sehemu zote muhimu zinazosababisha wananchi kudai katiba mpya hazina mjadala.

1: Rais anapotaja yeye kuchagua tume ina maana hatuzungumzii katiba mpya kwani kama ingekuwa na lengo hilo taratibu za muundo wa katiba mpya ni zaidi ya mamlaka ya rais..mwenye akili zake timamu ukiusoma miswada huu utajua haukuwa na malengo hayo hata kidogo..

2. Rais anapotaja sehemu muhimu za katiba zisiguswe ina maana katiba ya zamani inafanyiwa marekebisho zaidi ya utunzi mpya... Kuna tofauti kubwa ktk kuitazama katiba nzima, kisha kuchukua yaliyo bora na mazuri kuliko kuweka mipaka ndani ya katiba hiyo..

JK kama raia na mwananchi angejadili na kuweka mapendekezo yake ktk mjadala kama wanavyofanya viongozi na wataalam wengine lakini hadi hapa yaonyesha muswada huu umeandaliwa kama ni shinikizo la Ikulu ktk kufanya marekebisho..

3. Muswada kuletwa bungeni kwa lugha ya kiingereza ni sehemu nyingine ya kudhihirisha kwamba hii ni sawa na report au muswada wa matumizi ya serikali ukilenga WABUNGE na wataalam zaidi ya wananchi wanaodai katiba mpya na la endelezo la marekebisho ya katiba ya mwaka 1977.

Ndio maana mshirika kasema, kwa mtaji uliopo hatuwezi kuwa na katiba bora zaidi ya tulokuwa nayo..

Nimesema jana mapema sana kwamba chama CCM na viongozi wake watayatumia matukio ya jana kisiasa kulaumu vyama vya Upinzani na wamefanya hivyo kuwabebesha lawama wapinzani kwani wao waliandika muswada huu makusudi ulete vurugu na kutoelewana..

Na maadam vyama vya Upinzani ni kati ya wadau wanaitaka katiba mpya kwa uvunda na ubani kisiasa, CCM imefanya makusudi kuandika muswada huu wakijua wazi kwamba vyama hivyo ndio vitakuwa vya kwanza kuupinga, na hakuna mahala isipokuwa kuwapeleka ktk kumbi za wananchi badala ya kujadiliwa kwa kina bungeni ktk kikao maalum na waalikwa wakiwa wataalam toka fani mbali mbali kulingana na utashi na lugha ya muswada wenyewe, kisha wananchi wakahusishwa baadaye ktk hatua ya pili..

Lakini kwa makusudi kabisa CCM imetaka maoni ya wananchi sii kutaka Katiba mpya bali kushiriki ktk mchakato wa muswada ambao hauna maudhui isipokuwa kuleta mfarakano.. Hadi hapa CCM moja wananchi tumetoka bila na hakika vyama vya Upinzani vitaendelea kuonekana vinataka kuleta vurugu hali wakijua fika kwamba vyama hivyo vinawakilisha mawazo ya wananchi wengi..
 
GJ Mwanakatwe, japo tunashutumu sana, lazima tuwe fair na kuwa wakweli, huu sio muswada wa katiba mpya, ni muswada wa kukusanya maoni. Ukipita ndipo maoni yakusanywe na ni maoni hayo ndiyo yataamua katiba iweje, Sasa hata maoni bado hizi hoja za kupata katiba mbaya zaidi kuliko hii iliyopo zinatoka wapi?.

Sasa hapo unatofautishaje process to the out put? Sasa kama maoni yenyewe yamewekewa constraints unauhakika gani hicho kitakachokusanywa kitakuwa ndicho kilichotolewa kama kuna Alfa na Omega hapo ndiye mwamuzi? Wewe ndiye unataka kutupotosha tu relax na watu waanze hatua ya kuondoka. Kumbuka kila safari lazima ianze kwenye ziro ukisha ondoa mguu maana yake hizo kilometer zimesha pungua. Na ole wako uanze hiyo safari kwa mwendo kasi huku ukijua kabisa wewe ni mgonjwa wa pumu.
 
makinda ni zao la ufisadi, speaker anaonesha waziwazi maslahi yake, huu mswada ni sumu na big disaster, sikio la kufa halisikii dawa, the sinking ship ccm, hakuna think tank yeyote anayeunga huu upupu eti mswada, nawaomba chadema waseme waziwazi kuwa hii ni sumu ya kuingamiza ccm, makinda atachemsha tuu na unafiki wake, najisikia vibaya kumwona akifanya propaganda speaker mzima aone aibu anatia kichefuchefu ndani ya bunge, yeye ni speaker ndani ya bunge siyo kada wa chama, shame on you makinda mungu atakuhukumu hapahapa duniani.
 
Wenzetu wa Kenya pamoja na tofauti zao kubwa za kikabila kwa kiasi kikubwa waliziweka pembeni tofauti zao hizo na kutunga katiba ambayo ilikubaliwa na asilimia kubwa ya Wakenya. Sisi pamoja na kutokuwa na tofauti kubwa za kikabila kutokana umoja mkubwa uliojengeka miongoni mwa Watanzania hasa kwa juhudi za Baba wa Taifa, lakini tuna mafisadi kundi la watu wachache sana hawafiki hata 10,000 lakini wamenuia kwa kila hali kuhakikisha wanaivuruga nchi yetu ili waendelee kuwekana madarakani hata pale wasipokuwa na sifa zozote za kushika madaraka ya nchi. Watanzania tusikubali kusambaratishwa na Mafisadi hasa wakati huu wa mjadala wa katiba. Ni lazima tuhakikishe kwamba katiba mpya itakayotungwa itakuwa inakubalika miongoni mwa asilimia kubwa ya Watanzania na siyo Katiba ambayo itakubalika na mafisadi tu.

Niliona fahari kubwa sana siku Wakenya walipoonyesha mshikamano mkubwa sana pale walipoikubali katiba yao mpya. Kwa dalili za mwanzo katika mjadala huu wa kariba mpya ambao inaelekea umeshapokwa na Mafisadi sidhani kama kutakuwa na mshikamano wowote utakaonyeshwa na Watanzania maana asilimia kubwa ya Watanzania tutaikataa KATIBA MPYA YA KIFISADI.

Landmark Moment as New Kenyan Constitution Takes Effect | News | English
 
Dr. inawezekana huyu Mark ni Deo Filikunjombe, kwani ametumia maneno kama yale ambayo yalitumiwa na Deo Filikunjombe wakati wa kumtuhumu Mwanakijiji. Sababu pia alizotoa zinafananafanana
Mkeshaji, wewe wa tangu 7th January 2011 (Join Date) na post zako zote 559, siamini kwa hujui kitu kinaitwa 'name calling'!.
sasa ikiwa ndiye au siye, what diference does it make?.
 
Invisible, sisi kama wana jf, tutafute namna ya kuwasaidia wenzetu hawa ambao sasa hawatajwi tena kwa majina, bali wana kuwa labed kama 'wafanya vurugu', hali hii ikiachiwa kuendelea hivi hivi, itafikia wakati ita register kwenye mind ya Watanzania kuwa kina 'fulani' ni wafanya vurugu!.

kweli,ila wakizidi kuwaita wanavurugu na sie tutawaita 'wala nchi/mafisadi'
 
tutaamka nao na kulala nao katika hili
uyu speaker aaangalie sana siku atakimbia kiti pale
ynai bila kificho anaongoza bunge ki-ccm??
 
Back
Top Bottom