Mahojiano na Mohamed Vall wa Al Jazeera 2007

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
MAHOJIANO NA MOHAMED VALL WA AL JEZEERA 2007

Jana nilikuwa naangalia Al Jazeera yanayotokea Gaza mara nikamuona mtangazaji wa Al Jazeera, Mohamed Vall anatangaza habari za vita hivi.

Mohamed Vall akanikumbusha mahojiano tuliyofanya nyumbani kwangu Dar es Salaam na Tanga kati ya mwaka wa 2007 na 2008.

Hiki ni kisa cha kipekee katika maisha yangu ya kuhojiwa na vyombo vya habari.

Al Jazeera ilituma waandishi wake wakiongozwa na Mohamed Vall kuja Tanzania kufanya naamini ''documentary.''

Walinipigia simu Tanga na kuniuliza kama naweza kuja Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano au wao wanifate Tanga.

Nilikuja Dar es Salaam na wakafika nyumbani kwangu asubuhi kwa kuangalia mandhari ya nyumba yangu na kuipanga kwa namna waitakayo wao kwa ajili ya kufanya kipindi.

Kwa ufupi walibadilisha muonekano wa ukumbi wangu waliporidhika wakanifahamisha kuwa watarejea usiku kwa ajili ya mahojiano.

Mohamed Vall ndiye aliyenihoji na tulifanya kipindi cha takriban saa moja.

Tulizungumza kitu gani?
Al Jazeera walitaka kujua historia ya Waislam wa Tanzania.

Katika team yao kulikuwa na kijana mmoja yeye aliniambia kuwa ni Mtanzania na akinifahamu kwa miaka mingi sote tukiwa watoto Kinondoni.

Kwa hakika sura yake haikuwa si ngeni na alikuwa na muonekana wa Kisomali.

Nakumbuka kipindi kizima nilichokuwa nahojiwa mwanangu wa kwanza alikuwa kasimama mbele yangu sawasawa na mimi akiniangalia.

Sijui nani alimtuma kunikalia mbele yangu lakini kwa namna ya ajabu sana yeye akawa kama kioo cha mimi kujiangalia na kujitathmini.

Kila nilivyokuwa nikizungumza nilikuwa namuona kwa jicho langu la pemebeni akitabasamu na wakati mwingine akitingisha kichwa kama kusema, ''Ahsante,'' au ''Hakika,'' nk.

Sura ya mwanangu ilikuwa kama vile inaniambia kuwa maneno yangu niliyokuwa nasema yalikuwa mazuri yamamfurahisha.

Mwanangu alinikumbusha siku nafanya mtihani wa English Oral, Mtihani wa Cambridge 1970.

Siku zile tulikuwa tukitihaniwa Kiingereza kwa kuzungumza mbali na mtihani wa kawaida wa kujibu maswali kwa kuandika.

Mwalimu wangu wa English na Literature Miss Menez, msichana wa Kigoa siku ile alikuwa katika chumba cha mtihani na alikuwa kaweka kiti chake sawa na mimi uso kaukunja ananiangalia na kunisikiliza.

Nakumbuka jana yake wanafunzi wa Literature alituita na kutuambia kuwa ikiwa sisi wanafunzi wake hatukupata Merit Pass yaani First Class basi na yeye pia atakuwa kafeli mtihani.

Nilipokuwa najibu maswali nilimuona Miss Menez, wanafunzi sie kwa utundu wetu tulimpa jina, ''Lanky,'' kwa ajili ya urefu na wembamba wake.

Sijua nani alikwenda kumuambia.

Siku moja darasani akatuambia huku akicheka kuwa anajua jina tulilompa.

''So my golden class you have given me a nickname...''

Turejee kwa Al Jazeera.

Kila mazungumzo yalivyokuwa yanasonga mbele nilikuwa nawaona watu wa Al Jazeera ambao kwa hakika ndiyo walikuwa hadhira yangu walikuwa kama vile wanazamishwa na yale niliyokuwa nasema.

Sura zao ukiziangalia walikuwa wanafuatilia kila sentensi niliyokuwa naitoa.

Historia ya Waislam na uhuru wa Tanganyika na yaliyotokea baada ya uhuru siku zote imekuwa kisa cha kupendeza na kuvutia kusikiliza.

Mohamed Vall nakumbuka swali lake la mwisho aliniambia kuwa kesho alikuwa na mahojiano na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu.

Je, anaweza kuninukuu na kumuuliza maswali Rais kutafuta ukweli kwa yale niliyozungumza?

Jibu langu lilikuwa anaweza.

Baada ya kumaliza mahojiano haya wale vijana walinipongeza wakisemea kipindi kilikuwa kizuri sana.

Nilisubiri kwa muda mrefu kipindi kirushwe.

Hakikurushwa.

Baadae zikanifikia taarifa kuwa baada ya kumaliza kufanya vipindi Tanzania Bara walikwenda Zanzibar kwa mahijoano mengine.

Tape zao za vipindi vyote walivyofanya Tanzania Bara na Visiwani vilipotea hotelini Zanzibar.

Baada ya mwaka mmoja hivi Mohamed Vall na wenzake walirudi tena Tanzania na wakaja Tanga kwa mahojiano.

Sijui nini kilitokea safari hii.
Kipindi hakijaenda hewani hadi leo.

Picha ya mwisho ni mahoajiano na Mohamed Vall Tanga, Bombo Area 2008 nyingine ni mahojiano Dar es Salaam, Masaki 2007.

1696938074181.png

1696938104924.png

1696938130971.png

1696938164783.png
 
Tena bahati yako rais alikuwa JK muislam mwenzako, ingekuwa bwana John ungeozea jela na wale wapemba magaidi, tape hazikupotea, wanausalama walizichukua baada ya kuona hazina afya kwa usalama na mustakabali wa nchi, ulikuwa ni uchochezi
 
Tena bahati yako rais alikuwa JK muislam mwenzako,ingekuwa bwana John ungeozea jela na wale wapemba magaidi,tape hazikupotea,wanausalama walizichukua baada ya kuona hazina afya kwa usalama na mustakabali wa nchi,ulikuwa ni uchochezi
Mdukuzi,
Unaghadhibika kwa haraka sana.

Hayo niliyoeleza katika kipindi cha Al Jazeera yote yamo katika kitabu cha Abdul Sykes toka 1998.

Kitabu hakijapigwa marufuku kinasomwa miaka yote hii.

Tofauti ni kuwa katika Al Jazeera wangeniona na kunisikia.
 
Walifanya vyema kuzuia huo upuuzi usirushwe hewani.
Mbona kama una chuki za wazi ndugu yangu. Muda mwingine muwe mna walau mababu zenu Kwa uvivu wao awajaandikwa popote ila mwenzetu walau anacho Cha kutusimulia mababu zake walikuwa mashughuri. Japo history imekataa katu katu kuwataja.

Mimi binafsi huyu baba yangu Mohamed Said namkubali sana japo mnampa maneno ya kumvunja moyo lakini hayumbi Wala hateteleki.​
 
Nahisi labda wameiweka kiporo muda wa kuitoa hiyo documentary Bado haujafika.

Wazungu Wanayo historia yetu full ambayo sisi wenyewe tumeikana. Huwa nawaza pia pengine hata mambo yetu ya asili ambayo tumeyapa kisogo wazungu wametu hifadhia sehemu na IPO siku tutakuja kuinunua asili yetu Kwa bei mbaya sana.​
 
Walifanya vyema kuzuia huo upuuzi usirushwe hewani.
Lord...
Ungeweza kuyasema hayo uliyokusudia bila kutia tusi na ungeeleweka.
Hata wale ambao wananichukia hawajafikia kuniita ''mpuuzi.''

Nimezungumza na vyombo vingi vya habari vikubwa duniani:

1696966767953.png

BBC Dira ya Dunia

1696966864849.png

VoA Washington DC
1696967116359.png
Bwana Lord...
Naamini tumeelewana.
 
Tena bahati yako rais alikuwa JK muislam mwenzako,ingekuwa bwana John ungeozea jela na wale wapemba magaidi,tape hazikupotea,wanausalama walizichukua baada ya kuona hazina afya kwa usalama na mustakabali wa nchi,ulikuwa ni uchochezi
Sasa aljazeera wamekuja kumuhoji historia ya waisilam sasa unatukana nini kwani wakija bbc kuhoji historia ya anglikana au dw kuhoji historia ya kkkt hapa na harakati zao ungeongea hivyo..

Mambo mengine ni ya ajabu kabisa yaani unakasirika tu kwa sababu muisilamu kahojiwa mambo ya kiisilam..isee.
 
Mzeee wa hearsay za uislamu na Sykes family
Mpaji...
Wanasema hakuna mchango mkubwa nilioifanyia historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama kuandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Kuhusu Waislam wamenipa nishani mbili kwa mchango wangu katika historia ya Tanzania.

Kuhusu ''hearsay,'' soma hapo chini:

Father Smith of the Roman Catholic Church and the Party seem to be of the same mind on this dissension. [1]

Both Kiwanuka and Fr Smith are expressing their own personal opinion, not facts. No one denies the fact that some Christians were there.

Indeed Christian names appear in the dramatis personae of the play.
But no one can deny the truth that they did not occupy centre stage.

This work has given a descriptive analysis of the role of urban Muslims in the struggle for independence; their contribution in the founding of TANU; in membership drives and composition which took strong Muslim characteristics.

Dar es Salaam Province TANU Elders Council under its chairman Sheikh Suleiman Takadir had 173 members who were all Muslims. [2]
In response to Kiwanuka’s criticism the author published a short biography of Abdulwahid to commemorate 20 years of his death.[3]

This was followed by a memorial by the family in the Party and Government papers.[4]

This was not to pass without incident.

The editor of the Daily News, the government paper, rang up the family late in the night informing them that he would not publish Abdulwahid’s memorial the following day until he got permission from Party headquarters in Dodoma.

The reason given was that his life history touched important events and personalities in the history of the nation.

But somehow the memorial was published in both the Party and government dailies the following morning.

Two years earlier in 1986, after a silence of almost 25 years, Ally Sykes gave an interview to a British journalist, Paula Park.

Park wrote a full page article on the family’s political history. [5]

When the article was published Ally Sykes received telephone calls from both friends and business associates asking him if he was quoted correctly.

Shortly after, Park was quietly asked by immigration officials to leave the country.


[1] For the understanding of political parties and the role of culture, groupings, ideology, etc., see Maurice Duverger, Political Parties, Their Organisation and Activity in the Modern State, (New York, 1963).
[2] See Elder Council Section File 376, Party Archives, Dodoma.
[3] See M. Said, ‘Founder of a Political Movement: Abdulwahid K. Sykes 1924-1968’, Africa Events, London September, 1988, pp. 38-41.
[4] See Daily News, 23 rd October, 1988. Also Uhuru, 23 rd October, 1988.
[5]" ‘An Unsung Hero?’ Africa Events, London, November 1986 p.48.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes cha Kiingereza).

1696968349298.jpeg
 
Lord...
Ungeweza kuyasema hayo uliyokusudia bila kutia tusi na ungeeleweka.
Hata wale ambao wananichukia hawajafikia kuniita ''mpuuzi.''

Nimezungumza na vyombo vingi vya habari vikubwa duniani:

Bwana Lord...
Naamini tumeelewana.
Shikamoo Mzee Mohamed..

Ukubwa jalala.Shida ni moja JF imeingiliwa na watu wajinga wanaopaswa kushinda insta na wajinga wenzao.Badala ya kujifunza na kuelimika mtu anakuja na mihemuko ya ajabu ajabu, hakuna adabu, heshima Kwa wakubwa. Usife moyo msafara wa mamba na kenge ni wengi. Me binafsi najifunza Sana kutoka kwako,uandishi wako na umuhimu wa kutunza Yale niliyosimuliwa Kwa faida ya vizazi vijavyo. Wasamehe bure na usife moyo kuelimisha...🙏
 
Nilisubiri kwa muda mrefu kipindi kirushwe.

Hakikurushwa.
Taarifa ulizowapatia zilikuwa na mashaka sana. Wakaamua kujipa muda ili wafuatilie kivingine zisije zikawaondolea kuaminika.
Tape zao za vipindi vyote walivyofanya Tanzania Bara na Visiwani vilipotea hotelini Zanzibar.
Walikua wanaku hold tu wakati wanaendelea kufuatilia na kuhakiki simulizi zako.
Baada ya mwaka mmoja hivi Mohamed Vall na wenzake walirudi tena Tanzania na wakaja Tanga kwa mahojiano.

Sijui nini kilitokea safari hii.
Kipindi hakijaenda hewani hadi leo.
walishajiridhisha kwamba simulizi ulizo wasimulia hazikuwa credible. Uliwajibu na kuwasimulia mambo ambayo ulitamani yawe, badala ya kuwajibu au kuwasimulia ilivyokuwa.

Ila Hongera
 
Tena bahati yako rais alikuwa JK muislam mwenzako,ingekuwa bwana John ungeozea jela na wale wapemba magaidi,tape hazikupotea,wanausalama walizichukua baada ya kuona hazina afya kwa usalama na mustakabali wa nchi,ulikuwa ni uchochezi
Utakufa kwa kihoro cha chuki wewe. Jibu hoja kwa hoja sio dhihaka na kejeli.
 
Taarifa ulizowapatia zilikuwa na mashaka sana. Wakaamua kujipa muda ili wafuatilie kivingine zisije zikawaondolea kuaminika.

Walikua wanaku hold tu wakati wanaendelea kufuatilia na kuhakiki simulizi zako.

walishajiridhisha kwamba simulizi ulizo wasimulia hazikuwa credible. Uliwajibu na kuwasimulia mambo ambayo ulitamani yawe, badala ya kuwajibu au kuwasimulia ilivyokuwa.

Ila Hongera
Paki....
Umuhimu wa mchango wako ni kuwa unasoma ninayoandika.
 
Shikamoo Mzee Mohamed..
Ukubwa jalala.Shida ni moja JF imeingiliwa na watu wajinga wanaopaswa kushinda insta na wajinga wenzao.Badala ya kujifunza na kuelimika mtu anakuja na mihemuko ya ajabu ajabu,hakuna adabu,heshima Kwa wakubwa.Usife moyo msafara wa mamba na kenge ni wengi...Me binafsi najifunza Sana kutoka kwako,uandishi wako na umuhimu wa kutunza Yale niliyosimuliwa Kwa faida ya vizazi vijavyo.wasamehe bure na usife moyo kuelimisha...🙏
Red...
Marahaba.
Niko hapa kusomesha.
 
Mzee Mo
Nilisema...
Wewe na uliiuzunguka dunia na kurudi nyumbani na mafanikio....

Humu JF tuna idadi kubwa ya watu ambao wana maisha ya dhiki na njaa kali na husda, wanakimbizana na ratiba ya kwenda chooni
Na wale vijana waliobahatika kutoka na kung'gang'ania huko nje ni kwa kuoa vikongwe, kuosha wazee, na kuukana urijali kukubali kuolewa

Kwa hiyo kila uliweka historia na picha zako za maisha, hasa ya nchi ulivyopita sio kwa kudanga bali kikazi na pia elimu uliyopata isiyo ya kuungaunga kama zao, ni lazima wakutapikie na mapovu ya njaa na ufukara au msongo wa uhalisia ya maisha yao...wala hayahusiani na dini yako

Keep up the good work....
Take...
Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom