Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

ngoja atumike kama kondomu tu na nafasi ya kugombea ndani ya chama cha magamba hapati. labda arudi kwenye chama chake cha CCJ
 
Hata ubunge asahau.Nina mpango wa kutangaza nia.Wazee wameisha ahidi kunichukulia form.
 
kuhusu sita wala hata msitie shaka huyu hatuwezi kumpa hata nafasi ya kuingia kwenye raundi, anapewa promo na chama kwasabab ya kuisakama CDM hana la ziada ni mtu wa fitna na kujikomba waliokaribu wanajua
 
Ni wazi bwana Sitta alitaka na anataka kuutumia mchakato wa katiba kujijengea umaarufu na apate upenyo wa kuingia ikulu kupitia ajenda kwamba ameleta katiba mpya hivyo apewe muda wa kuitekeleza kwa kasi ileile.k

Kambi pinzani zikausoma mchezo na kazi ikawa moja,kuutumia mchakato kumuelekeza kibra na hata magazeti na mitandao ya kijamii kumchakaza

Hakika amechakaa na anahitaji total overhaul kumsafisha na muda umekwisha,haaminiki CCM kwa sababu FAHIM DOVUTWA alisema kwamba SITTA alikuwa na mawasiliano na UKAWA ili aupate uenyekiti.

CCM haaminiki kwa hoja ya CCJ,siasa kweli haina fomula.
 
huyu mzee anastahili kupelekwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya bmk na kodi za watanzania yaliyomkuta mramba na daniel yona yamwandame na yeye.
 
Mzee wa viwango yamempata kama yaliyompata Ekerege aliyekuwa mkurugenzi wa viwango TBS.
Huyu jamaa hafai kabisa mkimpa urais hatafanya cha maana zaidi ya kulipiza kisasi huyu muogopeni kuliko ukoma, yaani anataka kupata kura kwa kujipendekeza kwa wajumbe wa ccm kwa kutengeneza katiba ya wanasiasa huku akiwasaliti wananchi ambao ndiyo wapiga kura! Huyu siyo mtu, ana uchu wa madaraka ili alipize kisasi wale waliomuenguaga uspika, wananchi hana habari nao, eti alisema vyombo vya habari vishughulikiwe, hatufai huyu mtu.
 
Samwel Sitta amevikwa taji la miba na wapambe wake,mwenyewe akijua amependeza Kumbe anaaibika.
 
Halafu amekuwa mkali kama pilipili, naona anawafokea wajumbe wa bunge la katiba
 
Angalia jinsi anavyoliburuza bunge maalum la katiba.

Kwanza ameruhusu rasimu ya CCM kuingizwa kwenye bunge analoliongoza yeye na kutupilia mbali rasimu ya Warioba ambayo ndiyo rasimu ya wananchi-huu ni ujambazi Mkubwa Wa Kisiasa dhidi ya demokrasia.

Pili ameongoza ukiukwaji Mkubwa Wa demokrasia wa kutojali maoni ya wajumbe wa kutoka vyama vya upinzani wakiwakilisha maoni ya watanzania wengi wenye maoni tofauti Na Chama tawala hata kama hawa wajumbe ki-idadi ni wachache.

Tatu ni wazi kwamba huu mchakato wa kupata katiba mpya hauwezi kukamilika kabla ya 2015 hata Kama bunge hilo lisipoahirishwa Na kuendeshwa usiku na mcchana. Kwa ubinafsi wake ili apate milioni zake 150, analiburuza bunge la katiba bila kujali kuteketea kwa pesa zetu za kodi.-

Mwisho kana kwamba hayo hayatoshi, sasa anataka wajumbe wapige kura hata kama wako hija au wamelazwa hospitalini! Maajabu ya musa.

Kwa hayo tu niliyoyataja Hapo juu yanamfanya bwana Sitta akose kabisa sifa za kugombea urais.

NB: Niliwahi kufikiria 2015 Sitta angeweza kuwa mgombea mwenye unafuu ndani ya CCM lakini kwa huu utapeli wa Kisiasa hafai kabisa kuwa rais, pamoja na mambo yake ya kigeugeu.
 
Kama hiyo ilikuwa ni ndoto basi muombe mungu hasikupe NDOTO ZA NAMNA HII TENA. NI NUKSI.
 
Back
Top Bottom