Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Umetumwa? Tumia kalamu yako kuikomboa nchi kutoka kwenye dhuluma na manyanyaso,na sio kujikomba ili kupata utakacho. Yaani siamini kama wewe ni mwandishi uliyehitimu. Kama ulisomea huo uandishi basi elimu yako haijakukomboa..
 
kama ilivyo kawaida humu jamvini idadi kubwa ya wachangiaji siku zote hawapendi mada yoyote ambayo wanadhani inasaidia kuitetea serikali lakini masauala ya ukweli lazima yaanikwe hadharani,katika madai kumi na mawili ya madaktari ni dai la kumi na moja pekee ndilo linaloeleza uboreshaji wa huduma za afya lakini mengine yote ni ubinafsi wa madaktari.


katika utekelezaji wa uboreshaji huo mimi katika hospitali ya wilayani kwangu serikali imejenga chumba cha upasuaji cha kisasa chenye vifaa vingi hivyo nakubaliana na kwamba kumekuwepo na jitihada za kuboresha huduma-roma haikujengwa siku moja.


dk ulimboka kasafirishwa kwenda afrika ya kusini kwa ndege ya kukodi achilia mbali gharama za matibabu hapo siyo michango tu kupitia katika sms lazima kuna nguvu iliyojificha nyuma ya pazia-serikali haziondolewi kwa mtindo huo.


Hivi madaktari na kitabu chote walichopiga wanakubali kurubuniwa n dk ulimboka ambaye si mfanyakazi mwenzao bali ni mtu wa ngo's wanaokula deal la kuhakikisha nchi inaingia machafukoni nao wakiona mambo mabaya wakodi ndege na kukimbia nchi


nimesoma makala haya na yamenikuna ingawa dada yangu happy kwa makala haya nategemea utashambuliwa sana lakini hawa watu kama mheshimiwa Godbless Lema ni wa kuwaambia tukiendelea kuwaita makamanda tutakuwa tunawatia ujinga:

· TUMECHOSHWA NA UKATILI WA MADAKTARI

Na Happiness Katabazi


JANUARI 30 mwaka huu, gazeti hili lilichapisha makala niliyokuwa nimeiandika mimi iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Ni mgomo wa madaktari kweli au?


Walivyogoma mara ya pili ulioanza Machi 7 mwaka huu, niliandika makala ndefu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Madaktari waungwana hawasifiwi ushenzi’.Haikuchapishwa na gazeti hili kwasababu ambazo sitazitaja adharani ila niliisambaza kwenye mitandao ya kijamii.


Na ndani ya makala hizo mengi niliyokuwa nimeyabashiri ndiyo sasa yameanza kujitokeza na tunayashudia.Lakini leo tena naandika makala ya tatu kuhusu mgomo huu wa tatu ulioanza wiki iliyopita naninasisitiza tena mgomo huo ni batili na umedharau amri ya Mahakama Kuu Disheni ya Kazi, ambayo wiki iliyopita ilitoa amri ya kutangaza mgomo huo kuwa ni haramu lakini cha kushangaza madaktari wetu ambao ni wasomi ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kukaidi amri hiyo halali ya mahakama na mhimili wa serikali kisheria ndiyo unatakiwa uhakikishe amri hiyo na nyingine za mahakama zinatekelezwa kwa vitendo na sivinginevyo umeshindwa kusaidia utekelezaji wa amri hiyo kwa kuwakamata madaktari hao waliokaidi amri ya mahakama na kuwafikisha mahakamani ili wajibu mashitaka ya ni kwanini wamekaidi amri ya mahakama.


Matokeo ya kushindwa kutekeleza amri hiyo ya mahakama ndiyo sasa kunasababisha maskini wenzetu ambao ni wagonjwa wanashindwa kutibiwa na wengine kudaiwa kupoteza maisha kwasababu ya madaktari hao ambao kwa makusudi wameamua kukaidi amri ya mahakama na serikali inaendelea kuwachekea.


Ibara ya 13 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema “ Watu wote ni sawa mbele ya sheria,na wanayo haki ,bila ya ubaguzi wowote,kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria’ .


Sasa kwa Ibara hiyo ya Katiba inaanza kuonekana sasa baadhi ya madaktari waliogoma wapo juu ya sheria kwani wanakataa kutekeleza amri ya mahakama na serikali inawaacha watu hao waendelee kudharau amri hiyo wakati siku zote inafahamika kuwa nchi yetu inaongozwa na misingi ya sheria.


Lakini ni serikali hii kupitia jeshi la polisi ndiyo imekuwa ikiakikisha amri mbalimbali zinazotolewa na mahakama zinatekelezwa kikamilifu lakini cha kushangaza serikali hii inashindwa kuwafikisha mahakamani madaktari hao wanaoikaidi amri hiyo jambo ambalo hivi sasa limeanza kutafsiriwa kuwa kada ya madaktari wapo juu ya sheria.


Nikiachana na hilo nivigeukie vyombo vyetu vya habari kuhusu ushiriki wao katika mgomo huu wa madaktari,kwa namna moja au nyingine vyombo vingi vya habari vimekuwa vikitoa nafasi kubwa kwa madaktari wanaogoma na kuinyima serikali na jamii inayopinga mgomo huo kusikika kupitia vyombo vya habari na baadhi ya wanahabari wakiwa ndani na nje ya vyombo vya habari wamekuwa wakisikika wakikerwa na tabia hiyo ya madaktari ila wanaogopa kuandika makala na habari za kuwakosoa madaktari kwasababu ya kuhofia eti siku wakiugua na kwenda hospitalini huko wanaweza kujikuta wakichomwa sindano za sumu na madaktari hao.


Hali iliyosababisha wananchi wengi katika mgomo wa kwanza na wa pili kuona madaktari wapo sahii na mgomo huu wa tatu kadri siku zinavyozidi kusonga mbele wananchi na baadhi waandishi wa chache wameanza kutowaunga mkono hadi kufikia kuwapachika majina mabaya madaktari hao kuwa wana roho za kikatili zaidi ya wa kikundi cha ‘Boko Haram’ .


Hii ni changamoto kwa sisi vyombo vya habari tujitazame upya na tuifanyie kazi.
Hakuna ubishi kwamba madaktari wanadai maslahi yao na serikali katika mgomo wa pili uliyatimiza baadhi ya madai na ukaidi kuendelea kuyafanyia kazi madai yaliyosalia na hakuna ubishi kwamba wanafanyakazi katika mazingira magumu na pia nao wagonjwa nao wakati mwingine hawapatiwi tiba za uhakika kutoka kwa madaktari.


Lakini cha kushangaza madaktari hawa wameonekana ni watu walafi na wabinafsi wanaotaka masulufi manono wapewe wao tu na kada nyingine zisipate,wameonekana kukosa subira,hawana imani na serikali yao ambayo ndiyo mwajiri wao na ndiyo anayewalipa mishahara na wengine walisomeshwa na serikali hiyo.


Kwa mtindo huu ni wazi kabisa hawa wanaonekana hawana dhamila ya dhati ya kuitumikia serikali kwa moyo wa uzalendo kwani wamedhiirisha wazi kuwa muhimu kwao ni fedha kuliko kuokoa maisha na kutibia wagonjwa ambao ndiyo hasa wanasababisha wao wapate mshahara,wasome.Hivi bila wagonjwa nyie madaktari mngekuwa na hiyo ajira ya udaktari?


Ni madaktari hawa hawa akiwemo huyo Dk.Steven Ulimboka wamekuwa wakiutangazia umma kuwa pale hospitali ya Muhimbili hakuna dawa wala vifaa, sasa mbona tumeshuhudia yeye Ulimboka ambaye amepigwa na watu wasiyojulikana akifikishwa hospitalini hapo na kulakiwa madaktari wenzake wakaanza kumtibia na jinsi gani walivyomakatili wakagoma kuwatibia wananchi wenzetu siku hiyo wakamkimbilia kumtibu Ulimboka kwa dawa na vifaa ambavyo vimenunuliwa kwa kodi zetu.


Ni madaktari hawa hawa wanaojigamba kuwa wao ni madaktari bingwa sasa mbona wameshindwa kumtibia mwenzao hadi wamempeleka nje ya nchi akatibiwe?
Tumesikia madaktari hawa ambao kila kukicha wanadai mishahara wanayolipwa ni midogo na mazingira ya kazi ni mabovu, tuwaulize hayo mamilioni waliyochanga ghafla ya kumsafirisha mwenzao wameyapata wapi? Kama wanauzalendo kweli wa hili ni kwanini hizo fedha walizozichangisha wangezitumia kununulia vifaa na kuviweka pale Muhimbili ili vije kumtibia mwenzao na watanzania wengine?


Imeelezwa kuwa safari ya Ulimboka kwenda nje imegubikwa na usiri mkubwa,hivi kama siyo upuuzi ni kitu gani?Mnaficha nini na mnamficha nani kwamba Ulimboka ameendakutibiwa nchi gani?


Hivi leo hii mtu anaweza kwenda nje ya nchi bila kukata tiketi ya ndege,visa ambazo zitaonyesha anakwenda nchi gani? Kama mnaisi serikali ndiyo imemfanyia unyama ule na mkaamua kumuondoa kwa siri pale Muhimbili, hivi kwa akili zenu mnafikiri huko mlikopo mpeleka kutibiwa ndiyon serikali ya Tanzania haipo?
Na kama mnafahamu serikali ndiyo imemtendea unyama huo pelekeni ushahidi mahakamani au pelekeni ombi mahakamani na kutaka muendeshe kesi binafsi(Private Prosecution).


Hivi kama sio uhuni na ukatili tunafanyiwa na hawa baadhi ya madaktari wa serikali ambao mishahara yao inatokana na kodi zetu nini na wakati huu wanagoma bado wanaendelea kupewa mishahara?


Na mbaya zaidi wananchi wanashindwa kuwachachamalia hawa madaktari lakini ingetokea vyama vya siasa vimeitisha maandano ya kupinga mfumuko wa bei,malipo ya Dowans ni sisi wananchi tungejitokeza kuundamana tena hata kama hayo maandamano ni haramu lakini hili la madaktari kuendesha mgomo haramu ambao wananchi wenzetu wanaumia na kupoteza maisha wala hatuonekani kabisa kulichukulia uzito wa aina yake.Sisi ni watu wa ajabu sana.Tumekuwa na kasumba ya kushabia mambo yasiyo na msingi ila mambo ya msingi ambayo yanatuhusu moja kwa moja hatuyatilii maanani.


Rai yangu kwa madaktari wanaogoma, kama wanaona serikali haiwalipi vizuri siwaache hiyo kazi wakatafute kazi sehemu nyingine ambapo watalipwa mishahara minono?Kwanini muundelee kumng’ang’ania bwana(serikali) ambayo kwa akili zenu mnaona haiwajali na haiwapendi?


Tanzania bado ina ardhi kubwa ambayo imegunduliwa kuwa ina madini, simuende basi kwenye ardhi hizo mkachimbe madini ili muwe na mahela mengi kama mnavyotaka kuliko kung’ang’ania kazi serikali ambayo nyie mnadai hamlipwi vizuri?Kwani mmekatazwa.


Maana ninachokiona mimi hivi sasa hawa wanaogoma ni watu ambao kwa akili zao timamu wameamua kukiuka viapo vyao, wameichoka kazi ya kuwatibu wa gonjwa kwa kisingizio cha kudai maslahi manono,daktari mwenzao Ulimboka kafanyiwa ukatili.Sasa kama kafanyiwa ukatili na watu wasiyojulikana ni kwanini sasa mgomee amri ya mahakama,agizo la serikali la kuwataka mrejee kazini na mgome kuwatibu wagonjwa?Kwani ndiyo waliomfanyia ukatili huo?


Mkae mkijua hizo roho za wananchi wenzetu zinazopotea kwaajili ya mgomo wenu ipo siku mtadaiwa na mungu na mathara yake mtayapata hapa hapa duniani kwani mungu amewapa vipawa mje mvitumie duniani kwaajili ya kuwahudumia watu wake,sasa nyie mnapingana na agizo la mungu na maadili ya taaluma yenu, minaamini ipo siku mungu atawaadhibu na msije kulia na mtu.


Mwisho ni malizie kwa kuwataka wanaharakati na wale vyama vya siasa akiwemo Kada ya Chadema, Godbles Lema ambao wametoa matamko ya kulaani kitendo alichofanyiwa Ulimboka na Lema akasema akifa Ulimboka atalala barabarani, nawataka wageuze upande wa pili wa shilingi na waone kuwa kuna mamia ya wagonjwa wanakosa huduma na kupoteza maisha yao kwaajili ya mgomo huo haramu,mbona makundi hayo hatusikii yakitoa tamko ya kuwasema wananchi hao na kulaani mgomo huo haramu wa kisheria ambao mahakama ilisema mgomo huo ni batili?.


Wewe Lema unayesema utalala barabarani Ulimboka akifa, tumuulize huyu Lema ni kwanini alishindwa kulala barabarani siku ile Jaji Gabriel Rwakibalila wa Mahakama Kuu Kanda ua Arusha alipotoa hukumu dhidi yake ambapo alimvua ubunge na kumfungia kugombea ubunge baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kutoa lugha chafu?


Maana hukumu hiyo ndiyo imemfanya Lema hivi sasa awe kaka sisi tusiowabunge kwani analifuatilia bunge kupitia redio na televisheni, hapati tena posho na mshahara na hapewi heshima na stahili za kibunge tena,sasa tumuulize sasa alishindwa kulala barabarani kwa hukumu hiyo iliyokuwa ikumuhusu na imemwathiri yeye binafsi ndiyo leo hii atakuwa na ujasiri wa kufanya hivyo kwa Ulimboka ambaye hawana hata undugu?


Nimalizie kwa kuwataadhalisha madaktari wetu kuwa huo mgomo haramu wanaoufanya ipo siku watakuja kutokea baadhi ya ndugu wa wagonjwa watakaofika mahospitalini hapo halafu mkatae kuwapa huduma watajiuliza maswali yafuatayo;


Hivi hospitali hizo ni za serikali?Dawa na vifaa vya mahospitalini humo sizimenunuliwa kwa kodi za wananchi?Madaktari siwamesomeshwa kwa kodi za wananchi?


Wakimaliza kujiuliza maswali hayo watamalizia kwa kuwadhuru na wala msije kulia na mtu kwani sikila mtu anaweza kuvumilia huo uhuni na ukatili mnaotufanyia.


Mungu ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika


0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com


Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Julai 3 mwaka 2012.

...Umetumwa? Tumia kalamu yako kuikomboa nchi kutoka kwenye dhuluma na manyanyaso,na sio kujikomba ili kupata utakacho. Yaani siamini kama wewe ni mwandishi uliyehitimu. Kama ulisomea huo uandishi basi elimu yako haijakukomboa..
 
madaktari mmechemshaaaaaaaaaa, tena serikali naomba wawafanye kitu mbaya ikiwemo kufukuza kazi wale wote watakao shiriki mgomo

Najua hapo ndio mwisho wako wa kufikiria umefika mwisho, nenda shule angalau ufike hata form two utabadilika
 
Nimeisoma hii na sikuamini kuwa ni huyu Bi Mdogo kaandika haya. Baada ya kusoma hii makala, nimeona ndani yake hisia kama zile zinazotolewa na wabunge wa CCM wakiwa bungeni. Nimeona vijembe na mipasho mingi iliyozungushiwa na habari yenyewe. Mipasho na vijembe hivyo, vimepunguza hadhi na mantiki ya makala haya. Uandishi wa namna hii unamharibia sifa mwandishi na hata gazeti ambalo habari hizo huchapishwa.
 
Najua hapo ndio mwisho wako wa kufikiria umefika mwisho, nenda shule angalau ufike hata form two utabadilika

usimdhihaki mtu usie mjua,uko huru kutoa mawazo yako(thus why most of us we are great thinkers) pia wakati unamnyooshea mtu kidole ww vidole vinne vina kupoint.watch out
 
Achilia mbali kutekwa ingekuwa mwanaasha ameibiwa mdoli (toy) tu ungeona utendaji wa jeshi la polisi uliotukuka.

Ndugu uyasemayo ni kweli,

Kuna siku kuliibiwa ngombe huko home kwa J.K Bagamoyo; yaani nilishuhudia mwenyewe Live bila chenga, defender nyingi toka mkoa wa DSM, zilihamia huko kuwatafuta hao ng'ombe wa mheshimiwa. Na pia tulidodoswa kuwa pamoja na magari na askari wa miguu kutapakaa mitaani na vichakani huko Bagamoyo pia kulikuwa na Helkopta za Polisi zinatafuta kwa juu mji wa bagamoyo.

Yaani pale kwa kuwa ilimgusa mheshimiwa kweli Polisi walipatikana kufanya ile kazi, lakini wewe mlalahoi na mlipa kodi toa taarifa kama Polisi wakifika basi ni baada ya tukio kutafuta ushahidi umeibiwa nini ili wakagawane.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Katabazi is cursed !! wameenda kumtibu nje kwasababu hakuna vifaa. wewe unataka wanunue vifaaa waweke mhuhimbili waanzae kumtibu. havi unajua maana ya kidney failure? au unafikiri hivyo vifaa vinanunuliwa kariakoo? kununua na kuvileta tz zeti si chini ya miezi 2 sasa huyo mgonjwa atakuwapo? usiongee pumba humu. think before you waste your time to write stupidity!! kalye mpale..!!!!!!!!:A S-baby:
 
Najua hapo ndio mwisho wako wa kufikiria umefika mwisho, nenda shule angalau ufike hata form two utabadilika

kingine rafiki, mm na wengi tunaokataa mgomo wa madaktari ni kwa sbb ya kuuona ni wa kimaslahi zaid na pia unaaumiza watanzania wenzetu wa kipato cha kawaida sana ambao hawawezi kwenda hosp nyingine zaid ya hosp ya serikali without or with less money charged to them otherwise they will not afford,they will staying at home while they are sick.

ktk maisha usitake mawazo yako ndio yakubalike tu na wakati huna ushawishi then ukaishia matusi hapo hukuonesha jinsi ulivyo hata bila kukuona. na pia wakati mwingine usikubali kushawishika kwa kitu kusikia juu fanya jitihada kujua atleast undani wa kitu then changia
pia jua kuna makazi ukikaa hapa duniani au ukazungukwa na watu wa carribre fulani NI ELIMU TOSHA tena kibongo bongo ni form SIX na ww ukawa na hata masters mkikaa pamoja ww mwenyewe unajiona elimu yako bado, tena hizi elimu zenu za bongo ukimaliza tu ndio hata ku-peruse vitabu, magazet hamtaki ndio kabisa unakua kilaza zaid ya yote ww unaonekana unafikiria kama DR. Didas masaburi
 
lakini masauala ya ukweli lazima yaanikwe hadharani,katika madai kumi na mawili ya madaktari ni dai la kumi na moja pekee ndilo linaloeleza uboreshaji wa huduma za afya lakini mengine yote ni ubinafsi wa madaktari.


katika utekelezaji wa uboreshaji huo mimi katika hospitali ya wilayani kwangu serikali imejenga chumba cha upasuaji cha kisasa chenye vifaa vingi hivyo nakubaliana na kwamba kumekuwepo na jitihada za kuboresha huduma-roma haikujengwa siku moja.

View attachment 57961

Akina mama Hospitali.jpg

dk ulimboka kasafirishwa kwenda afrika ya kusini kwa ndege ya kukodi achilia mbali gharama za matibabu hapo siyo michango tu kupitia katika sms lazima kuna nguvu iliyojificha nyuma ya pazia-serikali haziondolewi kwa mtindo huo.

Hivyo ulitegemea kuwa Serikali inayotuhumiwa kukusudia kumuua je ingeweza kumpeleka kwa matibabu, na pia kama waliweza kumuweka Bunju Police Post kwa masaa kadhaa wakitegemea atakufa pale!!!!! TAFAKARI KABLA YA KUSEMA.

Hivi madaktari na kitabu chote walichopiga wanakubali kurubuniwa n dk ulimboka ambaye si mfanyakazi mwenzao bali ni mtu wa ngo's wanaokula deal la kuhakikisha nchi inaingia machafukoni nao wakiona mambo mabaya wakodi ndege na kukimbia nchi

Kama ni machafuko yatasababihwa na viongozi wa Serikali, na hawachoki kuvitaja vyama vya upinzani ili kuficha ukweli katika vitendo vyao.

nimesoma makala haya na yamenikuna ingawa dada yangu happy kwa makala haya nategemea utashambuliwa sana lakini hawa watu kama mheshimiwa Godbless Lema ni wa kuwaambia tukiendelea kuwaita makamanda tutakuwa tunawatia ujinga:

Kwa utumbo huu mimi binafsi simuungi mkono, na kumbe ndio maana hata Mhariri alikataa kuchapisha makala yake, kwa sababu aliiona haina maana na ujinga tu kuiweka katika gazeti lake. Makala kama hiyo angeliipeleka gazeti la UHURU na siyo gazeti RAI ambalo ni makini nahabari zake. SIKU NYINGINE apeLEKEE UHURU itachapishwa.

Kama una mawasiliano naye huyu Happiness mshauri kuwa asione Watanzania wapo kimya akadhani ni kobe.


MIZAMBWA
NABII MTARAJWIA!!!
 
Wewe Lema unayesema utalala barabarani Ulimboka akifa, tumuulize huyu Lema ni kwanini alishindwa kulala barabarani siku ile Jaji Gabriel Rwakibalila wa Mahakama Kuu Kanda ua Arusha alipotoa hukumu dhidi yake ambapo alimvua ubunge na kumfungia kugombea ubunge baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kutoa lugha chafu?


Maana hukumu hiyo ndiyo imemfanya Lema hivi sasa awe kaka sisi tusiowabunge kwani analifuatilia bunge kupitia redio na televisheni, hapati tena posho na mshahara na hapewi heshima na stahili za kibunge tena,sasa tumuulize sasa alishindwa kulala barabarani kwa hukumu hiyo iliyokuwa ikumuhusu na imemwathiri yeye binafsi ndiyo leo hii atakuwa na ujasiri wa kufanya hivyo kwa Ulimboka ambaye hawana hata undugu?
happ katabazi huna akili.....mhaya gani wewe huna akili......hayo maandishi ni ***** utumbo kabisa....naona aibu kwa mumeo aiseeeee...mke gani wewe???
 
Back
Top Bottom