Wadau maisha ya mtanzania siku hadi siku yanazidi kuwa magumu,kwa upande wa Dar miongoni mwa mambo ambayo yanaendelea kututesa na kutupotezea muda mwingi barabarani ni foleni za magari, katika siku ambazo zimeniumiza mimi ni jana, nilikuwa nikitokea posta mpya kuelekea tandika nikiwa kwenye daladala, tulipofika kituo cha baharini mama mjamzito alipanda katika gari ambalo nilikuwepo,tulipovuka usawa wa mnazimoja basi likiwa limejaa sana mama yule ghafla alilia kwa uchungu, mwanamke mmoja aliyekuwa karibu naye alimuliza vipi akajibu naumwa dereva akaelezwa asimamishe gari, wakati anajaribu kupaki ili watafute taxi na watu wampishe ashuke yule mama akashindwa hata kusogeza mguu kilichofuata akakaa ktk ngazi ya mlangoni mara mtoto akalia wanawake walio kuwa karibu yake wakamsaidia kupokea mtoto watu wote wakiona ikawa shida watu kushuka, ikabidi dereva kuendesha gari mpaka hosp iliyokuwa jirani abiria tukiwepo, kweli sipendi kuendelea kwani inaumiza sana MUNGU ATUSAIDIE WATANZANIA, sasa kwa tukio la jana nikajiuliza vipi kuhusu zile bajaji zilizonunuliwa maalumu kwa wajawazito kuna sehemu ya nurse kukaa ikitokea dharura aweze kumsaidia mama? au zina ukubwa gani kumwezesha mama mjamzito kulala vizuri wakielekea hosp? nawasilisha