Speech therapy

Sumji

R I P
Jun 11, 2009
34
0
Jamani mwenzenu nahitaji msaada
nina mtoto wa kiume hivi sasa ana umri wa miaka 4 na miezi 3. Mpaka sasa haongei kwa mfulilzo yaani haunganishi vizuri sentensi. Anaweza kuongea maneno machache kama kuita majina ya watu, kusalimia na sentensi chache kama"naomba maji". Ameshaanza kwanda shule na maendeleo yake ni mazuri na mwalimu amemsifia kwamba anafanya vizuri ktk kuhesabu na kuimba isipokuwa hawezi kujieleza. Sasa najiuliza je ni kawaida kwa umri wake au lazima nichukue hatua ya kumpeleka kwa wataalam.ni mwanangu wa kwanza.

Naomba ushauri jamani
 
Wacha mashaka sumji, kimsingi kuna watoto huwa wanachelwa kuongea au wanachelewa kutambaa au kutembea kwahiyo husitilie shaka chochote bado ni mapema sana kuanza kuwa na mashaka. Na kama ana maendeleo mazuri darasani huoni kuwa mtoto yuko pouwa tu ila ni wasiwasi wako ukichukulia tena ni mwanao wa kwanza basi unamuangalia kama mboni ya jicho
 
Kama ni mtoto wa getini, hili linawaza kuchangia, jitahidi ajichanganye na watoto wa majirani.
Pili, inategemea huyo house girl(au mtu mliyekuwa anamlea/shinda nae), kama sio msemaji/mcheshi/anaependa watoto-hiyo pia yaweza kuchangia.
Jitahidi kuzingatia hayo unaweza kumbadilisha.
 
kawaone wataalamu hospitalini...wahi maema, 4 yrs? its very late....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom