Sony na teknolojia ya S-Force Front Surround, Sound Pressure Horn

CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,789
1,782
Utazamaji wa filamu wa sasa sio kama ule wa zamani ambapo unasimuliwa matukio kwa kutumia picha zinazosonga (movie) na sauti kwenye mifumo ya stereo ukiwa umeketi sebuleni au kwenye ukumbi wa sinema bali sasa surround sound technology kujumlisha na video za 3D imewezesha mtu ‘kupelekwa kwenye tukio' (kiakili) badala ya kusimuliwa tu.

Unaangalia video ya wanyama unaona chatu anakuja unaingiwa na hofu ukifikiri kuwa uko pale pale porini, unataka kukimbia ukigeuka unagundua upo sebuleni kwako😳 Hata hivyo bado wataalamu wanahangaika kuboresha zaidi utazamaji wa filamu.

Kampuni ya Electronics ya Sony imetokeza teknolojia zinazoboresha surround sound technology. Technology hizo ni hizi hapa chini👇

1.1 S-force Front Surround
Hii teknolojia sio mbadala wa surround sound technology kama Dolby Digital au Dolby Atmos® bali inaziboresha hizo teknolojia kama tutakavyoona. Pia ieleweke kuwa surround sound technology inakuwa encoded kwenye movie wakati wa production lakini S-force Front Surround inapatikana kwenye tv au kwenye audio systems na inafanya kazi wakati wa movie playback kwa kudecode Surround Sound codecs za Dolby. Kwa kuongezea, S-force Front Surround ni entirely virtual lakini Surround sound signals zinaweza kukufikia physically yaani kila channel na spika yake au virtually yaani idadi ya channel kubwa kuliko idadi ya spika ikimaanisha baadhi ya signals zinatoka labda kwenye spika za mbele na kuzunguka ili zikufikie kutoka kulia/kushoto au nyuma yako pale ambapo mfano channels zipo 6 lakini spika zipo 3 tu.

Ili kuelewa jinsi S-force Front Surround inavyofanya kazi tuone kwanza kile kinachofanywa na surround sound technology. Wakati wa film production sauti zinapangwa (mixed) katika channels(mikondo)mbalimbali na kila channel inaelekezwa kwenye spika. Hii inamaanisha kama movie imepangwa katika channels 6( yaani 5.1) hii ina maana kuwa home theatre systems inayohitajika ni ya spika 6. Hapo ni spika ndogo 5 yaani mbele kulia 1,kushoto 1 katikati 1 halafu nyuma kushoto 1na kulia 1. Hiyo 1 inayobaki ni subwoofer. Kama movie iko encoded katika 7.1 basi kutakuwa na spika 2 za ziada moja ikiwa katikati kushoto kwako na nyingine kulia jumla zitakuwa 8. Mpangilio huu ni kwa teknolojia ya Dolby Digital au DTS. Haya ni mapinduzi makubwa kutoka stereo systems ambapo channels zipo 2 na spika 2 mbele yako na sauti zote zikitoka mbele yako. Tofauti ya stereo na surround sound ni ipi?

Tuchukue mfano rahisi. Unaangalia movie ambapo kuna scene inayoonyesha mvua inanyesha. Kwenye stereo sauti ya mvua,radi na kila sauti itatoka mbele yako tu. Hakuna uhalisia hapo. Lakini kwenye home theatre system utasikia mvua ikinyesha pande zote yaani mbele, kulia na kushoto na nyuma. Na (kama tutakavyoona baadaye kuhusu maboresho zaidi ya surround sound) mvua pia utaisikia kutoka juu. Isitoshe, radi inapiga upande wa kushoto kwenye scene halafu unasikia sauti ya radi, "paaaa", ikitoka kwenye spika za kushoto, kisha mgurumo unaofuata toka kwenye subwoofer unajaza chumba kizima🤔. Je si utahisi upo kwenye tukio unaloangalia? Ndio lengo la surround sound technology. Mpaka hapa tunaelewa umuhimu wa surround sound technology.
Sasa tuone jinsi unavyopata full surround sound signals kwenye sebule yako.

Ni kwamba huwezi kukaa sehemu yoyote sebuleni na kupata signal zote mfano 6, ukiacha signal ya subwoofer ambayo kwa kawaida inaenea chumba kizima, kuna sehemu katikati ya mzunguko wa spika ambapo signal hizo nyingine zinakutana (sound field) kulingana na mpangilio wa spika kwenye physical surround.(Pia hali ni hiyo hiyo kwenye virtual surround) Hii ni sehemu ndogo ya kukaa watu wachache tu. Kwenye kumbi za sinema spika zinaongezwa kitaalam kwa kila channel ili kupanua eneo au sound field ya surround signals ili watazamaji zaidi wanufaike na teknolojia hii.

Hapa kwenye sound field ndipo Sony wanapoingia na teknolojia ya S-force Front Surround. Teknolojia hii ya Sony inadecode dolby digital au dolby digital plus codecs kazi ambayo ingefanywa na Dolby Pro Logic IIx au Dolby Surround technology (au DTS neo:6 or DTS neural:X kama ni DTS codec). Matokeo yake ni kupanua hii sound field ili iweze kuaccomodate watazamaji zaidi. Hata hivyo kuna kitu cha ziada kwenye teknolojia hii ya S-force Front Surround. Kwa kuwa virtual surround systems hazifanyiwi calibration ili kujua sehemu sahihi ya kukaa kama ilivyo kwa physical systems, kupanuliwa kwa sound field kunasaidia kupata uwanja wa kutosha kukaa kwa bila kukosa signal yoyote. Hata kama upo peke yako unapata uhuru wa kukaa sehemu unayotaka.

Jambo lingine ni kwamba katika utazamaji wa filamu ili kuelewa story picha na mazungumzo(dialogue) ndio ya muhimu sana. Effects zinaongeza uhalisia katika sinema. Mfano utahisije ikiwa utaona helikopta inapita bila kusikia mgurumo wake? Au mtu anapiga kelele lakini husikii chochote? Movie itakosa mvuto na uhalisia na itachosha hata kama unaelewa nini kinaendelea. Muziki wa chinichini (underground music) ni kwa ajili ya kujiburudisha wakati unaendelea kufuatilia story ili usichoke. Lakini kama husikii vizuri mazungumzo utashindwa kuelewa story. Katika hali hiyo tunachofanya kwa kawaida ni kuongeza volume ili tuweze kusikia kinachosemwa. Lakini kumbuka kuwa unapoongeza volume lengo lako usikie mazungumzo ila hata mziki na sauti nyingine zitaongezeka pia. Kwa baadhi ya movie sio tatizo lakini kwa movie zingine unakuta mziki unafanya watu wasisikie vizuri kiasi kwamba hata ukiongeza volume bado husikii vizuri maneno wanayosema.

Dawa ni nini? S-force Front Surround inatatua tatizo hilo kwa kukusogezea mazungumzo. Yaani kwa mfano spika zipo futi 10 kutoka mahali ulipokaa Sony wanakufanya usikie mazungumzo kama vile wanaozungumza wapo futi 3 tu kutoka pale ulipo. Ili kurekebisha sauti ya mazungumzo, badala ya kutumia 'volume function' kuongeza /kupunguza sauti unatumia 'Voice Zoom Function' kwenye tv au audio system yako ili kuadjust mazungumzo hadi utakaporidhika .Yaani S-force Front Surround itaongeza sauti ya mazungumzo huku mziki na sauti zingine (ambient sounds) zikibaki chini.😳 Hiyo ndio kazi ya S-force Front Surround. Sasa tuone 👇

1.2 S-force Front Surround 3D
S-force Front Surround tuliyoongelea hapo juu inafanya kazi na 2D surround ikimaanisha kuwa sound signals zote ziko katika horizontal plane yaani mbele, kulia na kushoto, nyuma kulia na kushoto, mbele katikati na pia wakati mwingine katikati kulia na kushoto. Lakini sasa S-force Front Surround 3D inafanya kazi na 3D surround ambayo kwenye horizontal plane inaongezea height element yaani signals za kutoka juu ili kupata 3D surround.
Kabla hatujaongelea S-Force Surround 3D kwanza twende kwenye surround sound 3D technology. Dolby Laboratories ndio waasisi wa 3D surround kupitia teknolojia yao ya Dolby Atmos na Sony wanaonekana kupendelea technology za Dolby kwenye products zao. Dolby ndio kampuni pekee ambayo inatumia physical systems kwenye 3D surround yaani Dolby Atmos® to be specific. Wapinzani wao wakubwa Digital Theatre Systems (DTS) kwenye 3D wameenda moja kwa moja kwenye virtual surround kwa technology yao ya DTS:X®. Pia wapo wengine.

Dolby walipo upgrade kutoka 2D surround kwenda 3D surround hawakuongeza tu signals za kutoka juu bali pia wali transform kabisa teknolojia ya surround sound.

Kwenye 2D surround au tuseme dolby digital, kama tulivyoona hapo juu, wakati wa mixing signals zinapangwa kwenye channels 6 au 8 ambazo kila channels ina spika yake, of course, kama hiyo ni physical system yenye spika 6 au 8. Lakini Dolby atmos ina channels za msingiv(descrete channels) 10 yaani configuration ya 9.1 ambapo signal zinapangwa kama ilivyo kwenye dolby digital. Na kuna channels zingine 118 (matrixed channels) kwa ajili ya effects . Wakati wa production, sound mixing engineer anachofanya ni kuelekeza hizo effects kwenye nafasi (position) kwenye chumba na sio kwenye spika.

Tutoe mfano huu ili kuelewa. Tuseme unaangalia movie halafu upo barabarani gari linakuja kushoto kwako. Kwenye dolby digital au tuseme 2D surround bila shaka mgurumo wa gari utausikia kwenye spika ya kushoto. Lakini ukibadilisha spika ya kushoto ukaiweka kulia na ya kulia ukaiweka kushoto gari litatokea kushoto lakini mgurumo utatoka kulia. Hiyo movie bila shaka itakosa uhalisia na pia mvuto. Ndio maana spika za 2D surround system zinapaswa kupangwa kwa usahihi kabisa.

Lakini tukija kwenye dolby atmos system movie hiyo hiyo mgurumo wa gari utatoka kushoto muda wote hata ukiswitch spika😳 Bila shaka hii flexibility pia inarahisisha installation na set-up ya atmos system kwa sababu ukizingatia kuwa physical system inahitaji spika 64 kwenye ukumbi wa sinema na nusu ya idadi hiyo kwenye sebule yako, ni wazi installation ingeumiza sana kichwa kama kila spika ingepaswa kuwekwa exactly sehemu iliyokuwa programmed.
Pia zile channels 128 za dolby atmos zinampa mixing engineer uhuru mkubwa wa kupanga sauti upande wowote anaoona unafaa na umbali wowote kutoka kwa mtazamaji kulingana na nature ya hiyo sauti. Mfano sauti ya glass iliyodondoka sakafuni kutoka dining table atahakikisha inatokea chini. Kwa hiyo dolby atmos inafanya movie iwe halisi zaidi kuliko 2D surround.

Hata hivyo kama waswahili wasemavyo kuwa kizuri kinahitaji gharama. Mfumo wa atmos wenye spika 64 (ukumbi wa sinema) au spika 34 (nyumbani kwako) ni wa gharama kubwa sana. Lakini wamiliki wa kumbi za sinema wana sababu za kutosha kugharamia. Wanataka wateja wao wapate kile kilicho bora zaidi. isitoshe hiyo ni biashara hatimaye uwekezaji wao utarudi bila shaka. Hii ina maana kwenye ukumbi za sinema kwa sababu ya design na mpangilio wa ukumbi + 3D HD au 4K video+ high quality dolby atmos surround signals, hiyo immersive experience and realism utakayopata huwezi kupata nyumbani. Unaweza kusahau matatizo yako kwa muda😀. This is why bado watu wanaenda kwenye kumbi za sinema hata ingawa wana home sinema systems.

Hata hivyo kwa nyumbani mfumo huu wengi hatuwezi kuafford kiuchumi na pia huenda installation ya atmos system ikawa kikwazo kwa wengine kwa kuwa inahitaji makao ya kudumu. Ukiwa "mkimbizi"utashindwa kuenjoy 3D surround kwako maana huwezi kudrill dari la mtu ili kupachika spika za juu, utapewa notice ujue😂. Kuna taste pia maana watu wengine hawapendi system ya spika nyingi. Hivyo basi, ingawa virtualization inacompromise sound quality, ndio option ambayo wengi tunaweza kumudu. Lakini bado hata virtual 3D surround itakupeleka kwenye ulimwengu mwingine wa utazamaji wa filamu.

Ili kuimprove zaidi virtual 3D surround sound, Sony kupitia teknolojia yao ya S-Force Front Surround 3D, licha ya kupanua sound field na kukusogezea mazungumzo (dialogue) kama tulivyoona huko nyuma, pia wanakuhakikishia kupata full 3D surround sound spectrum ya Dolby Atmos® au kama wengine wanavyoita 360° surround. Hii ina maana S-force Front Surround 3D inadecode Dolby atmos codec kazi ambayo kwa kawaida inafanywa na Atmos Height Virtualization technology (au DTS virtual:X kama ni DTS:X codec) Sasa tuone👇

2. Sound Pressure Horn
Kama jina linavyoonyesha hii ni kama honi ya gari ambayo ipo kama tarumbeta. Tunajua kuwa vifaa vya muziki vinavyotoa sauti kwa upepo kama tarumbeta au saxaphone havitumii umeme.Tulinganishe na kitu ambacho wengi wanakijua: vuvuzela pia inatoa sauti bila umeme.
Tarumbeta au saxaphone inapopulizwa, mouthpiece ina pick vibrations za mdomo kisha acoustic signal ina resonate ndani ya horn. Kadri diameter ya horn inavyoongezeka, amplitude inaongezeka. Matokeo:upande huu vibrations za mdomo, upande mwingine sauti yenye uwezo wa kuharibu ngoma ya sikio!. Yote hayo bila umeme kutumika 🤫.

Sony wame utilize hii technique kutengeneza Sound Pressure Horn. Lengo ni kureplace subwoofer. But why? 🤔 Cost and Convenience.
Of course, gharama za kutengeneza Sound Pressure Horn ni ndogo sana ukilinganisha na gharama za kutengeneza subwoofer. Pia subwoofer zinahitaji dedicated amplifier ili zifanye kazi na hii inamaanisha umeme kwa hiyo matumizi ya umeme yanaongezeka ukitumia subwoofer

lakini, kama tulivyoeleza hapo juu, Sound Pressure Horn haihitaji umeme.
Jambo lingine subwoofer ni component inayoongezeka kwenye sound system inahitaji nafasi pia. Lakini Sound Pressure Horn inapachikwa ndani ya cabinets za spika. Watu wengine wanataka system ambayo ni simple lakini huku ikitimiza mahitaji yote. Hawataki maspika mengi mengi kwenye sitting room. Lakini unakuta hifi systems ya Sony ina components 3 tu yaani A/V receiver + 2 speaker cabinets kila cabinet ikiwa na tweeter kwa ajili ya high frequencies, woofer kwa ajili ya mid and low frequencies na Sound Pressure Horn kwa ajili ya sub low frequencies. Unapata kila unachohitaji from just a simple-looking machine.

Teknolojia ya S-Force Front Surround inapatikana kwenye TV, Soundbars, Hi fi systems na CD/DVD receivers za Sony. TV zenye hii teknolojia bila shaka lazima ziwe na subwoofer kwa sababu spika zake, kama zile za soundbars, haziwezi kuhandle sawa sawa low na hasa sub low frequencies kwa hiyo subwoofer back-up ni muhimu sana. Sony hawasemi kama tv hizo zitakuja na subwoofer au la. Ila specifications zinaonyesha sehemu ya kuconnect subwoofer lakini labda inanunuliwa tofauti na tv ingawa Sony hawasemi lolote (mfano Sony KD-65AG8). Kwa hiyo ukinunua tv yenye S-Force Front Surround technology ujue umenunua complete home theatre system.

Sound Pressure Horn inapatikana kwenye Sony hi fi systems ambazo pia zinakuwa na S-Force Front Surround technology hasa SHAKE series mfano Sony shake X30D. Mwisho 👇

3.LDAC Bluetooth streaming technology:
Kwa kumalizia Sony pia wamedevelop teknolojia ya LDAC kwa ajili ya kuboresha bluetooth streaming kutoka kwenye simu, kompyuta, nk. Hii technology inafanya data transmission rate (bit rates/sec) iongezeke hadi mara 3 ukilinganisha na bluetooth streaming ya kawaida.

Kwa hiyo audio file linakuja katika quality ya juu zaidi. Lakini Sony hawaelezi kwa undani jinsi hii teknolojia inavyofanya kazi. Hata hivyo bila shaka hilo si muhimu sana.🙏
 
Inabid uanze kutoa tutorial YouTube kk man sio wote hatun pesa ya kununuwa mziki mzur tatz elim
 
Hii radio ina nn wakuu mbona bei yake ya juu sana
Screenshot_2023-08-08-22-33-59-115_com.instagram.android.jpg
 
Andika Vizuri
Weka Parandesi, Koma, Nukta, Aya Baada Ya....



Uandishi Mchafu Unaoondoa Hamu Kwa Msomaji Yoyote
Fanya Masahihisho Kwenye Bandiko Lako Haraka
Shida amekopi kitu ambacho nchini mwake hakipatikani, hatuna studio za kutengeneza hayo wala transimita za kurusha hayo.
 
Back
Top Bottom