FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,893
- 109,227
i smell something fishy. Hayupo nasi tena. Ila 67 unatuongopea wewe kwamba ulikuwepo darasa hilo
You have the right to your thinking. Try me.
i smell something fishy. Hayupo nasi tena. Ila 67 unatuongopea wewe kwamba ulikuwepo darasa hilo
You have the right to your thinking. Try me.
ulishaone lile tangazo la Twaweza? Lile ambalo wanafunzi wanakimbia mchakamchaka, wanajifunza stadi za maisha na mengine. Hiyo ilikuwa enzi za Mwalimu. Baada ya hapo mambo yakabadilika. Sasa wanafunzi wanaenda shule wanakaa chini, madarasa yamebomoka, n.k. Twaweza walikosea?
Baadhi ya wanafunzi wa moja ya Sekondari za kata, Rombo wakiwa darasani
Baadhi ya wanafunzi wa Sekondari ya Urauri, Wilaya ya Rombo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mojawapo ya darasa katika shule mpya ya sekondari ya Masengwa wilayani Shinyanga muda mfupi baada ya kuifungua rasmi jana mchana.25-01-2010
Mimi nimeacha kutizama kabisa, naona kama naweza kuzimia. Hawa watoto wanamjua 50 cent lakini hawamjui hata rais wa awamu ya pili wa Nchi hii.
Leo hakuna hata Atlas yenye kuonyesha miji, mikoa, mataifa mbalimbali na hata hali ya hewa. Hawa mabepari mamboleo wameviondoa kabisa, inatia hasira.
Hata somo la sanaa wamefuta!
Na ushahidi wa wazi hata hapa JF, graduate mzima anaandika "dhambi" - zambi, "uongo" - uhongo...nk nk. Si hilo tu hata suala dogo la kuweka 'paragraph' linawashinda. Huu ni msiba.
This is not random selection. Ulitegemea Rais akafungue kimeo? Hata kati ya vipofu mwenye chongo mfalme. Elimu yetu dada Faiza imedidimia hasa miaka ya karibuni
Dogo kila swali hajui mwisho akaulizwa habari za diamond anamjua kuliko wazazi wake,alipopewa chance wacha aimbe karibia nyimbo zote za diamond,
Ukweli tatizo linaanzia mashuleni mpaka ndani ya family zetu,tusitegemee maajabu sana kama walimu wenyewe ndio hawa waliopata dv 4 na wazazi wenyewe hawa wakisasa wakirudi home mkononi wana magazeti ya udaku na na DVD za bongo movie,tuna kazi ndefu sana
Umesaema atlas nimekumbuka, tulikuwa tunapenda kucheza michezo wa kutafuta miji kwente atlas.
Anayeona, anachagua yeye mji mtafute.
Ilikuwa inasaidia sana kujua ramani, it was fun.
Hivi tuna ramani ya mikoa mipya kweli? Uoto wa asili sijui na ma nini nini?
Mwingine akaulizwa mdahalo ni nini??
akiwa hajui maana ya mdahalo alijibu hivi.
1. unachukua mdahalo wako unauosha vizuri.
2.hakikisha mdahalo wako haujakomaa.
3. bandika sufuria yako jikoni.
4. wekamdahalo wako kisha uache uchemke kwa dakika kumi na tano.
5. mdahalo wako ukiwa tayari uepue.
6.mdahalo huu unaweza kuula na kinywaji chochote.
Hii issue ilikuwa very interesting, unakuta unachagua mto umeandikwa kwa herufi ndogo alafu unamwambia mwenzako autafute, siku hizi hata mtu umuulize mto Malagalasi hajui ulipo, niliwahi kukutana na swali toka kwa dogo yupo form 3 ananiuiza kama Dodoma kuna ziwa
Hahahah....but before you do that remember;
No matter how hot your anger is, it can not cook yams-Nigeria
back to Topic:
Nakumbuka nikiwa sekondari ya Mawezi, Moshi.
Likizo tulikuwa tunakutana na washikaji tuliosoma wote primary halafu wakapangiwa special schools Kibaha, Mzumbe, na Ilboru.
Na wale wa seminary ambapo wanapewa notes na test kila wiki…jamani kuna watu wana raha.
Basi hawa woote tunakutana mtaani tunafundishana weee na kubadilishana knowledge mpaka likizo inaisha…hiyo ndo ilikuwa tuition yetu. Ndiyo si tulisoma wote primary kwahiyo bado ni marafiki.
Na likizo wanakuja nyumbani. Wana interact na sie wa shule za kata tunabadilishana mawazo.
Matokeo form four: Division one (leo hii ningekuwa top ten ya watahiniwa wa CSEE 2012)
A level nikapangiwa Same sekondari. Huko tukawa tunatoroka na kuja kupiga kitabu Moshi sekondari (Old Moshi Sec) wenyewe waliamua kujiita Gold Moshi…dem dayz!
Likizo tena tunakutana na washkaji waliopangiwa Special schools hizo tunabadilishana utirial ma test pepa manini.
Matokeo form six: Division one nzuri tu ya kunipa grades za kusoma Electronic Science & Communication chuo.
Mtazamo wangu:
Ile dhana ya special schools ilisaidia sana kuboresha elimu na kuongeza morali wa wanafunzi kusoma.
My call:
- Sasa hivi unakuta mwanafunzi anasoma hapo hapo na wale wale aliosoma nao primary hawapati challenges za nje hata kidogo.
- Waliofuta special schools hawakukumbuka ule usemi wa, "the world is a book and those who don't travel read only a book" otherwise walidhani kina Nyerere pamoja na umaskini tuliokuwa nao bado walifanya hivyo. Walipeleka hadi watu kusoma nje kwanini???
Kawambwa & Co. rudisheni special schools kwa maana ile ile ya special schools….
Ha ha ha, ungemwambia kuna ziwa Mtera.
Ilikuwa raha sana kutafuta miji, mito
Ila kuna mmoja aliwahi tusumbua, tulitafuta kwa saa nzima hatuoni, tena ilikuwa ramani ya asia
Kasema tutafute 'mate', tumetafuta hadi tumechoka tunaomba atuoneshe
Kumbe katema pembeni kwenye ramani, afu akatuonyesha mate si haya hapa. Kidogo tumuue
Sitakaa nimshahau yule binti
Pia sisi kama taifa hatujaamua kuchagua mfumo wa elimu inayotufaa nakupata elimu endelevu,kwamfano unayoizungumzia ni elimu tuliorithi kutoka kwa mkoloni tukaiboresha ikaenda nasi kwa wakati huo,kumbuka pia baada yahapo tukaona kama elimu hiyo ilipitwa na wakati tukaja na maboresho mengine ambayo yalizidi kututumbukiza shimoni ikiwa ni kuongeza idadi ya watoto wanao anza elimu ya awali na darasa la kwanza,baada yahapo tukaja namfumo waelimu ya kata nayo ilkuja kwa nia njema kwamba idiadi ya vijana wanasoma sekondari na kuhitim iongezeka lakini tukasahau nyuma mambo muhimu katika uwasilishwaji wa elimu hii,ikiwamo uhaba wa waalimu na vitendea kazi,ubadirishwaji wa mitaala bila ya kuwapa waalimu miongozo nk.
Naona sasa niwakati wakuchagua kilicho bora na chenye manufaa katika elimu yetu ilikutuwezesha kuzalisha wataalam wenye ufanisi na watakao weza kukabiliana na changamoto zandani na nje ya nchi
Kwa mtazamo huo huo ni heri turudi kule kwa wakoloni...then tuendelee from there!!!
Nimeipenda hii mdau, kweli hii au mazungumzo baada ya habari ya enzi zile za "Tenge mkwapua nyama"