Bidhaa kutoka Zanzibar kutolipishwa kodi, Serikali kuunganisha mifumo ya kodi Bara na Zanzibar

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,827
Ukinunua vitu Zanzibar na kuja navyo Tanzania Bara vitu husika vilikuwa vinalipiwa kodi ikiwa ni mara ya pili baada ya kulipiwa kodi Zanzibar kabla.

Jambo hilo linaenda kuwa historia baada ya kamishna wa kodi wa mamlaka ya mapato Zanzibar(ZRA), Yussuf Juma Mwenda kusema wanamalizia hatua za mwisho kuunganisha mifumo ya kodi ya Tanzania Bara na Zanzibar ili mtu alipe kodi mara moja pekee.

"Hili jambo likiisha, malalamiko yatasuluhishwa. Ukiwa na risiti halali kutoka ZRA au TRA hautalipishwa kodi mara mbili". Alisema.

The Citizen
 
Ila Kuna kodi inabidi tu zilipwe mara mbili, no way out, mfano kodi za VAT
 
Hivi ukitoka na bidhaa Dar na kwenda nazo Mologoro au Mwanza au Mbeya au Ntwala au Tanga unalipishwa ? na kote huko kuna bandari aka border.

Zanzibar ilikuwa isiwepo hata check point zaidi ya kuonyesha kitambulisho halisi na ilivyo kila mtu anatakiwa akitembea awe na kitambulisho cha Utaifa
Tupeni ukweli au ndio Zanzibar ni Nchi kamili na mamlaka yake bado kutangazwa rasmi au ndio wanaishi kizagazaga tu ?
 
Kodi lazima italipishwa hizo ni siasa tu kwa sababu viwango vya ushuru kwa mzigo unaoshuka Zanzibar vipo chini tofauti na mzigo unaoshuka bandari za Tanzania Bara hivyo ikiwa mzigo unaoshuka Zanzibar ukipelekwa bara ni lazima ukifika Bara ulipiwe ile tofauti ya ushuru waliyolipia Zanzibar mfano kama mzigo huo ukishuka Zanzibar wamelipa Tshs 50,000 lakini mzigo huo huo ungeshuka Bara ungetakiwa ulipiwe Tsh.75000 basi hiyo tofauti ya 25000 lazima ilipwe vinginevyo kila mfanyabiashara atataka kushusha mzigo Zanzibar kisha aulete Sokoni Tanzania Bara kitu ambacho kitaathiri mapato ya serikali.
 
Jambo hilo linaenda kuwa historia baada ya kamishna wa kodi wa mamlaka ya mapato Zanzibar(ZRA), Yussuf Juma Mwenda kusema wanamalizia hatua za mwisho kuunganisha mifumo ya kodi ya Tanzania Bara na Zanzibar ili mtu alipe kodi mara moja pekee.
Kero ya Muungano namba moja, vipi kuhusu kugawana mapato
 
Ukinunua vitu Zanzibar na kuja navyo Tanzania Bara vitu husika vilikuwa vinalipiwa kodi ikiwa ni mara ya pili baada ya kulipiwa kodi Zanzibar kabla.

Jambo hilo linaenda kuwa historia baada ya kamishna wa kodi wa mamlaka ya mapato Zanzibar(ZRA), Yussuf Juma Mwenda kusema wanamalizia hatua za mwisho kuunganisha mifumo ya kodi ya Tanzania Bara na Zanzibar ili mtu alipe kodi mara moja pekee.

"Hili jambo likiisha, malalamiko yatasuluhishwa. Ukiwa na risiti halali kutoka ZRA au TRA hautalipishwa kodi mara mbili". Alisema.

The Citizen
Kwa hili kidogo nawapongeza serikali maana ilikuwa ni kero kubwa sn
 
Hivi ukitoka na bidhaa Dar na kwenda nazo Mologoro au Mwanza au Mbeya au Ntwala au Tanga unalipishwa ? na kote huko kuna bandari aka border.

Zanzibar ilikuwa isiwepo hata check point zaidi ya kuonyesha kitambulisho halisi na ilivyo kila mtu anatakiwa akitembea awe na kitambulisho cha Utaifa
Tupeni ukweli au ndio Zanzibar ni Nchi kamili na mamlaka yake bado kutangazwa rasmi au ndio wanaishi kizagazaga tu ?
Kodi ikikatwa Zanzibar inaishia huko huko, haisaidi uchumi WA bara tofauti na Kodi iliyokatwa dar inaweza kutumika karagwe , hii ndio tofauti Kuu.
 
Ukinunua vitu Zanzibar na kuja navyo Tanzania Bara vitu husika vilikuwa vinalipiwa kodi ikiwa ni mara ya pili baada ya kulipiwa kodi Zanzibar kabla.

Jambo hilo linaenda kuwa historia baada ya kamishna wa kodi wa mamlaka ya mapato Zanzibar(ZRA), Yussuf Juma Mwenda kusema wanamalizia hatua za mwisho kuunganisha mifumo ya kodi ya Tanzania Bara na Zanzibar ili mtu alipe kodi mara moja pekee.

"Hili jambo likiisha, malalamiko yatasuluhishwa. Ukiwa na risiti halali kutoka ZRA au TRA hautalipishwa kodi mara mbili". Alisema.

The Citizen
watu wataenda kununua bidhaa zanzibar pekee, bara hawatanunua.
 
Ngoja tuone ila kama kodi za Zanzibar zitabaki vile vile basi Zanzibar ndio watakuwa wamecheza kama pele, mizigo mingi tabidi tushushie kwao, kukwepa gharama kubwa za huku kwetu bara, hivyo bandari yao itakuwa busy zaidi.
 
Back
Top Bottom