Slaa sisi ni watu wazima na timilifu

Status
Not open for further replies.
Mungu katuumba na alichokifanya ni kufanya mawazo yetu yasifanane, kila mtu anawaza kivyake ila mawazo ya huyu mleta mada sijui aliumbwa na nani'
 
Sasa hivi ml60 za kila mwezi mbona hatukuwahi kusikia popote wala kujua? Au kwa sababu wengine hatupo makao makuu? Imekuwaje chama kitoe ukweli kuhusu hii michango ya ml.60 baada ya msuguano wa Nape na CDM?

Sasa nadhani ni muda muafaka wa chama kubainisha wazi vyanzo vyote vya mapato na matumizi yake hata kupitia website ya chama ili kila mwanachama aweze kujua vizuri mapato ya chama na kuondoa sintofahamu na propaganda chafu za CCM.

Naomba kuwasilisha.

Uliwahi kukichangia mara ngapi CDM? CCM huwa wanatoa mahesabu yao?
 
Basi Chadema wakafute kesi ya NAPE kama haya yanaukweli.

Nape alisema kuwa CDM wanapewa pesa chafu na nchi za ulaya ili kuvuruga
amani Tanzania.Hakusema wanapewa na chama toka nje bali Nchi.Sasa hapo
ndio anatakiwa athibitishe hiyo nchi ni ipi.Hili swala la chama kusaidia CDM
lilishajitokeza tena siku za nyuma na Dr akalitolea ufafanuzi,sasa sijui nape
alikuwa wapi kipindi kile.
 
Kwahiyo Nape hakudanganya!!!

Sijui tuseme alidanganya au alitia chumvi au alipotosha umma na kuchanganya mambo. alihusisha misaada hiyo na mikataba ambayo baadaye itakigharimu taifa kwa kupoteza au kulazimika kutoa mali asili. Actually yeye anajua ukweli huo unaojadiliwa hapa, isipokuwa alikuwa kazini akakuta amepitiliza.
 
Kwahiyo Nape hakudanganya!!!

Kama amedanganya au anasema ukweli kwetu si hoja, hoja ni kuifungua ile mikoba anayodai kutembea nayo kwenye gari, na kuishawishi Mahakama pasipo shaka "KWA NINI ASIFUNGWE KWA UZUSHI"!
 
Hata wakipewa bilioni 60 inakuhusu nini anzisha cha kwako pia km umeona ni mradi hichi kinachokusanya kodi zetu kwa lazima na kuwaibia maskini ni ngapi kwanini usikihoji?
Think twice.
 
NIMECHOSHWA NA KAULI ZA MZEE WETU SLAA, eti kuwa wanapata msaada usiozidi milioni 60 kutoka kwa chama cha kikisto cha ujerumani sasa swali langu nauliza, kila mtu dunia hii anafahamu ubaya na uzuri ya misada ya wazungu kwa maana hakuna cha bure, na kwakuwa chadema tumeshuhudia kwa hapahapa tanzania wanauwezo wa kuchangisha mamilioni ya pesa kwa siku moja nawanchangia bila kupewa masharti, sasa kuna ulazima gani wa kwenda kwa wazungu hawa kupiga magoti kupewa milioni 60kwa mwaka??
funguka wewe!....,unaji uma uma nin wewe? toa unafiki wako humu ndani
 
In Psychology we call it 'fear of unknown'. Kuogopa vitu/kitu usicho kijua!

Hatuogopi tusichokijuwa:

quote_icon.png
By zomba

Wana chadema, ni masikitiko makubwa kuona hawa ndio marafiki zenu na wafadhili wa kuwaendeleza kisiasa, Jee, hizi ndio siasa wanazowafadhili kuzileta Tanzania?

Huyu mama ndio Kiongozi wa Christian Democratic Union ya Ujerumani, ambao wenyewe wamekiri kuwa wanawadhili chadema kuwaendeleza kisiasa. Na Katibu Mkuu wa Chadma pia kakiri kuwa wanapokea misaada ya kuwaendeleza kutoka hiki chama cha kisiasa cha Kikristo.

Kwa kifupi, huyu Mama hapa chini anaoneshwa akimzawadia tuzo na kupongeza mchora katuni za kumkashifu Mtume Muhammad (SAW):

Merkel honours Danish Muhammad cartoonist Westergaard


A depiction of Muhammad's turban as a fused bomb sparked global outrage when it was published in Denmark.
Presenting him with a press freedom award, Mrs Merkel said Mr Westergaard was entitled to draw his caricatures.
"Europe is a place where a cartoonist is allowed to draw something like this," she said.
"We are talking here about the freedom of opinion and the freedom of the press," Ms Merkel said at the ceremony in the German city of Potsdam.

The offending cartoon - which led to a groundswell of Muslim anger in many countries around the world - was one of 12 first published by Danish newspaper Jyllands-Posten in 2005.

_49034086_010135181-1.jpg


Angela Merkel congratulates Danish cartoonist Kurt Westergaard on his prize

Soma zaidi: BBC News - Merkel honours Danish Muhammad cartoonist Westergaard
 
Nyinyi mbona mnaongelea jambo lililopo mahakamani? CDM wamemshtaki Nape juu ya jambo hili so midomo shut!
 
Nape alisema kuwa CDM wanapewa pesa chafu na nchi za ulaya ili kuvuruga
amani Tanzania.Hakusema wanapewa na chama toka nje bali Nchi.Sasa hapo
ndio anatakiwa athibitishe hiyo nchi ni ipi.Hili swala la chama kusaidia CDM
lilishajitokeza tena siku za nyuma na Dr akalitolea ufafanuzi,sasa sijui nape
alikuwa wapi kipindi kile.
Mkuu nchi si ni Ujerumani? Kumbe hakusema serikali ya nchi fulani! Tusubiri tuone mahakama itasemaje; kesi nzuri sana manake unaweza shituka Nape anatakaswa!

CDM walikuwa na mawazo mazuri sana ya kuchangisha pesa toka kwa watanzania kuanzia wakulima, wafugaji, machinga, wakwezi, nk. Hii michango huwa haina masharti mengi na makubwa. Sharti moja tu kwamba tunataka muingie madarakani mtutumikie sisi watanzania wenzenu. Lakini sasa hili la misaada toka nje huwa lina masharti mengi na magumu. Sharti lao linafanana na lile la wachangiaji watanzania nalo ni tunawasaidia muingie madarakani ili mtutumikie! Badala ya kutumikia Watanzani utanza kuwatumiki wachangiajia wa nje. No free lunch in this world.
 
NIMECHOSHWA NA KAULI ZA MZEE WETU SLAA, eti kuwa wanapata msaada usiozidi milioni 60 kutoka kwa chama cha kikisto cha ujerumani sasa swali langu nauliza, kila mtu dunia hii anafahamu ubaya na uzuri ya misada ya wazungu kwa maana hakuna cha bure, na kwakuwa chadema tumeshuhudia kwa hapahapa tanzania wanauwezo wa kuchangisha mamilioni ya pesa kwa siku moja nawanchangia bila kupewa masharti, sasa kuna ulazima gani wa kwenda kwa wazungu hawa kupiga magoti kupewa milioni 60kwa mwaka??
Mkuu watanzania wa leo si wa kuuziwa upuuzi kama huu wa kwako. Kama kuna watu wa kulalamika juu ya chama fulani kusaidiwa pesa toka nje basi si CCM au Nape; kwani huyu Nape anaelewa fika ni kiasi gani chama chake kinapokea toka nje na ndani kwa magenge ya kihalifu ya mitandao ya madawa ya kulevya achilia mbali michango toka kwa vibakauchumi waliosheheni ndani ya chama chao na kulindwa na CCM. Nape ameshindwa kuwaeleza watanzania ni kiasi gani CCM wanapokea toka China, Irani, Korea na nchi kibao wanazoziita nchi rafiki! Kama anabisha atoke hadharani atoe takwimu za kiasi gani CCM inapokea toka huko na kiasi walichoiba toka asasi kama Benki Kuu, iliyokuwa Bima ya Taifa (ambayo waliiua kabisa)TANESCO, na mashirika mengi ambayo tuna data zake. fedha wanayopokea CHADEMA toka kwa marafiki zao ni za wazi, zinafahamika ni kiasi gani na zimetumikaje na zinakaguliwa; za CCM je?
 
Sijui tuseme alidanganya au alitia chumvi au alipotosha umma na kuchanganya mambo. alihusisha misaada hiyo na mikataba ambayo baadaye itakigharimu taifa kwa kupoteza au kulazimika kutoa mali asili. Actually yeye anajua ukweli huo unaojadiliwa hapa, isipokuwa alikuwa kazini akakuta amepitiliza.

Ki logic alikuwa sawa. Tumeona misaada inavyotuumiza. Unapewa misaada ambayo imeambatana na masharti lukuki mengine ya wazi lakini mengine yamefichama!
 
Labda tumuombe Slaa awe muwazi zaidi na kuweka bayana memorandum ya ushirikiano wao na hicho chama. Lazima kutakuwa na makubaliano yanayotengeza ushirikiano na chama hicho, je makubaliano hayo yanasemaje? kila pande inawajibika kutekeleza yapi katika uhusiano huo? upane wa CHADEMA wananufaika kwa msaada wa "uwezeshaji", je upande wa CDU wananufaika namna gani?
 
Acha Uzuzu wewe, Kila Chama huwa kina Vyama Rafiki na CCM vyama vyake Rafiki na ambavyo huwa vinaipatia CCM pesa ni Vyama vya Kikomonist China, na hata ANC cha south, Ila vingine ni vya Africa sema havina Uwezo wa Kusaidia CCM,
r
CHADEMA nao wana vyama Rafiki kama vya Ghana, Liberia, Republican, Conservative cha Uingereza, CDU na vingine vingi, Na kuna Muungano wao unaitwa DU, so kusaidiana huwa ni jambo la kawaida na si Pesa za Za Serikali bali za kwao wenyewe, Hata CHADEMA wanao uwezo wa kusaidia vyama vilivyo kwenye huo umoja wao, na hizo pesa zina Kaguriwa na Mkaguzi CAG, na ni pesa kwa ajiri ya CAPACITY BUILIDING si za Kampeni wala nini, na hata CCM wanajua hilo na si ishu ya Siri ni ishu ya Uwazi kabisa

Na hata hivyo vinavyo saidia CCM ni kwa ajiri ya kuendesha shughuli za kiofisi na si Kampeni, hakuna Nchi ya Kijinga inayo weza kusapoti chama cha Nchi nyingine kwenye Kampeni kwa sababu wanatambua Madhara yake, na hata Policy za uhusiano haziruhusu

Sasa Nape yeye anatakiwa Kudhibitisha Nchi na si Chama, na MOU iliyo sainiwa kati ya CHADEMA na hizo Nchi, so hapo ndo kazi ilipo

CHADEMA Ruzuku ya Milioni 200 NA ZAIDI KWA MWEZI Watashindwa kufanya mikutano?

wewe ZUZU mkuu, na mazuzu wenzako wa CHADEMA, mnieleweshe hapa alichokisema nape nauye na alichokipinga mnyika, na alichokiri mpumbavu wenu slaa asiye na akili na mwenye elimu isiyomsaidia vina tofauti gani???
 
CHadem and its followers are stupid.......opportunists....wasio na akili, kinachoniudhi, wameharibu vijana wengi na kuwajaza upuuzi...bora miaka 1000 ya uongozi wa CCM kuliko dakika moja ya uongozi wa CDM.....watatupeleka pabaya....wanachojali wachaga wale ni hela tu...na ushahidi upo....WAPUUZI TUPU.......NA UBAYA, JF IMEJAA MAZUZU NA MAPUUZI YA AINA HII,,,,,,CDM NI KIRUSI TU....
 
Ndugu ukubali ukatae ukishakuwa 3rd world country lazima wewe ni mtu wa kupewa misaada tu. Sasa kama serikali iliyoko madarakani inategemea misaada unashangaa lipi kwa Vyama vya upinzani ambao ki ukweli hata hiyo ruzuku haitoshi na imewekwa ili kuwazuia wasiweze kuwafikia watanzania. My take ni kwamba kupewa msaada si tatizo, tatizo ni kwamba unautumia vipi huo msaada ili kujinasua kwenye hali mbaya ya kiuchumi na kuweza kuwa unajitegemea bila misaada. kuna nchi nyingi za Asia ambazo zilikuwa zinategemea misaada lakini wameweza kuitumia vizuri hii misaada na rasilimali zao na sasa wanajitegemea.
Vita iliyopo hapa Africa si ya wananchi na Mataifa makubwa ya wazungu bali ni wananchi na viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza nchi za Africa si waaminifu na hili ndio tatizo katika nchi nyingi za Africa.
Zana ya kusema matatizo yetu yameletwa na wazungu au mataifa makubwa ni zana potofu na mufilisi na imeanzishwa na viongozi ambao si waadilifu baada ya kuona wanakosolewa na mataifa makubwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, ubadhirifu na kushindwa kufuata demokrasia ya kweli. Jiulize ni nani anaeingia kwenye mikataba mibovu na wawekezaji?, ni nani ambao wanamiliki akaunti za mabilioni nje ya nchi? ni nani ambao wanashiriki katika kupindisha sheria za nchi kwa maslahi yao ya kisiasa?
kwani hao wazungu wametoa mashart gani? Funguka mpaka mwisho ili tukusaidie.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom