Slaa akanusha vikali taarifa za Rostam kuunga mkono CDM Arumeru; Vita ya Saikolojia kuendelea!

Kulikuwa na taarifa zimeenezwa na hata kuwafanya baadhi ya watu kuamini - kimsingi wakitilia mashaka msimamo wa CDM na mafisadi. Dr. Slaa ametoa maelezo mafupi juu ya hilo:

Kuelekea siku hizi chache zilizobakia kutakuwa na majaribio ya kuteka akili za wapiga kura kwa kutangaza taarifa mbalimbali na tusishangae kama vyombo vya habari vya serikali vikatumika kutoa taarifa ambayo itachelewa kusahihishwa ambayo itatoa madai fulani. Madai hayo yaweza kuwa ni yale ya kuonesha kuwa matokeo tayari yako wazi kwa CCM kushinda kwa mfano "CCM yaelekea kushinda". Mbinu kama hii tumewahi kuona ikitokea sehemu nyingine ambapo watu wanakata tamaa na kuacha kupiga kura kwa sababu tayari CCM itashinda.

Mojawapo ya vitu vinavyosumbua sana ni hisia kuwa hakuna jinsi ya kushinda kwani CCM ina serikali, vyombo vya dola, Tume n.k na hivyo kushinda itakuwa kazi sana. Matokeo yake baadhi ya watu wanaweza kuamini kabisa kuwa kura zao hazina maana yoyote kwani hata wapige kura vipi bado "zitachakachuliwa". CDM haina njia nyingine ila:

a. Kuonesha ugumu wa kuiba kura za wabunge hasa kama watu wanapiga na kuwa tayari kulinda kura hizo - watu wajue ni lazima matokeo ya kila kituo yatangazwe hadharani na wananchi wanayo haki na ruhusa ya kupiga picha matokeo hayo na kuyatangaza mahali popote.

b. Kura zote zinahesabiwa kwenye vituo; hakuna kuhamisha masanduku kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine "ili zihesabiwa". kura zote zinahesabiwa kwenye vituo zilipopigiwa na baada ya kukamilisha matokeo ni LAZIMA yawekwe nje ya kituo kwa mtu yeyote kuyaona.

c. Mawakala wa vyama ni sauti ya chama hicho kwenye chumba cha kura; hivyo chama kinatarajiwa kuwa na mawakala waadilifu, wenyeji na watu wanaojua maeneo hayo na ni jukumu lao kuhoji, kuuliza jambo lolote ambalo wanaona haliendi sawa. Kwa mfano, kwenye chumba cha uchaguzi hairuhusiwi kuleta sanduku jingine la kura kutoka nje mara baada ya vifaa vyote kuchunguzwa mwanzo wa siku ya kupiga kura. Mabadiliko yoyote ya utaratibu mawakala wanaruhusiwa kunukuu na wakiwa makini waweze kuandika chini.

d. Wakati wa kuhesabu kura mawakala ni lazima wawe na sehemu yao wenyewe ambapo wanahesabu kura na kujumlisha. Matokeo ya kujumlisha kura hayawezi kutofautiana hata kwa kura moja! Kama wamehesabiwa watu 1000 kupiga kura zote ni lazima ziwe 1000 (halali, zilizoharibika n.k). Mawakala ni lazima wahakikishe kura zinajumlishwa kwa usahihi na kuwa makini wanapohesabu na kuamua kura zilizoharibika.

Vyovyote vile ilivyo, CDM wanapaswa kuwa makini na vita ya saikolojia inayoendelea.
Mkuu Mwanakijiji ujumbe huu ungetolewa na tume ya uchaguzi kuweka mambo wazi ili siku ya kupiga kura kusiwe na mikanganyiko!!!!!Watu wa tume watoe utaratibu wa shughuli za kupiga kura kwenye kituo hadi kutangazwa matokeo!!!! Ujumbe wako ni sahihi kabisa wahusika wachukue hatua!!!!
 
Mwanakijiji
Nadhani wewe au DR SLAA au wote wawili mnatakiwa kuwa clear zaidi kuepusha mianya ya upotoshaji. kwa Kadri gazeti husika lilivyoandiaka inawezekana kweli Rostamu alifika Arumeru sababu wameeleza kwamba alikuwa kwenye mizunguko ya kibiashara. Hivyo DR SLAA angeweka wazi kama ni kweli Rostamu ameonekana Arumeru, sababu kwa ufupi wa maelezo yake na kama ni kweli Rostamu alionekana huko mwanya wa upotoshaji unakuwa haujadhibitiwa. Mategemeo yangu ni majibu ya Namna hii.

Ama
Habari hizo ni za upotoshaji asilimia mia moja sababu Rostamu Azizi hajaonekana Arumeru Mashariki.

Au
Ni kweli Rostamu Azizi Ameonekana Arumeru hivyo inawezekana akawa ametoa kauli hizo eneo lolote alikonukuliwa akiwa ndani ya Arumeru, lakini haijatokea Rostamu kuzungumza akiwa kwenye Jukwaa la Chadema, Na kama hili limetokea basi inawezekana muandishi anamaanisha kwamba Rostamu amezungumza akiwa kwenye maeneo ambayo CHADEMA inakubarika kwa wingi sana lakini sio sahihi kusema kwenye makambi ya CHADEMA kwa sababu CHADEMA haina kitu kinaitwa makambi kwenye muundo wake.

Na kwamba, Rostamu kama Raia ana haki ya kutoa Uhuru wa Mawazo yake juu ya mchakato wa Arumeru Mashariki lakini hilo haliondoi ufahamu wa CHADEMA kwamba Yeye ni mmoja wa wana CCM waliochangia kuzorotesha utendaji wa serikali ya awamu ya nne kwa kuingiza biashara zao za kifisadi kwenye michakato ya uendeshaji wa srikali na kwamba Mpaka sasa ni Imani ya CHADEMA kwamba Rostamu ndio mmliki wa kampuni ya Kagoda. na msimamo wa CHADEMA ni kwamba anatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Mkuu Matola, heshima mbele sana kiongozi.

Hii ni post ya nne au tano nakutana na habari ya picha za maji marefu, unaweza kuziweka hapa ambao tumepitwa tuzione na issue yenyewe ilikuwa inahusu nini mkuu, kama vipi tuwekee hata link ya hiyo habari, samahani kwa usumbufu mkuu.
majimarefu.jpg
 
Hizo ndo siasa za Tanzania kwa wakati huu, yatasemwa mengi sana lakini ukweli utabaki pale pale kwamba CDM ndo kiboko ya mafisadi.
 
Mwanakijiji
Nadhani ama wewe na DR SLAA au wote wawili mnatakiwa kuwa clear zaidi kuepusha mianya ya upotoshaji. kwa Kadri gazeti husika lilivyoandiaka inawezekana kweli Rostamu alifika Arumeru sababu wameeleza kwamba alikuwa kwenye mizunguko ya kibiashara. Hivyo DR SLAA angeweka wazi kama ni kweli Rostamu ameonekana Arumeru, sababu kwa ufupi wa maelezo yake na kama ni kweli Rostamu alionekana huko mwanya wa upotoshaji unakuwa haujadhibitiwa. Mategemeo yangu ni majibu ya Namna hii.

Ama
Habari hizo ni za upotoshaji asilimia mia moja sababu Rostamu Azizi hajaonekana Arumeru Mashariki.

Au
Ni kweli Rostamu Azizi Ameonekana Arumeru hivyo inawezekana akawa ametoa kauli hizo eneo lolote alikonukuliwa akiwa ndani ya Arumeru, lakini haijatokea Rostamu kuzungumza akiwa kwenye Jukwaa la Chadema, Na kama hili limetokea basi inawezekana muandishi anamaanisha kwamba Rostamu amezungumza akiwa kwenye maeneo ambayo CHADEMA inakubarika kwa wingi sana lakini sio sahihi kusema kwenye makambi ya CHADEMA kwa sababu CHADEMA haina kitu kinaitwa makambi kwenye muundo wake.

Na kwamba, Rostamu kama Raia ana haki ya kutoa Uhuru wa Mawazo yake juu ya mchakato wa Arumeru Mashariki lakini hilo haliondoi ufahamu wa CHADEMA kwamba Yeye ni mmoja wa wana CCM waliochangia kuzorotesha utendaji wa serikali ya awamu ya nne kwa kuingiza biashara zao za kifisadi kwenye michakato ya uendeshaji wa srikali na kwamba Mpaka sasa ni Imani ya CHADEMA kwamba Rostamu ndio mmliki wa kampuni ya Kagoda. na msimamo wa CHADEMA ni kwamba anatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Umenisaidia sana! Tena nakupa asante ya kikweli jumlisha na "I like" ya kubofya. Mzee Mwkjj anageiweka hivi thread yake ingesaidia sana sana!
 
Mkuu Mwanakijiji ujumbe huu ungetolewa na tume ya uchaguzi kuweka mambo wazi ili siku ya kupiga kura kusiwe na mikanganyiko!!!!!Watu wa tume watoe utaratibu wa shughuli za kupiga kura kwenye kituo hadi kutangazwa matokeo!!!! Ujumbe wako ni sahihi kabisa wahusika wachukue hatua!!!!
hao tume ya uchaguzi wanaelewa yote haya na nadhani wanasikia hasira wakisoma hii post hapa maana wanataka wananchi waendelee kuwa wajinga ili 'malengo' yao ya kusaidia chama fulani yafanikiwe.

Sijui kama wametafakari kuwa 'ujinga' wa watz sasa hausaidii tu ushindi wa watu fulani katika uchaguzi na siasa bali unasidia hata 'uvamizi' wa majirani zetu kuwa rahisi kama tunavyoona sasa.

Ni bora NEC waachie watu wafanye maamuzi yao bila kukwazwa

Inaonesha wewe ni afande! ngoja nimwite advocate wangu ili nikijibu awe karibu kusikia majibu yangu

Afande anayetimiza wajibu wake pasi na kushurutishwa ama kwa nia ya kumfurahisha mtu/kikundi fulani cha watu!!!!
 
aisee kumbe picha ilikua hivi mwanzoni hatukujua sasa tumejua aibu yenu
 
Hapa kumbe mama wa Vifaranga kweli alivuta mkwanja kimya kimya akawaacha vifaranga wanang'aa macho tu
 
Back
Top Bottom