South Sudan independence photos

Asante kwa kunifafanulia kwa undani jambo hili....ki ukweli naweza kukiri kuwa ni uvivu wa kufuatilia lakini nimefurahi sana hawa jamaa kupata uhuru......nimekuwa nikikutana nao wengi wao Kenya na kuwahurumia jinsi ambavyo unaweza kufeel kuwa mkimbizi katika nchi yako.......sasa kingine.....mbona Kenya imekuwa mstari wa mbele sana katika ukombozi wao....nikinyanyua ramani yangu naona Kenya ndio imepakana nao kwa kiasi kidogo sana ukilinganisha na Uganda, DRC, CAR na hata Ethiopia....nini Kenya inataka hapa......

Wakati wakipigana vita na waarabu walikuwa wanasaidiwa na Israel, nchi zingine zote ziliwabania, misaada hiyo ilikuwa inapitia Kenya. Pili kambi za wakambizi wao nyingi zipo Kenya, kama vile sisi tulivyo na wakimbuzi wa Rwanda/Burundi na DRC, tatu Kenya ina majority ya wakiristo na wale wasudan wa kusini ni wakiristo. North Uganda na mipaka mingine uliyoitaja ina influence za waislamu ambao naturally ni wapambe/watwana wa waarabu.
 
Safi sana..
Miaka 50 inayokuja uhuru wao utastawi
Na wananchi watakuwa na maisha bora...

Kila lakherii..:)
 
Preta
Darfur ipo mangaribi, na wenyeji wa huko ni Waislam ila tatizo lao ni WAISLAM WEUSI, NDO MAANA HAWA WAARABU wanawabagua wakajionea njia sahihi ni kubeba silaha na kuanza kupigana dhidi ya udhalimu wa hawa waarabu.

Kusini mwa Sudan kunakaliwa na watu weusi TII, hawa jamaa wengi wao ni wakristu na wengine hawana DINI KABISA walianza kupigana kupinga udhalimu wa waarabu kutoka North tangu miaka ya sabini, Hawa Waarabu ni ndugu zetu na tunafuata Dini yao lakini walichowafanyia hawa jamaa wa kusini mwa Sudani naamini huyu Mungu wa Ibrahim na Isaka anayajua, huwezi amini mpaka miaka ya karibuni walikuwa wanawachukua watu kutoka Kusini mwa Sudani kama Slaves, na wanawaona kama sio binadamu kabisa.

C'moon bro! civility is needed in this one, can't u see that u r being racist? What is weusi tiiiiii? describing a person that way in some countries tena zisizo za Africa unaweza kushtakiwa. We need to refrain from this kind of language b'coz people are just people.
 
Halafu hawa jamaa pamoja na kuwa wakristu, wanatumia kiarabu kuwasiliana. Nimesikia jana kwenye sherehe za uhuru. Wana lugha ngapi hawa?
 
We hujui weusi ndo wenye raha we unafikir kwanin kina bill gates hawachelew kutembelea afrika

haha hawa wenzetu wamezidi

126495-south-sudan-7-of-10.jpg
 
Very nice. Happy birthday to you beloved South Sudan!!!

Kulikuwa na miungano ya mataifa kama Senegambia, yaliachana na kuwa Senegal na Gambia na taifa kama Sudan limegawanyika sembuse Tanzania? Wazanzibari anzisheni mchakato wa kujitenga tumechoshwa na kelele zenu ili mpate maendeleo ya haraka kama mnavyojidai. Anzeni haraka sisi tubaki na Tanganyika yetu!
 
Asante kwa kunifafanulia kwa undani jambo hili....ki ukweli naweza kukiri kuwa ni uvivu wa kufuatilia lakini nimefurahi sana hawa jamaa kupata uhuru......nimekuwa nikikutana nao wengi wao Kenya na kuwahurumia jinsi ambavyo unaweza kufeel kuwa mkimbizi katika nchi yako.......sasa kingine.....mbona Kenya imekuwa mstari wa mbele sana katika ukombozi wao....nikinyanyua ramani yangu naona Kenya ndio imepakana nao kwa kiasi kidogo sana ukilinganisha na Uganda, DRC, CAR na hata Ethiopia....nini Kenya inataka hapa......

Ni kweli Kenya walijitoa Muhanga kuhakikisha hawa jamaa wanapata uhuru, Zipo sababu nyingi saana, Ya kwanza ni BIASHARA, kenya iliamini South Sudan Huru watanufaika nayo saana kibishara, Hili halina ubishi, baada ya kutiliani saini makubaliano ya amani haikuchukua miezi wakenya walianza kumiminika South Sudan kwa wing Mwishoni mwa mwaka 2009 kulikuwa na Wakenya zaidi ya elfu kuninatisa wanafanya kazi kwenye mashirika ya kutoa misaada, makampuni binafsi, na wengi walianzisha biashara zao nyingi tuLingine makampuni mengi ya kesnya yalikimbilia Kusini mwa sudan na kufungua maofisi yao, mfano mzuri ni Kenya Commercial Bank KQ na mengineyo

Kingine Kenya wanataka wawe ndio wanasafirisha mafuta yote ya kusini mwa sudan, ili kufanikisha hili wameshaanza/wako mbioni kujenga bandari Mpya ya LAMU pamoja na reli itakayofika JUBA na Ethiopia, Hili nadhani raisi Kibaki tayari ameshalibariki na watakuwa kwenye maandalizi ya mwisho. kuna uwezekano mkubwa Likajengwa BOmba la Mafuta kutoka South Sudan mpaka bandari mpya la Lamu

Kumbuka kwamba Geography ya kenya pia imesaidia wao kunufaika tangu huu mgogoro unaanza mpaka unakwisha, mashirika mengi yanayotoa misaada kusini mwa Sudan makao yao makuu yapo Nairobi, wanatumia saana viwanja vyao vya ndeke kusafirisha misaada pamoja na mahitaji mengine. Silaha pia zote zinazotumiwa na Jeshi la SPLAA zinanunuliwa/ zilikuwa zinanunuliwa na Wakenya, kama utakumbuka kuna Meli iliyokuwa imebeba silaha ilitekwa na maharamia wa kisomali, Wakenya wakasema silaha ni za jeshi lao kumbe ilikuwa danganya toto. Pia viongozi karibu wote wa ngazi za juu wa SPLAA na familia zao walikuwa wanaishi Nairobi. Garang yeye alikuwa na makazi Ethiopia ila mara nyingi hata Nairobi, na Kampala alikuwa anafika kila mara kwa ajili ya logistic

Hawa jamaa walikuwa washirika wakubwa saana wa UGANDA na mara nyingi JOHN Garang alikuwa na makazi kampala lakini baada ya Garang kufa kwa ajali hawana imani kabisa na Mseveni wanahisi/hata mke wa Garang alishasema hawa jamaa ndio waliomuuwa Garang, Hata jana sikumuona M7 labda alikuja baadae

Hope kwa haya maelezo utapata mwanga kidogo
 
Wakati wakipigana vita na waarabu walikuwa wanasaidiwa na Israel, nchi zingine zote ziliwabania, misaada hiyo ilikuwa inapitia Kenya. Pili kambi za wakambizi wao nyingi zipo Kenya, kama vile sisi tulivyo na wakimbuzi wa Rwanda/Burundi na DRC, tatu Kenya ina majority ya wakiristo na wale wasudan wa kusini ni wakiristo. North Uganda na mipaka mingine uliyoitaja ina influence za waislamu ambao naturally ni wapambe/watwana wa waarabu.

South Sudan imesaidiwa saana na UGANDA,Ethiopia,Kenya, Tanzania,Eritrea, na mataifa mengi mno ya Ulaya,Sidhani kama hizi nchi zimeshawahi wabania, Kwa taarifa yako Mtoto wa kwanza wa Garang,ambaye sasa ni mwanajeshi ndani ya SPLAA, amesoma Tanzania, Uganda imewasaidia saana hawa jamaa si kwa silaha, mafunzo, Mpaka leo kaskazini mwa uganda kuna kambi kadhaa za mafunzo za SPLAA. Garang kwa safari zake za nje alikuwa anatumia ndege binafsi ya M7. Operation base ya Garang ilikuwa Ethiopia, nakumbuka kuna kipindi SPLAA walizidiwa nguvu baadaya ya Libya kumpa bashiri ndege za kivita pamoja na silaha ndogondogo, ilibidi Eritrea wapeleke wanajeshi Kusini mwa Sudan waende wakaokoe jahazi

Kumbuka sio Israel pekee hata marekani,Norway, UK; Canada na mataifa mengine walitoa msaada mkubwa saana kwa SPLAA, nakumbuka kipindi vita ilikuwa inaendelea Kulikuwa na NGO moja tu kutoka Norway ilikuwa inatoa misaada South Sudan.
Kutokana na kuonewa kwa miaka mingi, wingi wa maliasili walizonazo Nchi nyingi zilikuwa zinasaidia kwa kila namana isipokuwa china tu, cha kushangaza niliwaona jana wanatangaza wanafungua ubalozi JUBA wiki hii
 
kwa madhila waliyopata wangebadili hata jina kabisa. neno sudan lisiwepo
 
Back
Top Bottom