Social media na ndoa yangu

Ndio mke wako huyo komaa nae
shida ni kuwahi kufa, kukomaa sio shida. Moyo hauwezi kuhimili mambo magumu kwa muda mrefu. Ndio maana hata Eliya aliomba Mungu amchukue mapema ili kupunguza tabu ya ulimwenguni hapa. Sasa mzee nikiwahi kufa hata hao watoto wa kulea hatakuwepo. Ni bora nilinde nafsi ili niapate hata muda wa kulea hao watoto. Otherwise, najiona kama my life has reached its end. Haya mambo mara nyingi yanageuka kua option kati ya kuishi na kifo. Baadhi ya wanawake wakiwa insecured sana wanaoption ya kuua wanaume. Angalia yule trafiki eti mapak mkewe ni mshukiwa wa mauaji.
 
N

Nafikiri anza na plan A kwanza mnyang'anye hiyo simu mnunulie hizi za kawaida swala lakuachana iwe ni option ya mwisho baada ya hili kushindikana.

Kumnyanganya naweza sana shida ya hawa wanawake wa siku hizi kwanza wanafanya kazi hivyo wanamishahara. Pia, wanasaccos ambayo inampa jeuri sana. Maana anaenda tu anachukua hela huko na anafanya mambo yake. So uwezo wa kununua anao nyingine anao sana. Mimi nlimuoa wakati hana kazi na hata saccos hazijui. Siku hizi kwenye saccos huko wanadanganyana sana hata ndoa inakua haina maana kabisa. Hata hela hakuzoea kushika alikua mpole balaa, siku hizi duh, hapa kazi tuuu. Ndo maana nimefikiria option ya divorce, maana hata ulimbukeni wa kushika hela nao unasumbua. Maana anafikiria maisha ni kitu rahisi sana kitu ambacho sio kweli, wakati hata kumanage mshahara wake tu kwa matumizi yake binafsi hawezi.
 
Wewe ulishaamua kumuacha...tafakari tena zile ahadi za ndoa!!!
 
Wakati namuoa hata hakuwepo kwenye social networks kabisa, enzi hizo alikua na simu mchina ya tochi.
Yaani wewe story ya mkeo kama yangu na mke wangu, lakini mimi nimeamua kumsamehe na kumuacha aendelee na upuuzi wake na ulimbukeni wake japo mara chache akijaribu kunihusisha na huo umaku wa social media namuwashia moto mzito.

Wafikirie wanao zaidi, halafu jaribu kulegeza moyo wako huku ukijikita kujikwamua kiuchumi usishindane naye..... Let her be
 
Kumnyanganya naweza sana shida ya hawa wanawake wa siku hizi kwanza wanafanya kazi hivyo wanamishahara. Pia, wanasaccos ambayo inampa jeuri sana. Maana anaenda tu anachukua hela huko na anafanya mambo yake. So uwezo wa kununua anao nyingine anao sana. Mimi nlimuoa wakati hana kazi na hata saccos hazijui. Siku hizi kwenye saccos huko wanadanganyana sana hata ndoa inakua haina maana kabisa. Hata hela hakuzoea kushika alikua mpole balaa, siku hizi duh, hapa kazi tuuu. Ndo maana nimefikiria option ya divorce, maana hata ulimbukeni wa kushika hela nao unasumbua. Maana anafikiria maisha ni kitu rahisi sana kitu ambacho sio kweli, wakati hata kumanage mshahara wake tu kwa matumizi yake binafsi hawezi.
Hizi ndo shida za kuoa mke akiwa hana kipato hujui tabia yake ipoje akiwa nacho,
Anyway mi labda sielewi au kuna ya nyuma ya pazia huyasemi,yani unaacha mke kisa tabia yake mitandao ya kijamii tu au??
I wish tungemsikia mkeo ana Yapi yakusema kuhusu wewe
 
shida ni kuwahi kufa, kukomaa sio shida. Moyo hauwezi kuhimili mambo magumu kwa muda mrefu. Ndio maana hata Eliya aliomba Mungu amchukue mapema ili kupunguza tabu ya ulimwenguni hapa. Sasa mzee nikiwahi kufa hata hao watoto wa kulea hatakuwepo. Ni bora nilinde nafsi ili niapate hata muda wa kulea hao watoto. Otherwise, najiona kama my life has reached its end. Haya mambo mara nyingi yanageuka kua option kati ya kuishi na kifo. Baadhi ya wanawake wakiwa insecured sana wanaoption ya kuua wanaume. Angalia yule trafiki eti mapak mkewe ni mshukiwa wa mauaji.
Is social media this serious hadi tunaongelea kifo,jmn I think this is exaggerated..
 
Pamoja na yote hayo inaonekana wewe ni Perfectionist type na unachukulia kila kitu serious...anyways sijui lakini dont take everything serious coz you will be very stressfull!!! its just an opinion though
 
Hakuna cha kuwashirikisha wazazi wala washauri mkuu. Yeye sio mtoto ni mtu mzima. Usipoteze muda zaidi maisha hayakusubiri. Oportunities hazisubiri Mkuu. Songa mbele na maisha. Tafuta muda ongea nae kwa kirefu uchafu wake wote na hatua unazotegemea kuchukua iwapo hatabadirika. Then mwambie wazi kuwa unampa wiki au mwezi asipobadilika unampiga chini. Maisha magumu hivi halafu watu wanaendekeza kupoteza muda. We mwanaume maliza hilo jambo usipoteze muda zaidi
 
Picha haijalishi kama za aibu ama ni za aina gani. Kikubwa na kumsikiliza upande wa pili kama yeye binafsi hataki basi ni la kuheshimu hilo........

Hivi unadhani mapenzi yanaisha kwa vitu vikubwa? Haya mambo madogo madogo ndiyo yanayomaliza mapenzi.......
Trust me you are one in a few women. Hongera sana sister kwa kujitambua. Wewe ni dhahabu. Baadhi ya wanaume wanabahati.

Wengine hawajui kuwa mapenzi sio vita au mashindano...sio mkubwa nani na mdogo nani. Mapenzi ni kusikilizana, kuheshimiana, kupendana na kujaliana etc etc. It is a win-win situation.
 
Ndugu yangu PIMs pole. Kiukweli tabia ya mkeo sio nzuri kwa tafsiri yoyote ile. Just for the mere fact kwamba mlishazungumza kama familia kuhusu vitu vipi mfanye na vipi msifanye kwa faida ya familia yenu.

Hata hivyo kabla hujavunja ndoa nashauri uongee naye tena. Safari hii mpe hint ya uamuzi unaoweza kuchukua endapo hatabadilika. Muonyeshe kwamba uko serious. Then fuatilia utekelezaji.
 
Navyowajua mwanamke hadi kufikia hatua hiyo, kuna mahali tu mwanaume ulikosea. Hawaanzagi kubadiliika from no where... Sie wanaume wengi wetu hatutimizi ile leading role, we tend to be too participatory matokeo yake ndo haya unamwambia hiki sitaki na yeye anakujibu nitafanya tu si mimi nakipenda. Tunalea wenyewe huu upuuzi halafu baadae tunalalamika tena.

Kifupi wanaume wengi tunashindwa kuwa-manage wake zetu, tumebaki kukimbilia tu kutoa talaka ilihali tunatesa watoto bure
 
Pole sana rafiki kwa changamoto hiyo kubwa, nasema kubwa kwakua najua mpaka unakuja hapa ushavumilia vya kutosha. Ila napenda kukushauri huu ndo muda wa kumtafuta Mungu kuliko kipindi chote ulichowahi kumtafuta, ndoa ilianzishwa na Mungu mwenyewe pale edeni na hivyo hitimisho la ndoa Mungu pekee ndiye huweza kutoa jibu. Imani ya mtu binafsi kwa Mungu ina nguvu sana. Mambo ya ndoa yakutatuliwa na wanandoa wenyewe huleta maana zaidi kuliko kuwashirikisha wengine kwakua shida yenu mnaijua wenyewe na hakuna atakayeijua kwa undani na kiukweli isipokuwa nyie wahusika.

Chakufanya:
1. Ongea na mkeo akwambie tatizo ni nini, mruhusu atoe madukuduku yake yote juu yako, usimzuie hata kidogo maana akisema ndo ndoa inapona hivyo, kisha toa mtazamo wako juu ya hayo aliyokueleza bila kumtukana wala kumkejeli au kuonyesha dharau kisha amueni kwa pamoja muondoke na msimamo upi kwa mustakabali wa familiya.

2. Ndoa ni ya wote hivyo mnapoingia kwenye ndoa lazima kila mmoja awe mtumishi wa mwenzake na ili kufanikiwa katika hili lazima kila mmoja awe tayari kupoteza baadhi ya vitu fulanifulani kwa ajili ya mwenzake na familia kwa ujumla ili mambo yaende sawa.

3. Usipuuze kitu anachokipenda mwenza wako kwa kudhani ni cha kipuuzi ila chako unakiona cha maana kamwe hamtoelewana ndo maana yawezekana akawa anakufanyia usichopenda kwa makusudi ili uumie kama anavyoumia yeye.

4. Kuomba ushauri kwa mtaalamu wa ushauri ni sawa na kumpatia akulelee mkeo kitu ambacho ni hatari, ukimpeleka kwa viongozi wa dini nao wakati mwingine sio waaminifu kwa hukutumia wewe kama kisa wawapo madhabahuni, ukiwaambia wazazi ni kutengeneza chuki hata ikitokea mmeyamaliza hamtakuwa na taswira nzuri mbele ya macho yao.

5. Ikishindikana kabisa mtalakiane, ila tahadhari katika hili ni kwamba mambo yenu ya siri yatawekwa hadharani maana kila mmoja anatakiwa aweke ukweli wote ili mahakama ijiridhishe lakini pia habari itachapishwa kwenye gazeti ambapo kila mtu atasoma kuanzia ndugu zenu, jamaa, marafiki, watoto na wanajamii. Kisha mtagawana mali zenu pasu kwa pasu. Kama upo tayari kukabili aibu hii jiandae kutoa talaka.

Hitimisho:
Mungu yupo na anatenda hakika kwa kila amwaminie, mtangulize Mungu kwa kuomba na ikiwezekana funga kwa ajili ya ndoa yako utaona mabadiliko ambayo hutoamini na kamwe hutosahau ambacho Mungu atakutendea. Mungu akutie nguvu na aiponye ndoa yako iwe yenye furaha na amni.
 
Trust me you are one in a few women. Hongera sana sister kwa kujitambua. Wewe ni dhahabu. Baadhi ya wanaume wanabahati.

Wengine hawajui kuwa mapenzi sio vita au mashindano...sio mkubwa nani na mdogo nani. Mapenzi ni kusikilizana, kuheshimiana, kupendana na kujaliana etc etc. It is a win-win situation.
asante mkuu................
 
Tv na mitandao imewaharibu dada zetu hataree. Ukiona mkeo amebadilika kitabia ujuwe kuna kishetani mtu ndicho kinacho mbadilisha. Marafiki wengine wana tabia za kibinaadamu lakini wengine wana tabia za kishetani. Mimi na Jf tu hio mitandao mengine nayasikia tu.

Mmmmh vitu vingine mnamsingizia shetani bure,,, mtu ni mzima tu na akili yake lakini anafanya kitu kwa maksudi mkuu
 
Back
Top Bottom