SMZ yazidi kuubomoa Muungano yataka bara walipe kodi ya ardhi

Mwiba,
Mie na-support kabisa Zanzibar kujimegua na kufanya mambo yake. Kufuata Tanzania Bara ni kupoteza muda kwa sababu Tanzania bara kuna matatizo mengi na sugu ambayo hawana muda wowote wa kufikiria matatizo ya Zanzibar. Tanzania is too big for the Tanzania president; better leave Zanzibar total autonomy to the Zanzibar President. That will be the best for both Tanganyika and Zanzibar.

And that is the pwoint ,msitutishe na kuzama wacha tuzame kwani sisi tutakuwa sio wa kwanza ,lakini kutuzalilisha hilo halikubaliki.
 
better leave Zanzibar total autonomy to the Zanzibar President. That will be the best for both Tanganyika and Zanzibar.
That will be the best for both Tanzania (siyoTanganyika) and Zanzibar. Na hivi ndivyo Muungano kama tunazungumzia ule wa 1964 ulivyotaka iwe. Isipokuwa kuna mambo (machache) yameainishwa kuwa yatakuwa katika milki ya Jamhuri ya Muungano (Rais wa Jamhuri ya Muungano.) Sasa nani katufikisha hapa tulipo sijui. Hivyo, wanaodai hiyo autonomy nafikiri wanataka turudi katika azma yetu ya awali na siyo kuelekea katika mawazo ya ndotoni.
 
That will be the best for both Tanzania (siyoTanganyika) and Zanzibar. Na hivi ndivyo Muungano kama tunazungumzia ule wa 1964 ulivyotaka iwe. Isipokuwa kuna mambo (machache) yameainishwa kuwa yatakuwa katika milki ya Jamhuri ya Muungano (Rais wa Jamhuri ya Muungano.) Sasa nani katufikisha hapa tulipo sijui. Hivyo, wanaodai hiyo autonomy nafikiri wanataka turudi katika azma yetu ya awali na siyo kuelekea katika mawazo ya ndotoni.
vile vile WaTanzania Bara huwa hatuelezi vizuri kwa nini hatukubaliani na kwa Wazanzibar kuwa na total Autonomy; sisi hufikiria tu kuwa ati ni kujitenga. There are issues to compromise, hawa watu wamekuwa chini ya muungano since 1964 na hamna mafanikio waliyoyapata ila ni kudidimia tu. Better to have a referundum; labda Tanzania ikubali on only one issue; on Muungano on defence with a Senior General for Zanzibar who have to be under a comand of the Chief Of the Defence of URT. Other issues give them autonomy what to practice including those policies which influence social political and economic development. Sometimes we have to agree, the smaller the better and easier to organize.
 
Hapana, ni sahihi kabisa kwani wanatutafuta wabara bila sababu. Waende wakagombane wao kwa wao nyumbani kwao, wakishapatana warudi tuungane. Wakiridhia huko visiwani, wawelezaji wa kipemba nao walipe $5,000 kwa kila hekari ya ardhi Tanzania Bara

Sasa wapemba walipe $5000 kwa kila hekari ya ardhi Tanzania Bara kutumia sheria ya nchi gani? Tanzania Bara au JMT?, tangu lini umesikia kuna nchi inaitwa Tanzania Bara, hapa tunarudi pale pale - Serikali ya Tanganyika irudishwe na iyashughulikie masuala kama haya, sasa ugumu uko wapi jamani?, au munawataka kuwafanyia wazenji "change bin change"? - weshashituka wapemba wamekaza makalio sasa.
 
Suluhisho la kumaliza dhulma hii ni:

1. Kuanzisha Serikali ya Tanganyika. Tunaona hii ya muungano haina meno kabisa dhidi ya Sheria kandamizi dhidi ya Watanganyika.

2. Kuvunja Serikali ya Zanzibar na kubaki na Serikali moja. wazenji hasa viopngozi wataipinga kuogopa kupoteza ulaji.

3. Kuvunja huu Muungano kabisa, ili wazanzibari wanaoishi huku Tanganyika wajulikane kama foreigners ili waombe vibali vya kuishi nchi jirani ya Tanganyika, watakaokubaliwa wavilipie, watakashindwa warudi kwao Zanzibar. Pia washindwe kumiliki ardhi etc. HII NDIYO BEST OPTION, kwanini tunawabembeleza hawa?

Kufuatia udhaifu wa kiuongozi na kimaamuzi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM kwenye kikao cha NEC Butiama, ilishaonekana kuwa wazanzibari wanajua udhaifu wake. Na watamyumbisha sana tu.


Ole wenu mnaotawaliwa na kiongozi dhaifu!

Wewe, munabembeleza kwa sababu munajua munaweza kufaidika baadae na rasilimali zilizopo offshore Zanzibar hivyo lengo ni kuibembeleza Zanzibar na kuivunja nguvu kidogo kidogo mpaka ikubali kuwa mkoa, sasa angalia uhamiaji wa watanganyika kwenda Zanzibar - is it just a coincidence au ndio mbinu za kuongeza idadi ya wazanzibara ambao huko mbele watakuja kusaidia kupunguza kasi ya hisia za kizanzibari?, siwezi kuiita hii mbinu ethnic cleansing lakini naweza kusema ni ethnic neutralization, wapemba waliopo Buguruni hawafikii hata 1% ya wadanganyika wakati wazanzibara waliohamia zanzibar baada ya kuondolewa hati za kusafiri wanaweza kufikia hata 10% ya wazanzibari, tembea zanzibar na utashangaa, wamejazana kweli kila unakopita unaisikia accent ya kibara utadhani upo Manzese, halafu wengine sasa wamekuwa na kiburi cha hata kuwabughudhi wazawa asilia, angalieni hapa tunaweza kuja kuwa na Rwanda nyengine Zanzibar kati ya wazanzibari na wazanzibara.
 
Hakuna cha jazba, ndugu yangu.

Hii sheria mpya tunayoijadili ( na si historia) haitofautishi kiwango anacholipa asie raia wa Tanzania ( Mfilipino na wengine) na mtanzania bara. Wote wanatakiwa kulipa dola 5000 kwa mwaka kwa hekta. Sasa utasemaje kuwa hauwatengi kama wewe mwenyewe umewaweka kundi moja na hao wageni? Talk is cheap. Hatuwezi kuuenzi Muungano kwa maneno tu wakati tunafanya vingine kwa matendo!

Tangu lini mshirazi amekuwa ana asili ya Zanzibar kuliko mtanzania bara? Kwani wakina Seyyid Said walipokuja hawakukuta watu? Na hao watu walitokea wapi? Na nauliza hivi, si kwa jazba, bali kutaka kuelewa. Maana naona inaelekea huo uzanzibari ni haki ya washirazi na wengine ( wenye asili ya bara, ungazija n.k.) wanafanyiwa feva tu!

Unasemaje watanzania bara watamiliki ardhi wakati unawawekea viwango ambavyo ni usury!
Au unataka wakae huko kitwana maana kazi zote za maana mmeishasema wapewe upendeleo wazanzibari. Na huko tena watanzania bara wamewekwa kundi moja na wasio watanzania.

Hapana, Mkuu. Ni vitendo vyenu vinavyotuambia kuwa huu Muungano ni gelesha tu. Unathaminiwa mnapofaidika lakini mnapoweza mnautumia kuwakomoa watanzania bara!

Amandla....

Kasome historia na utajua asili ya wazanzibari. Kila mtu pale visiwani ni muhamiaji na kutokana na uhamiaji huu ndio Uzanzibari umekuja, asilimia kubwa ya Wazanzibari wala hawajui asili yao imetokea wapi, umetokea mchanganyiko mkubwa tu na huu ndio uzanzibari, kama una rafiki yako mzanzibari hebu muulize yeye kabila gani? asilimia kubwa ya wazanzibari halisi hawajui haya mambo ya makabila. Uzanzibari ulivyo ni kwamba unamkusanya kila mtu ambae ana mizizi ya kifamilia kule huyu anaweza akawa mndengereko, mzaramu, msukuma,muarabu, mshirazi, muhindi etc na wala haumbagui mtu. Usitake kuleta siasa za Pan Africanism za 1960s ambazo ndio zimetuleta hapa, kama unahisi watu wenye asili ya kiafrika tu ndio wenye haki zaidi Zanzibar basi kwanini usiende Kenya kudai haki zako as well?, au hata Comoro?, kama si huu muungano ungeliweza hata kutoa kauli kama unayotoa leo? Zanzibar ni ya wazanzibari na wenyewe wanajuana.
 
Nafikiri ungekuwa unasoma vitu kwa jicho la uchambuzi . Hapo hiyo kodi anakusudiwa Mfanyabiashara mgeni (asiye Mzanzibari -na kwa maana hiyo asiye Mtanzania)). sasa Mfanyabiashara kutoka Bara siyo Mgeni yeye ni Mtanzania ambaye anafursa ya kuwa Mzanzibari baada ya kutimiza mambo fulani (ambayo tumeyakubali kwa mujibu wa Katiba na misingi ya Muungano wetu). sasa kwa nini anataka kujifanya kama mgeni (kwa kulipa kodi) baada ya kutimiza hayo mambo fulani akawa Mzanzibari na kufanya biashara zake kama Mzanzibari- Mtanzania (bila ya kodi ya ardhi?)

Na nyinyi mumezidi mbona Wazanzibari hawalalamiki wanapowekewa vikwazo kama hivi, kwanini gari zinazosajiliwa Zanzibar zinachukuliwa kama gari zilizosajiliwa nchi nyengine na zikiingia Bara basi zinalipa kila kitu kama gari za Kenya au Uganda. Kwa nini wanalipa kodi bandarini Dar wakiingiza mizigo yao na kwanini wanasachiwa mizigo yao kama wanavuka mpaka kuingia nchi nyengine? au ndio vile tena mkuki kwa nguruwe?. Waacheni na wao wakupeni taste of your own medicine.
 
Back
Top Bottom