Somo Kubwa wanaume tumepewa kutoka kwa Erik Spoelstra

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,090
Nilipokuwa ndo ninaanza kubalehe marehemu Babu aliwahi kuniambia “Ukitaka kuwa na Maisha mazuri na yenye furaha kama mwanaume basi usije kuoa! Mwanamke anakondesha Mjukuu! Mwanamke sio ndugu yako kabsa! Kaa nao mbali!" Sikuelewa hata kidogo ila nilipotimiza miaka kadhaa mbeleni nikaanza kumuelewa babu.
1704965489259.jpeg
Baada ya kuona yaliyotokea kwa Mwamba Hakimi nilidhani kuwa wanaume wenye kuchezwa na machale wapo wachache kumbe kuna miamba imetulia inatunga sharia kama kobe tu, ingawa kisa na mkasa uliomhusu Hakimi na aliyekuwa Mke wake kushangaza watu ulimwenguni ila kuna mwamba sasa hivi ndo ana-trend sana kwa kile ambacho amekifanya mara baada ya kutalikiana na mke wake. Talaka nyingi zimepata kutokea kwa watu maarufu kama vile, Reese Witherspoon na Jim Toth, Pamela Anderson na Jon Peters ila mpaka sasa watu wawili wametuonesha akili kubwa sana katika kutazama mbele ya muda.​
1704965505926.jpeg
Talaka ya hivi majuzi ya kocha mkuu wa Miami Heat, Bwana Erik Spoelstra kutoka kwa mkewe, Nikki Spoelstra, imeteka hisia za mashabiki wa mpira wa vikapu na vyombo vya habari vingi duniani. Kama ilivyo kwa talaka yoyote ya watu mashuhuri wa hali ya juu na wenye ushawishi, kuna masomo ambayo yanaweza kujifunza kutokana na hali hii ya kusikitisha. Ingawa talaka kamwe sio matokeo bora, ni fursa ya kutafakari na kukua zaidi kimahusiano kwa watu wote wawili. Katika andiko hili, tutachunguza baadhi ya masomo muhimu ambayo wanaume wanaweza kuchukua kutokana na talaka ya Erik Spoelstra.​
1704965528606.jpeg
Kwanza kabisa, mawasiliano ni muhimu. Ukosefu wa mawasiliano ya wazi na ya uaminifu inaweza kusababisha kutoelewana na chuki, ambayo inaweza hatimaye kuharibu uhusiano. Ni muhimu kwa wanaume kueleza hisia zao, wasiwasi na mahitaji yao kwa wenzi wao. Kwa kusitawisha mawasiliano yenye matokeo, wenzi wa ndoa wanaweza kuepuka migogoro isiyo ya lazima na kushughulikia masuala kabla ya kuwa vikwazo visivyoweza kushindwa.​
1704965547852.jpeg
Pili, mafanikio yanaweza kuja kwa gharama. Mafanikio ya ukocha ya Erik Spoelstra na kuongezewa kwake mkataba mpya wa dola milioni 120 bila shaka ulileta mafanikio ya kifedha na kuongezeka kwa majukumu ingawa Bi Nikki hagusi hata mia kwenye pesa hizo. Hata hivyo, ni muhimu kwa wanaume kukumbuka kwamba kujitolea kupita kiasi kwa kazi ya mtu kunaweza kuharibu uhusiano wa kibinafsi. Nikki amelipuka mtandaoni na kuanza kuonesha kuumia sana baada ya kusaini mkataba huo baada ya kumalizana na talaka, yaani alikuwa akitaka Erik kusaini mapema ili apate mgawo wake ila ya Mungu mengi bhana.​
1704965563061.jpeg
Tatu na mwisho ni kutumia fikra zaidi kuliko hisia katika kitu chochote unachokifanya kama mwanaume! Usiruhusu hisia zikuendeshe hata siku moja. Taarifa za kuongezewa mpunga wa dola milioni 120 zilitoka tu baada ya kutoka kwa talaka! Umeona mahesabu hayo! Yaani huo mpunga umemfanya mpaka bi mdada atoe povu kwa kuona amepishana na gari la mshahara. Mwanaume kuwa makini sana endapo ukipata mwanamke ambaye hujapambana naye kimaisha, tazama kwa umakini mtiririko wa pesa na mali zako. Erik alitulia na kuenda na mwendokasi wa Nikki kudai talaka ili baadaye atie saini mktaba wake na avute mpunga.​
1704965620630.jpeg
Sasa wanaume tumepata role models wawili wakubwa ambao wametuonesha misingi na namna ya kuishi na wanawake kwa utimamu mkubwa wa akili. Pale Ashraf Hakim hapa bwana Mkubwa Erik Spoelstra, mmeupiga mwingi sana wanaume!​
1704966163531.jpeg
Ubarikiwe sana kwa funzo hilo Mkuu!
 
Ykishakuwa na hela tu ni mtihani, ngumu kujua yupi real yupi fake, hapo lazima akili ifanye kazi VERE WELE yani.
 
Mbona kuna ndoa nyingi zilizo fanikiwa jizzy na beyonce?

Messi na Antoniela?


ni bahati ya kuwa na mpenz mnae endana

kwaio wew unasema ukitaka kuwa tajir kata ndoa hio ni fikra mbovu Sadio mane jana ameoa mwanamke aliekua akimsomesha

kila siku watu wanaoana tatizo kubwa ni pale mnapo tafuta wapenz insta mkaoe
 
Back
Top Bottom