Kutoka kiongozi wa mhimili wa pili wa dola (bunge) hadi kuongoza wizara isiyojulikana ya Afrika Mashariki naweza kusema isiyo na hadhi kwake kwa vile huwezi kuilinganisha na wizara kama ya Katiba na Sheria.
Sitta amepewa nafasi hiyo ili kumpoza kutokana na machungu aliyopata baada ya jina lake kukatwa kwa makusudi kwenye kinyang'anyiro cha uspika kwa madai kwamba safari hii ni zamu ya wanawake kuongoza mhimili huo wa dola.
Sitta amewekwa hapo kama pazia kwa nia ya kumfunga mdomo ili asitumie nafasi yake kama mbunge huru kuichachafya serikali kama alivyokuwa akiruhusu mijadala ya aina hiyo wakati alipokuwa spika katika Bunge lililopita.
SS ajifunze kwa waliomtangulia kuongoza wizara hiyo kama Dk. Ibrahim Msabaha na Deodorous Kamala kuwa hawakusikika na mwisho wa siku si kuwa walianguka kisiasa tu bali walishindwa kwenye majimbo yao pia.
Nampa miaka miwili tutakuwa tumemsahau kwenye nyanja za siasa.
Kutoka kiongozi wa mhimili wa pili wa dola (bunge) hadi kuongoza wizara isiyojulikana ya Afrika Mashariki naweza kusema isiyo na hadhi kwake kwa vile huwezi kuilinganisha na wizara kama ya Katiba na Sheria.
Sitta amepewa nafasi hiyo ili kumpoza kutokana na machungu aliyopata baada ya jina lake kukatwa kwa makusudi kwenye kinyanganyiro cha uspika kwa madai kwamba safari hii ni zamu ya wanawake kuongoza mhimili huo wa dola.
Sitta amewekwa hapo kama pazia kwa nia ya kumfunga mdomo ili asitumie nafasi yake kama mbunge huru kuichachafya serikali kama alivyokuwa akiruhusu mijadala ya aina hiyo wakati alipokuwa spika katika Bunge lililopita.
SS ajifunze kwa waliomtangulia kuongoza wizara hiyo kama Dk. Ibrahim Msabaha na Deodorous Kamala kuwa hawakusikika na mwisho wa siku si kuwa walianguka kisiasa tu bali walishindwa kwenye majimbo yao pia.
Nampa miaka miwili tutakuwa tumemsahau kwenye nyanja za siasa.
Chatu kamfuga mbwa mpenda ubwabwa, na kamnasa kwa kutumia mdomo wake unaonukia ubwabwa!!Chatu kafuga mbwa?? Au mbwa kafuga chatu?
Nanukuu .....
"Hata hivyo, wiki hii Sitta alifafanua kwamba kuenguliwa kwake katika uspika kutamfanya awashe moto zaidi kwa uhuru kwa mafisadi, kwani anayo tiketi ya uwakilishi ya wananchi wa Urambo Mashariki.
Akizungumza na Mwananchi wiki hii Sitta alisema 'Sita ni yule yule' na kwamba wanaodhani kuwa mbunge wa kawaida kutampunguzia nguvu kusimamia anayoamini ni makosa makubwa.
Sitta alisema kuanzia Bunge la Februari atawasha moto pale itakapostahili na kwamba ataendeleza misingi aliyoacha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ya kupambana na rushwa na ubabaishaji wa aina yoyote.
Alisisitiza kuwa hataruhusu ubabaishaji wala ufisadi kwani vinaondoa thamani ya utu wa mtanzania wa kawaida na kumkosesha haki zake za kufaidi raslimali za nchi."
TUNASUBIRI TUONE KAMA SIX ATAKWENDA SAWIA NA KAULI ZAKE AU ATAGEUKA JIWE!
Ukiwa mchapa kazi utang'ara kwenye kazi yoyote utakayopewa. Mrema, alisha prove hivyo, kwani hata walipompeleka kwenye wizara ambayo ilionekana kama wana mmaliza kisiasa, bado alipata kazi za kufanya na aka nga'ra. Hivyo hivyo Magufuli.
Huenda ni wakati muafaka kwa mheshimiwa Sitta ku prove beyond reasonable doubt kwamba yeye ni mchapa kazi kweli kweli na sio opportunist aliyetumia nafasi ya uspika kujikweza.
Huko EA kuna changamoto nyingi sana ambazo zinaenda na maslahi ya taifa. Atusaidie mikataba ya EA iwe yenye manufaa kwa Tanzania.