Soma changamoto zangu, utajifunza kitu.

MTOTO KITAA

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
245
115
Wakuu habar! leo naomba nizungumze changamoto zangu na mpaka mafanikio ya hapa nilipofika, walengwa wakubwa ni ndugu zangu mwaka wa kwanza.lengo si kuwatisha, bali huwenda ukajifunza kitu.wazazi wangu kiujumla ni kundi la watu masikini,kitado cha kwanza mpaka cha nne, nilisoma kwa shida sana, ikifika kipindi cha kufukuzwa ada mi nilikuwa mmoja wapo, kwa mwaka mzima darasani nilikuwa nasoma miezi hata miez minne haifiki, sio kwamba sipend kukb darasani, bali ni kukosa ada huku nikifukuzwa darasani, nikajikaza mpaka nikamaliza kidato cha nne kwa mbinde sana, mungu akanijalia nikapata daraja la tatu, nilikosa point moja tu, niwe nimepata daraja la la pili, baati mbaya nilikosa kuchaguliwa kidato cha tano. nikapagawa sana,maana nilijua ndoto yangu imepotea, nilihuzunika sana! mama yangu alinifuata na kuniambia nitakupeleka kusoma advance huko tanga, ila kwa sababu sina pesa nitakopa kwa marafik zake, ada ya hiyo shule inaitwa ARAFA watu wanaotokea tanga wanaifahamu, ada yake ilikuwa rahisi sana, inaendelea....
 
nilipata shida sana kuvaa yale mavaz ya unifomu za hapo shuleni, kwa kuwa nilikuwa na lengo moja tu la kufika chuo kikuu, nikajikaza nikasoma kwa bidii mpaka nikamaliza advance kwa mbinde huku nikidaiwa ada,nilifaulu na kupata kupata daraja la pili, nikashukuru mungu sana. mda w kuomba chuo ukafika na ndio kipind cha kuanzishwa mfumo wa TCU,mama yangu alishauri nikasomee uwalimu, alimaanisha nisiende chuo, ila nikasome diploma ya uwalimu, baba alipata ushauri kutoka kwa ndugu kuwa niende chui kikuu, kwa kuwa mama hakuwa na sauti mbele ya baba na ukoo, akakubali yaishe na hapo ndugu upande wa baba walisema watanichangia nauri ya kwenda chuo na wakati huo nikisubiria pesa ya bodi ya mkopo. safari ikaiva, nilichaguliwa chuo cha SAUT Mwanza, kweli ndugu walijichanga ikafika laki moja na nusu, nikafunga safari hadi mwanza, kumbuka simjui mtu, sina ndugu wala rafiki.kutoka dar hadi mwanza unafika usiku wa saa tano au sita, inategemea na aina ya gari unalopanda, nikafika saa sita kasoro,inaendelea......
 
kumbuka nauri ya dar to mwanza ni 45000,so nilituia 50000, nikabakiwa na laki moja, basi ikabidi nilale stend ya mabasi, nyegezi, baridi langu, mbu rafiki zangu. asubuh ikafika, napishana na wototo wa vigogo wanaletwa na magari yao, mie nipo na kibeg changu mpaka chuo, nikafika mapokez nikata jina langu na kweli nilipangiwa hapo, koz niliyopangiwa ni public relation and mkt, sio education. nikauliza utaratibu nikaambiwa natakiwa nilipe ada 30% na registratio fee, hata kama umepata au haujapata mkopo. jumla natakiwa nilipe kama laki tano. mungu wangu nitaipata wapi, kumbuka ndugu walijichanga nikapata laki na nusu. na naambiwa haupew hostel mpaka umalize hicho kiasi, hapo ndipo nilipo changanyikiwa,nitalala wapi? wazaz wameishiwa! ndugu hawana kitu! masomo yameanza! chuo nimeomba mpaka nimeenda kwa VC, sikufanikiwa, nani wa kuniokoa??? nikamuomba mwana mmoja, nilale naye kwenye kitanda chake, kama nnavyojua vitanda vya hostel, ni futi mbili. nilikaa siku mbili siend class, maan akiri inajiuliza nitalala wapi,
 
hari ikawa ngumu sana, nilikuwa nakaa histel ya mikumi, kwa wale ambao wapo chuo cha saut wanaifahamu, mungu akasaidia baada ya wiki moja, kulikuwa na jamaa mmoja akahamishwa chuo na kupelekwa saut ya tabora, so kitanda kikawa waz, mim nikalala pale kama wiki mbili tu, mara majina ya bodi y mikopo yakatoka, nikawa nimepata 30% yaani 70% nijilipie. kumbuka bado sijafanya registration kama laki tano nadaiwa, wenzangu anafurahia boom, mimi nikawa nalia, tena nalia machozi, nikasema, niache tu chuo nirudi mtaani,lakini nafsi ikakataa na kunikumbusha kuwa wewe ni mtoto wa kiume, kumbuka kutoka kidato cha kwanza hadi hapa ulipofika, mwenyezimungu mkubwa bodi wakatuma pesa kama lakisaba na kitu, nikashukuru mungu, nikatoa laki tano na nusu, nikafanya registration. na nikapigwa penat juu, pia nikapewa rasmi kile kitanda alichoacha yule jamaa, mfukoni nikwa na laki mbili hivi. kidogo maisha yakaanza kuwa nafuu, nikaanza kuingia darasani,kununua vifaa na mbndaliz ,nikawa nimetumia kama 50000, inaendelea....
 
sasa naingia darasani, mfukoni nina laki na nusu, natakiwa nijibane mpaka miez mitatu itimie, ndio boom lingine nipewe, je kwa pesa hiyo nitafika?? kila lecture akiingia class anaacha notes zake zikatolewe copy, maisha yakawa ndio hivyo, ikabidi nijibane kwa kutokula mchana nikawa nakula usiku na asubuh nakunywa chai tupu, au kama nikila wali mchana, basi usiku nakula miogo na chai.miasha yakasonga nikawa nakopa kwa wana, na hata wengine walinipa kampani tu.mungu mkubwa nilikaja boom,lingine ndio maisha yakawa nafuu,hatimaye nikajibanabana,sivai pamba za ukweli, mpaka namaliza chuo sijawahi kwenda club,na wala sinywi bia, starehe zote hizo, sio kwamba sizipend, ila hari ya maisha tu, kuhusu mademu, niliwaogopa sana watoto wa chuo, kwa maana niliogopa gharama zao, nilipata mpenzi wa sec ndio akawa ananiliwaza. nimeamua kufupisha maana mtachoka kusoma. Sasa maisha bàada ya kumaliza chuo, huku mtaani......inaendele.a.......
 
baada ya kumaliza chuo, mtaani nimekaa kama mwaka hivi, siku moja nilikuwa maeneo ya uwanja wa taifa, kwa upande wa pili kuna stend ya mabasi ya kwenda ubungo, nikamuona dada mmoja hivi akishuka kwenye gari yake, na kwenda upande wa pili, alivaa unifom a benk moja hivi, ni superbrand. mawazo yakanijia kuwa nimfate yule dada nikamueleze shida yangu, huenda mungu akaweka shani yake,wakati anarud kwenye gari yake, nikamsimamisha,nikamwambia dada samahani mi naitw...... ni mtu mwema naomba ondoa shaka, mim ninashida, na kama ipo ndani ya uwezo wako naomba unisaidie au hata kunipa ushauri nitashukuru pia. basi nikamweleza shida yangu ni ajira mbna nimechoka kuzunguka kuomba. akanisikiliza na pia akania sawa nimekuelewa, pale ofisin zikitoka nitakujulisha, nipe tu namba yako ya simu, na pia akaniuliza nilichosomea, kisha akaondoka. nimekaa kama wiki hivi, yule dada akanipigia simu na kuniambia njoo ofisini uniketee cv yako, huwezi amini nilifurah sana kama vile nimepata kaz, maan sikuamini kama angetilia maanan...
 
nikaenda ofisini kwake, nilimchukulia poa, kumbe meneja fulani hapo benk, akaniambia asante kwa kuniletea, na akanipa na naur ya kurudia. nimekaa kama wiki mbili tu akanipigia simu na kuniambia andika barua ya post ya .... kisha peleka vyeti vyako kwa mwanasheria, kisha njoo navyo hapa ofisini, nikampelekea, akaniabia asante tutawasiliana,mungu si mrisho mpoto, siku akanipgia simu akaniambia dogo, kaa stend bay mda wowte wiki inayokuja utapigiwa simu ya kwenda interview, pitia benk chukuwa vipeperushi anza kusoma product zetu, nikafanya kama nilivyoambiwa, ile wiki ikapita sikupigiwa simu, nikamuendea hewani, nikamueleza na akasema, vuta subira baada ya siku yatu, kama hwajaupigia niabie, niavuta subira, simu naenda nayo hadi chooni,kweli bwana siku ya pili yake nikapigiwa simu, nikaambiwa naitajika..... kwa usaili,saa tatu asubuhi, nikafika nikafanya usahili, nikapata nafasi kwenye hiyo taasis. mungu ni mwema, na ni kwa neema tu. natumaini umejifunza kitu hapo. mod naomba unionganishie uzi. asante
 
vijana wa sasa. bei ya msosi wanauliza jamii forum. kozi znafundishwaje wanauliza jamii forum. pa kulala wanauliza jf. hadi wasupa (wadada) wanauliza jf. ada wanauliza jf.
 
Back
Top Bottom