Special thread: Kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
21,251
34,198
Habari wana jamvi!

Leo nimeona si vibaya kushare nanyi kidogo nnachojua kuhusu kilimo cha umwagiliaji, na katika uzi huu nitajaribu kuelezea kile nnachojua na pia kupata mawazo kutoka kwa wadau mbali mbali hasa wakulima ambao kwa namna moja au nyingine ndio main actors katika sector ya umwagiliaji!

Kwa miaka kadhaa iliyopita mashirika mbali mbali na serikali vimekua vikiweka mkazo sana katika kilimo cha umwagiliaji, nadhani wote tunakumbuka kilichotokea mwaka huu na mwaka jana ambapo wakulima wengi walipata hasara kwa kulima alafu mvua ikakatika mazao yakiwa katika critical stage, stage ambayo maji ni lazima yawepo kwa ajili ya mimea shambani!

Kwa kifupi katika ulimwengu wa sasa hakuna kilimo cha kibiashara kitafanikiwa bila kuwa na mfumo sahihi na mathubuti kwa ajili ya umwagiliaji!!

Kwa kuanza, leo nitaomba tujifunze/tujikumbushe aina mbali mbali za umwagiliaji au njia ambazo mkulima anaweza kufikisha maji kwenye mmea.

1. Umwagiliaji wa maji kwa kutumia mifereji (furrow/surface irrigation method)

Huu ni umwagiliaji ambao mkulima anatumia mifereji kufikisha maji shambani, umwagiliaji huu unaaminika kutumiwa miaka mingi sana iliyopita, kwa kifupi ndio umwagiliaji mkongongwe (oldest) kushinda njia nyingine za umwagiliaji! Pamoja na faida zake ila umwagiliaji huu unahitaji maji mengi sana na pia unapelekea upotezaji mwingi sana wa maji shambani na uharibifu wa ardhi. Kwa kifupi sio bora ukilnganisha na njia nyingine za umwagiliaji. Katika kundi hili pia kuna border irrigation method

2. Umwagiliaji wa matone (drip irrigation)

Huu ni umwagiliaji wa kisasa kabisa ambao unatumia maji machache na katika njia ambayo ni fanisi. Umwagiliaji huu unaingina katika kundi la “pressurized irrigation” ambapo mara nyingi mtumiaji anahitaji pump kama mechanism ya kulift/kupush/kusukuma maji. Lakini pia umwagiliaji huu unaweza kutumia njia ya “gravitation” ambapo mmwagiliaji anaweka maji kwenye pipa lililo juu (la simtank) na kuruhusu maji yashuke kwa kani mvutano kwenda kwenye drip pipes!

3. Sprinkler irrigation

Hii inatumia njia ambayo maji yanarushwa hewani kama mvua na kushuka kwenye mimea, hii njia pia inaangukia kwenye kundi la “pressurized irrigation” kama ilivyo drip irrigation. Katika njia hii ni lazima mmwagiliaji awe na pump au mechanism yoyote itayotoa pressure!

Ziko njia nyingi za umwagiliaji lakini hizi ndio common kwa maeneo mengi hapa kwetu Tanzania na duniani kwa ujumla!! Katika uzi huu tutajifunza umwagiliaji kwa ujumla, mahitaji ili kuanzisha kilimo cha umwagiliaji, changamoto zake kupitia kwa members wengine humu ambao pia watakua na mawazo au mchango kwenye hii sector na zaidi ya yote tutapitia njia moja baada ya nyingine na kujifunza kwa undani zaidi!

Kama una nia ya kufanya kilimo biashara, basi hakuna jinsi utakwepa kilimo cha umwagiliaji hasa ukizingatia mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka ya hivi karibuni

Karibuni sana wanajamvi kwa maswali, mawazo katika hii sector ya kilimo hasa cha umwagiliaji!

SEHEMU YA KWANZA Link: Things to consider before you start to irrigate
SEHEMU YA PILI : Madumuni ya umwagiliaji, post namba 75
 
Umwagiliaji wa matone (drip irrigation) katika zao la mahindi
image 1.JPG
 
Pamoja na hasara zake njia ya kwanza(surface irrigation) imekua ikitumika na wakulima wengi wa kada ya chini kwa sababu yakua na gharama ndogo kwa mwanzo kuliko hizo njia nyingine.
Uko sahihi kabisa mkuu! na ndio maana mpaka leo njia hii ipo hai sehemu nyingi ikiwemo hapa kwetu!

Kuna namna nyingi ambazo wataalam wamebuni ili waweze kupunguza upotevu wa maji katika hii njia na moja wapo ni kuondoa feeder streams zinazopeleka maji kwenye mifereji inayoingia shambani. Wamefanya hivi kwa kuondoa feeder streams kwa kuzi-replace na pipes. Tutaiona hii pia kwa undani kadri muda utavyo ruhusu!
 
Ndugu upepo wa pesa uliniambia nibaki MMU tu kwingine haunitaki lkn nimevutiwa na uzi wako je naweza kukuuliza? I'm real serious
Nashukuru sana moniccca na tofauti zetu tusizipe nafasi hapa, infact yashapita hayo!! feel free to ask moniccca naamini kwa nnachokijua pamoja na msaada wanajamvi tutapata solution ya swali lako! once again, welcome!
 
Nakubaliana na wewe Upepo wa Pesa hasa kuhusu upotevu wa maji na kuharibu udongo, pia inasababisha kustawi kwa vitu visivyohitajika na kuongeza gharama za palizi.

Kuna yeyote anaefaham ni wapi wanatengeneza mifumo ya kienyeji ya drip irrigation inayoweza kuwa ya bei nafuu lakini ufanisi bora? Kwa wakulima wadogo itasaidia sana. Tukumbuke sasa hivi ukame unatishia hali ya mazao kutokana na mito/mabwawa kukauka. Drip irrigation itasaidia sana maji kidogo kunufaisha wakulima wengi. Mifumo hii ina gharama sana kwa ukinunua kwa mawakala au kiwandani, inawawia vigumu wakulima wengi wanaoanza au wenye mitaji midogo.
 
Nakubaliana na wewe Upepo wa Pesa hasa kuhusu upotevu wa maji na kuharibu udongo, pia inasababisha kustawi kwa vitu visivyohitajika na kuongeza gharama za palizi.
Ni kweli kabisa mkuu!!! zipo pia hasara kama uongezwaji wa chumvi kwenye ardhi, hii nayo ni hatari zaidi, infact tutaiongelea kwa undani zaidi kadri muda utavyiruhu!!
Kuna yeyote anaefaham ni wapi wanatengeneza mifumo ya kienyeji ya drip irrigation inayoweza kuwa ya bei nafuu lakini ufanisi bora? Kwa wakulima wadogo itasaidia sana.
Nakumbuka nikiwa mwaka wa nne chuoni mwalimu alituonyesha mfumo ambao walikua wana develop kwa ku modify drip systems zilizopo nadhani hawajamaliza, ila ukikamilika utakua nafuu sana hawa kwa watumiaji wa chini!!

Kuna njia pia ya umwagiliaji wa ndoo na madumu yaani yanankua yanatobolewa, hii njia ni mahususi kwa small scale farmers na sizani kama unaweza tumia kwa mashamba makubwa!
local 2.jpg

source: HOME
local.jpg

Tukumbuke sasa hivi ukame unatishia hali ya mazao kutokana na mito/mabwawa kukauka. Drip irrigation itasaidia sana maji kidogo kunufaisha wakulima wengi. Mifumo hii ina gharama sana kwa ukinunua kwa mawakala au kiwandani, inawawia vigumu wakulima wengi wanaoanza au wenye mitaji midogo.
Kwa tunapoenda drip irrigation itakua ni ya mwimu sana hasa kwa changamoto za mvua na uongezekaji wa idadi ya watu duniani ambao unaenda sambamba na uhitaji mkubwa wa chakula ambacho kinapatikana kupitia kilimo!

Ni kweli kabisa mkuu mawakala wengi bei zao sio rafiki, lakini tujue hiyo ni initial cost ila ukisha install unaweza itumia muda mrefu tu!!
 
nimetumia hiyo furrow mifereji ipo sambamba na mteremko imeanza kuleta mmomonyoko. nataka niibadilishe ikae perpendicular na mteremko
 
nimetumia hiyo furrow mifereji ipo sambamba na mteremko imeanza kuleta mmomonyoko. nataka niibadilishe ikae perpendicular na mteremko
Furrows should follow the contours of the field but have just enough slope to carry irrigation water.
 
nimetumia hiyo furrow mifereji ipo sambamba na mteremko imeanza kuleta mmomonyoko. nataka niibadilishe ikae perpendicular na mteremko
Yes. Uko sahihi ikiwa sambamba na mteremko maji yakua na speed au mwendokasi mkubwa sana ambapo itapelekea mmomonyoko wa ardhi ma kupoteza rububa ya udongo!! Zaidi ya yote maji yatakua hayaingii ardhini kwa kiwango stahiki!!!

Ili kupunguza speed ya maji na uharibifu wa ardhi...unaeza iweka mifereji perpendicular to the slope lakin vizuri ikawa kwenye angle flani zaidi ya 90 degree!! Hapa utapata speed nzuri na maji yataingia ardhini ya kutosha na utaitunza ardhi yako!!

Usisahau pia kupanda majani au miti sehem ambazo ziko hatatini kupata soil erosion!

Karibu mkuu
 
Nataka kujua
1. Accre moja inakula roler ngapi za drip pipe?
2. Bei ya roler moja ni shilingi ngapi?
3. Hizo drip pipes zinadumu kwa muda gani?
4. Hapa kwetu nani no suppliers wa kuaminika kabisa.

Nitashukuru sana sana nikipata majibu haya
Mkuu kabla ya yote lazima ujue spacing ya zao lako!! Ukishajua...then ujue eneo lako ni eka ngapi!!! ...na kuhusu kudumu kwa drip ina tegemea ..je utazukia au utaweka juu...na je mazingira yakoje??? Jua kali..zinakanyagwa mara kwa mara!! ?? Ngoja nikitulia ntakuja na data kamili!!!
 
Back
Top Bottom