Deo Meck Mbagi
JF-Expert Member
- Apr 19, 2015
- 360
- 525
Mh. Spika simamia ajira za wasaidizi wa Mbunge kuondoa ubinafsi, uchoyo na ufisadi.
Bunge la Jamhuri lina idadi ya wabunge 369 wakiwa wametimia wote. Kwa idadi hiyo kila mtu akiwa na wasaidizi watatu ina maana jumla ya watu 1107 watakuwa wamepata ajira kila kipindi cha bunge. Na ajira hizi zikirasimishwa ili wasaidizi hao wawe wanalipwa mshahara moja kwa moja na bunge, litachangia kuongeza idadi ya ajira rasmi za bunge na pia kuongeza idadi ya walipa kodi.
Hivi sasa ajira za watumishi hao wa mbunge imekuwa kama hisani, wabunge wengi hawaajiri na kutoa mikataba ya kazi kama wanavyoagizwa na bunge. Na watu hao sababu wanakuwa hawana mikataba wanakuwa wanyonge na wananyonywa na wabunge hao. Na kibaya zaidi watumishi hao hawajui ni kiasi gani kinachotoka bungeni na kuingizwa kwenye akaunti ya mbunge kama mishahara yao.
Kwa dunia ya sasa lazima tubadilike, wabunge wengi wamekuwa hawawalipi stahiki za hao watumishi. Badala yake wamekuwa wanawalipa kiwango kidogo sana na wakati mwingine hawawalipi. Na baadhi ya watumishi hao pindi wanapodai mishahara ambazo ni haki zao basi wabunge huwafukuza kazi. Huu ni ubinafsi, uchoyo na ufisadi ulio wazi unaofanywa na wabunge wako Mh. Spika.
Wakati kukiwa na kilio kikubwa cha vijana kukosa ajira, huku ajira zaidi ya 1000 zikiwekwa mifukoni mwa wabunge bila utaratibu maalum ni jambo ambalo linapaswa kukomeshwa.
Nashukuru nimepiga simu bungeni na kupewa ushirikiano, kwa maelezo ya aliyepokea simu ni kuwa waajiriwa wote wa ofisi ya mbunge wanapaswa kuwa na sifa ambazo bunge limeanisha na wanapaswa kupewa mikataba. Lakini akakiri ni kweli idadi kubwa ya wabunge hawapeleki mikataba. Wanawapa ajira kwa midomo jambo ambalo linakuwa gumu wakati wanadai mishahara/haki zao. Na ameniomba nisistize kuhusu mikataba. Ni jukumu la wanaoajiriwa na mbunge katika ofisi yake pia kuomba mikataba, na sio kukubali kufanya kazi kiholela, unakuja kufukuzwa kazi huna pa kudai maana hauna mkataba wa maandishi, na wakati serikali inafanya kazi kwa maandishi na kwa nyaraka.
Hivyo ni muhimu bunge kama chombo kinachopaswa kuisimamia serikali kionyeshe mfano wa kujisimamia wenyewe na kusimamia wabunge wake. Kila mbunge lazima awe na jukumu la kuhakikisha anapeleka mikataba ya ajira za watu hao ndani ya muda utakaowekwa toka achaguliwe au ateuliwe kushika wadhifa huo wa mbunge. Na apeleke na akaunti namba za watumishi hao ili bunge badala ya kumuingizia Mbunge mishahara ya watu hao, basi kila mtu aingiziwe mshahara wake yeye mwenyewe.
Wakilipwa watawezwa kukatwa kodi na kuchangia maendeleo ya Taifa. Hapa tunaongelea walipa kodi wapya zaidi ya 1100 hapa ambao hivi sasa hawalipi kodi sababu mfumo sio mzuri na ambao pia hawalipwi wanachostahili.
Na ni aibu kubwa kwa Mbunge ambaye anaitwa Mheshimiwa kuwa mwizi wa posho ambazo zinastahili kwenda kwa wasaidizi wake, ambao pia wengine ni wapiga kura wake.
Hivyo nihitimishe kwa kumuomba na kumsihi Mh. Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania walau katika bunge lako hili tukufu uweze kuliangalia jambo hili na kutumia busara yako kuweza kusimamia haki hizi na ajira hizi za watanzania wanaoonewa na kudhurumiwa haki zao na wabunge wako. Ili ajira hizi zirasimishwe na kuweza kuchangia katika ujenzi wa Taifa.
Mungu libariki Bunge, Mungu Ibariki Tanzania.
Deo Meck
- Wabunge wengi hawalipi mishahara kamili kama inavyotoka bungeni.
- Watumishi hao ambao ni watatu, Katibu, Dereva na Mhudumu wa ofisi hawapewi mikataba ya kazi na wabunge kinyume na agizo la Bunge.
- Wasaidizi hao wakidai haki zao wanafukuzwa kazi sababu hawana mikataba
- Ajira zao zirasimishwe ili waweze kulipa kodi na kuchangia maendeleo ya Taifa.
- Kuna wabunge toka wachaguliwe/kuteuliwa hawana wasaidizi hao na wanalipwa pesa za kodi za Watanzania kinyume cha utaratibu.