Special thread: Kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)

Nakumbuka kipindi nafanya research chuo nilihangaika sana... Japo kiukweli wengi bei zao si rafiki...kuna mdau kaweka namba za wachina hapa jukwaani, jaribu kiwacheki alafu na mimi ntakuchekia namba za mtu wa hapo dsm kama bado ntakua nazo maana ni mda kidogo umepita toka niwasiliane nae!!
Mkuu nikupe heshima kwa hili somo la umwagiliaji ulolianzisha naamini utatusaidia wengi tunaolima kwa mazoea.
Ila nina jambo nataka unielimishe ukiwa kama mtaalam. Mie nina shamba maeneo uloyataja kule mawala TPC mkoani kilimanjaro na nimechimba kisima kinachotoa maji ya kutosha kwa umwagiliaji, tatizo linalotukabili wengi ni baadhi ya maeneo ardhi kuwa na magadi na maji ya kisima kuwa na chumvi chumvi na kusababisha mazao kudumaa.
Sasa mkuu swali linakuja ni namna gani naweza kupunguza magadi shambani au nipande aina gani ya mazao ambayo yataendana na eneo husika?
 
Mkuu nikupe heshima kwa hili somo la umwagiliaji ulolianzisha naamini utatusaidia wengi tunaolima kwa mazoea.
Ila nina jambo nataka unielimishe ukiwa kama mtaalam. Mie nina shamba maeneo uloyataja kule mawala TPC mkoani kilimanjaro na nimechimba kisima kinachotoa maji ya kutosha kwa umwagiliaji, tatizo linalotukabili wengi ni baadhi ya maeneo ardhi kuwa na magadi na maji ya kisima kuwa na chumvi chumvi na kusababisha mazao kudumaa.
Sasa mkuu swali linakuja ni namna gani naweza kupunguza magadi shambani au nipande aina gani ya mazao ambayo yataendana na eneo husika?
Habari yako mkuu!? Shukrani kwa swali lako zuri mkuu! Nlikua hapo Tpc kiwandani na wao pia wana hiyo shida tena kubwa sana!!

Ki uhalisia moja kati ya sababu nyingi za chumvi chumvi ardhini ni maji!! Swali ni je, hayo maji hayana chumvi??? Kwasababu umesema ardhi ina chumvi solution zipo nyingi ila ya kwanza kabisa ni kupima chumvi kwenye maji na kama yakiwa na chumvi msije yatumia tena!!

Pili ni kupanda mazao ambayo yanastahimili ardhi yenye chumvi mfano mahindi japo nayo hayastahimili kwa kiwango kikubwa!!

Tatu punguza matumizi ya mbolea za kiwandani kwa kiwango kikubwa maana inaweza changia madhara zaidi.

Hiyo ni kwa kifupi mkuu...nadhani hii ntaizungumzia kwa undani zaidi wiki hii au ijayo mwanzoni!!!

NB: mazao ya mboga mboga hayataweza fanya vizuri kwenye ardhi kama hiyo unless hatua stahiki zichukuliwe kuondoa chumvi ardhini. Karibu
 
Habari yako mkuu!? Shukrani kwa swali lako zuri mkuu! Nlikua hapo Tpc kiwandani na wao pia wana hiyo shida tena kubwa sana!!

Ki uhalisia moja kati ya sababu nyingi za chumvi chumvi ardhini ni maji!! Swali ni je, hayo maji hayana chumvi??? Kwasababu umesema ardhi ina chumvi solution zipo nyingi ila ya kwanza kabisa ni kupima chumvi kwenye maji na kama yakiwa na chumvi msije yatumia tena!!

Pili ni kupanda mazao ambayo yanastahimili ardhi yenye chumvi mfano mahindi japo nayo hayastahimili kwa kiwango kikubwa!!

Tatu punguza matumizi ya mbolea za kiwandani kwa kiwango kikubwa maana inaweza changia madhara zaidi.

Hiyo ni kwa kifupi mkuu...nadhani hii ntaizungumzia kwa undani zaidi wiki hii au ijayo mwanzoni!!!

NB: mazao ya mboga mboga hayataweza fanya vizuri kwenye ardhi kama hiyo unless hatua stahiki zichukuliwe kuondoa chumvi ardhini. Karibu
Nashukuru kwa majibu kiongozi, ni ukweli maji yana chumvichumvi kwa mbali, hii ndio kusema maji ndio yanasababisha udongo kuwa na magadi au? Naomba ufafanuzi zaidi mtaalam.
Na endapo nitaweza kuchimba kisima kirefu zaidi kuna uwezekano wa kupata maji yasiyo na chumvi? Sababu hiki kisima cha sasa vijana walichimba kwa zana za mkono.
 
Nashukuru kwa majibu kiongozi, ni ukweli maji yana chumvichumvi kwa mbali, hii ndio kusema maji ndio yanasababisha udongo kuwa na magadi au? Naomba ufafanuzi zaidi mtaalam.
Na endapo nitaweza kuchimba kisima kirefu zaidi kuna uwezekano wa kupata maji yasiyo na chumvi? Sababu hiki kisima cha sasa vijana walichimba kwa zana za mkono.

Mkuu kama nlivyosema hapo mwanzo, nimeshakua pale tpc sugar! Na chumvi ya hapo inatokana na asili ya udongo na maji! So yes, kwa kiasi flani maji yanachangia hasa kama umeyatumia mda mrefu kwa umwagiliaji! Kwenye maelezo yako umesema ni watu walichimba kisima ambacho si kirefu, hii inaonyesha dhahiri maji yatakua na chumvi japo ni vyema ukayafanyia vipimo ili upate jibu la moja kwa moja!!!

Kwa swali lako la pili, yes kama ukichimba kisima kirefu kuna uwezekano ukapata maji salama japo nayo yatahitaji kupimwa!! Nnasema hivyo maana pale tpc mashamba yao yana visima virefu ambavyo ndio wanatumia sana kwenye umwagiliaji kuliko maji ya kikuletwa na karanga na maji ya chem chem kutoka eneo la kahe!!
 
Naishukuru serikali hasa ya awamu ya nne kwa kuweka mkazo wa kilimo hasa cha umwagiliaji, japo hawakufanikiwa sana ila ni lazima tukubaliane kwamba kilimo kwa sasa hasa cha umwagiliaji hakiwezi fanikiwa kama hakuna juhudi za kuwezesha kilimo cha umwagiliaji!!

Kilimo cha umwagiliaji kwa maendeleo ya viwanda na jamii kwa ujumla!


NB: bado napokea mawazo ya mada ya wiki hii. Karibuni sana!
 
Ni kweli kabisa mkuu!!! zipo pia hasara kama uongezwaji wa chumvi kwenye ardhi, hii nayo ni hatari zaidi, infact tutaiongelea kwa undani zaidi kadri muda utavyiruhu!!

Nakumbuka nikiwa mwaka wa nne chuoni mwalimu alituonyesha mfumo ambao walikua wana develop kwa ku modify drip systems zilizopo nadhani hawajamaliza, ila ukikamilika utakua nafuu sana hawa kwa watumiaji wa chini!!

Kuna njia pia ya umwagiliaji wa ndoo na madumu yaani yanankua yanatobolewa, hii njia ni mahususi kwa small scale farmers na sizani kama unaweza tumia kwa mashamba makubwa!
View attachment 425040
source: HOME
View attachment 425041

Kwa tunapoenda drip irrigation itakua ni ya mwimu sana hasa kwa changamoto za mvua na uongezekaji wa idadi ya watu duniani ambao unaenda sambamba na uhitaji mkubwa wa chakula ambacho kinapatikana kupitia kilimo!

Ni kweli kabisa mkuu mawakala wengi bei zao sio rafiki, lakini tujue hiyo ni initial cost ila ukisha install unaweza itumia muda mrefu tu!!
Hii nimeependa sana nahitaji kufahamu jinsi ya kuitumia!!!
 
Baada ya kutangazwa upungufu wa mvua hasa miezi ya 10 mpaka 12 na mamlaka ya hali ya hewa katika maeneo mengi ya tanzania, bado challenge ina baki ni vipi mkulima ataweza kulima huku tukijua kuna upungufu wa mvua??

Nadhani ni mida sahihi kwa maeneo yanayopata mvua kuanza kuvuna mvua kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kilimo!!

Bado tunapokea mawazo na ushauri kwa ajili ya mafa zetu!!!
 
Wadau next topic inaweza kua moja kati ya hizi!!
1. Aina ya Vyanzo vya maji kwa ajili ya umwagiliaji. Pia tutaangalia madhara yanayoweza tokea kama hutatumia maji kwa uangalifu

2. Elimu kuhusu pump na jinsi ya kuchagua pump kulingana na mahitaji

3. Jinsi ya kukadiria mahitaji ya drip pipes/ drip line unapotaka kununua

Hayo ni mawazo yangu, kama utakua na wazo usisite kuweka ili tulifanye kama mada! Karibuni

Mkuu Upepo wa Pesa kwema? Hongera kwa uzi uliojaa elimu ya bure kabisa kuhusu kilimo cha umwagiliaji, kwa kweli kabisa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa inabidi tuachane na kilimo cha kutegemea mvua na tujikite katika kilimo cha umwagiliaji na ningependekeza kama una ujuzi pia wa kilimo cha green house kama kuna uwezekano huo unamwaga somo pia kuhusu green house mkuu, hapa nchini kuna kampuni ina deal na vifaa vya green house lakini wanauza kwa bei ya ghali sanaa hakika bei yao sio rafiki kwa mkulima wa hali ya chini je tunafanyaje na sisi ambao tunataka kumiliki green house lakini we can't afford bei ya wale jamaa??
Nirudi kwenye mada yetu mkuu me binafsi ningeomba ujadili topic ya jinsi ya kukadiria mahitaji ya dripline/pipes kabla ya kununua hii itatusaidia wengi kuingia kichwa kichwa kabla ya kununua na pia hata kupunguza gharama za kumlipa mtu afanye hiyo kazi wakati unaweza kufanya mwenyewe.

Nikupe pongezi nyingine mkuu kwa uzi mzuri, Nawasilisha.

NB:Kuhusu kilimo cha green house nitoa pendekezo tuu sio lazima tujadili kwenye uzi huu iyo itategemea mkuu Upepo wa Pesa atakavyo pendekeza kama ataruhusu tujadili humu au akafungua uzi mwingine mahususi kwa ajiri ya GH na link akaiweka juu ya uzi huu naamini itakua msaada na wengi mtakubaliana na mimi kuwa kilimo cha green house kinaendana sana kilimocha umwagiliaji ingawa sio lazima sana kuwa na green house endapo kama unafanya kilimo cha umwagiliaji.
 
Tatzo la watanzania tunaumizana sana...mtu anataka 1.8-2m kwa drip pipes za heka moja while for io hela ukiagiza kutoka china unapata pipes za heka 5....
+86 150 7569 8509 add hio no then anza kuchat na huyo dada watsap mpe requirements zako atakutengenezea design na kukuuzia drip pipes na kukutumia hadi tz unachotakiwa ni kulipia gharama za bandari,wakala na tra utoe mzigo wako...
+8675533556323 hii no ni kwa wale wanaohitaji solar water pump systems kwa wale ambao hawapo karibu na mito...with solar power pump system & drip irrigation u r one point close kua mkulima wa kisasa...Goodluck guys
Mkuu kwema? Hivi drip pipes hazina msamaha wa kodi??
 
Je ni nini madhumuni ya umwagiliaji?? (ukiona unatoka nje ya haya jua haufanyi umwagiliaji bali unafanya kitu kingine kabisa)

Tumeshaona nini maana ya umwagiliaji (irrigation), tuliona ni kitendo cha kuweka maji kwenye mmea kwa njia isiyo asili (in artificial way). Tunapofanya kwa njia ambayo si asili ya umwagiliaji basi tunakua tuna uwezo wa ku-control maji tunayotaka kuweka kwenye mmea kwa kiwango, eneo na kiasi kinacho hitajika!

Tunapofanya umwagiliaji kuna madhumuni mengi ambayo mmwagiliaji anataka kuyafanikisha ili aweze kufanya umwagiliaji bila kuleta madhara kwenye jamii na mazingira kwa ujumla! yafuatayo ndiyo ambayo yako common:

1. Kuupatia mmea maji yanahitajika kwa ajili ya ukuaji wa mmea (to supply water required for plant growth).

Kama tunavyojua maji hayahitajiki na mmea kama chakula au source of nutrients, ila kazi kuu ya maji kwenye mmea ni kusafirisha madini au nutrients kutoka kwenye udongo na kupeleka kwenye mmea kupitia mizizi (soil-water-plant continuum). Bila maji mmea unakufa si kwa sababu tu umekosa maji bali umekosa mechanism ya kuuwezesha kupeleka chakula kwenye mmea kutoka kwenye udongo!! Hivyo basi tunapomwagilia maji ni ili kuuwezesha mmea kupata madini au chakula kutoka kwenye udongo kwenda kweye mizizi na kusambaza kwenye sehemu nyingine za mmea!!

2. Kupunguza upotevu wa maji (to use water efficiently).

Upotevu wa maji sio dhumuni la umwagiliaji, na kama tunavyojua maji sasa yanaanza pungua kutoka vyanzo mbali mbali, sasa ni busara kama tukitumia kidogo yaliyopo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao! Na ili tutumie maji vizuri katika umwagiliaji ni lazima tufanye umwagiliaji unaojali na kupunguza upotevu wa maji!

Wengi wanapomwagilia wanahakikisha mpaka maji yame tuwama kabisa ndio wana ridhika, ki uhalisia haya ni makosa makubwa na ni upotevu wa maji!!! Zaidi ya yote ni uharibifu wa mazao na ardhi!

3. Kupunguza uharibifu wa ardhi (to avoid/reduce soil erosion)

Kama nilivyosema awali umwagiliaji unatupa mazao ila umwagiliaji pia unaweza kuwa bomu!! Umwagiliaji hasa wa mifereji unaweza kuleta madhara makubwa kwenye ardhi kama usipo angaliwa kwa umakini hasa katika spidi ya maji yanayoingia shambani!

Maji yanapotuwama yanaweza pelekea upoteaji wa virutubisho (leaching of nutrients) na kuua microorganisms wanahitajika katika kutengeneza rutuba ya udongo! Pamoja na kwamba tunataka kuzalisha mazao, ni vyema pia tukajali na kuilinda ardhi yetu!!!

Hayo ndiyo madhumuni makuu matatu ya umwagiliaji, na kitaalamu tunaamini kwamba the main objective of irrigation is to maintain plant root zone at field capacity. Sasa ni vyema tukiwa tunafanya umwagiliaji tuangalie madhumuni hayo ya umwagiliaji ili kuhakikisha umwagiliaji unakua na manufaa na sio madhara katika mashamba na jamii kwa ujumla!
 
Mkuu kuna kipindi nakumbuka bidhaa au tools za kilimo zilikua hazina kodi sasa sijui kama mpaka leo kodi imeondolewa au vipi!!
Na mimi nakumbuka ilikua hivyo sasa jamaa kanishtua alivyosema unalipia kodi ndio maana nikamuuliza atupe jibu sababu anamefanya manunuzi muda si mrefu, ila sidhani kama wameweka kodi siku hizi maana tunanyonyana wenyewe sasa.
 
Back
Top Bottom