Sitta awashukia maadui wake: Amwita mmoja "Mhalifu sugu"!

Mkuu kama huna data si uache kuanzisha thread tu.....? vinginevyo uwataje hao wanaomchafua spika kama heading yako inavyoonyesha...sio kutupa kazi ya kukuletea umbea hapa mkuu!
 
Sitta ni mwanasiasa mzuri sana, ambaye kwa level ya watanzania wengi wetu tunaingia kwenye mtego wake kwa kuamini kuwa anaonewa/anawindwa na the so called mafisadi, what is doing is just trying to pre-empty tuhuma endapo zikielekezwa kwake watu waone si za kweli, lakini jiulizeni au waulizeni watu ambao walishafanya nae kazi kuanzia akiwa waziri enzi za Mwl - Mwinyi - Mkapa hapa tena ndo ilikuwa balaa akiwa TIC, this guy is not clean at all....hawa leo anaowaita ni wahalifu ndo walikuwa best friends wake, kwa mimi nachokiona hapa ni hasira tu kuukosa uwaziri mkuu...kama anachosema ni kweli maisha yake yako hatarini aweke ushahidi hadharani na awataje kwa majina. sitta kwanza alikuwa mbunge pekee wa urambo kwa miaka 15, wanachi baada ya kuona hafanyi lolote wakamfuata Prof. Kapuya ili akagombee, kwa kuwa hawa wawili wanafahamiana Prof. akamueleza kuhisi nia yake hiyo huyu alivyokuwa mjanja na wakati akiwa waziri wa sheria akapendekaeza jimbo lile ligawanywe mashariki na Magharibi,lakini pamoja mbinu zote hizo akandoka mtu mzima kwenye uchaguzi wa 1995, tokea hapo akatengeneza uadui na Kapuya kwa kudai yeye ndo aliyemuaribia kule kwao, pamoja na kuupata tena ubunge lakini hawa jamaa ni paka na chui mpaka sasa, ingawa hawa wote financier wao RA, ukitaka kuona ubaya wa huyu bwana aliweza hata kupandikiza mgombea wa upinzani kwenye jimbo la mwenzie ili amuangushe.
EMBU TUJIULIZE, KWANINI ALIOMBA APEWE ULINZI NDANI YA BUNGE??...
 
Kumekuwa na jitihada za makusudi kutaka kuwasafisha MAFISADI na inongezeka kadiri tunavyoelekea 2010.

Hata kama haya unayodai juu 6 yakiwa kweli, haiondoi ukweli kwamba wale anowatuhumu ni MAFISADI na waliibia taifa muda mrefu.
 
hivi huyu sitta yuko sawa kweli kichwani.anongea ongea nini kwenye magazeti.huyu si ndio alisema mawaziri wawe na ngozi ngumu kuhimili mikwaruzo au nakosea jamani
 
Ulichosema kimo ktk hilo gazeti la Raia Mwema la leo
 
hivi huyu sitta yuko sawa kweli kichwani.anongea ongea nini kwenye magazeti.huyu si ndio alisema mawaziri wawe na ngozi ngumu kuhimili mikwaruzo au nakosea jamani
na hiyo migozi yao migumu ndio inayotutesa maana wao wanadundana lakini hawasikii maumivu lakini sie ainya nyasi ndio tunaoumia
 
kwa kweli migozi yao migumu kama kenge....kwa kweli nimecheka sana .asante mkuu
 
Nadhani, twende kwenye uchaguzi mkuu mapema tu ili tukate huu mzizi wa kizabizabina.

hapo ndo penyewe mkuu...maneno ya Dr.Slaa yananitia moyo sana,anataka rais avunje serikali twende kwenye uchaguzi.Kwa mtazamo wangu nadiriki kusema serikali ya JK imepoteza mvuto na muelekeo haina kabisaaaaaa.Nhoja nitafute kadi yangu ya kupigia kura mapemaaa
 
...... kwa mimi nachokiona hapa ni hasira tu kuukosa uwaziri mkuu...kama anachosema ni kweli maisha yake yako hatarini aweke ushahidi hadharani na awataje kwa majina..... ingawa hawa wote financier wao RA, ukitaka kuona ubaya wa huyu bwana aliweza hata kupandikiza mgombea wa upinzani kwenye jimbo la mwenzie ili amuangushe.
EMBU TUJIULIZE, KWANINI ALIOMBA APEWE ULINZI NDANI YA BUNGE??...

Umeeleza vizuri, lakini naona nawe kama unataka kutoonyesha kuwa kina RA na genge lao wanaonewa bure kwa kuwa wali-influence JK kumnyima u-PM bwana Six. Inaelekea mwenzetu unashiba vizuri!
 
Umegonga IKULU mkuu. Wapo sawa kabisa, kulialia kama mademu(sorry wa beijing:
icon7.gif
!

acheni upumbafu sitta anamuongelea Rostam Aziz
 
Rostam Aziz ndo ana issue ya tender ya mahindi ambayo hakutimiza kama walivyo kubaliana na serikali.
 
Sitta ni mwanasiasa mzuri sana, ambaye kwa level ya watanzania wengi wetu tunaingia kwenye mtego wake kwa kuamini kuwa anaonewa/anawindwa na the so called mafisadi, what is doing is just trying to pre-empty tuhuma endapo zikielekezwa kwake watu waone si za kweli, lakini jiulizeni au waulizeni watu ambao walishafanya nae kazi kuanzia akiwa waziri enzi za Mwl - Mwinyi - Mkapa hapa tena ndo ilikuwa balaa akiwa TIC, this guy is not clean at all....hawa leo anaowaita ni wahalifu ndo walikuwa best friends wake, kwa mimi nachokiona hapa ni hasira tu kuukosa uwaziri mkuu...kama anachosema ni kweli maisha yake yako hatarini aweke ushahidi hadharani na awataje kwa majina. sitta kwanza alikuwa mbunge pekee wa urambo kwa miaka 15, wanachi baada ya kuona hafanyi lolote wakamfuata Prof. Kapuya ili akagombee, kwa kuwa hawa wawili wanafahamiana Prof. akamueleza kuhisi nia yake hiyo huyu alivyokuwa mjanja na wakati akiwa waziri wa sheria akapendekaeza jimbo lile ligawanywe mashariki na Magharibi,lakini pamoja mbinu zote hizo akandoka mtu mzima kwenye uchaguzi wa 1995, tokea hapo akatengeneza uadui na Kapuya kwa kudai yeye ndo aliyemuaribia kule kwao, pamoja na kuupata tena ubunge lakini hawa jamaa ni paka na chui mpaka sasa, ingawa hawa wote financier wao RA, ukitaka kuona ubaya wa huyu bwana aliweza hata kupandikiza mgombea wa upinzani kwenye jimbo la mwenzie ili amuangushe.
EMBU TUJIULIZE, KWANINI ALIOMBA APEWE ULINZI NDANI YA BUNGE??...

Ushahidi kwa serikali ipi? Mbona vinasa sauti alivyovikamata Dr. Slaa mpaka kesho hakuna taarifa? Wewe hizo za sitta kupandikiza mpinzani una ushahidi? Acha ufala bwana!!agh.....!
 
Pamoja na vitisho vyote hivi (kama ni vya kweli) Rais wa nchi yupo KIMYAA! hata kutoa neno kuhusiana na tuhuma hizi nzito zinazotolewa na Sitta halafu bila hata aibu ataomba tena achaguliwe 2010! Bora ujiuzulu Kikwete nchi imekushinda kabisa
 
Sitta aanika majeruhi kashfa ya Richmond

Mwandishi Wetu
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo
Agosti 5, 2009
rC.jpg

bul2.gif
Hosea naye aligeuzia Bunge kibao

bul2.gif
Achunguza kamati za Shelukindo, Dk. Slaa, Zitto

SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, ameanika siri ya yeye kuandamwa akisema wanaomuandama wengi ni katika kundi la majeruhi wa tuhuma za ufisadi, hususan za kuhusiana na mradi wa umeme wa dharura uliokabidhiwa kampuni tata ya Richmond Development LLC.
Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema kwa njia ya simu kutokea jimboni kwake Urambo Mashariki, mkoani Tabora, mwabzoni mwa wiki hii, Sitta alisema anaamini maadui zake kisiasa ndio wanaopandikiza tuhuma hizo ili ionekane mbele ya umma kuwa yeye ni kiongozi asiyefaa.
Katika hali inayodhihirisha kuwarushia kijembe baadhi ya wanasiasa wenzake, Sitta alisema watu wanaomuandama ni majeruhi wa msimamo mkali wa Bunge katika kupinga ufisadi akilenga moja kwa moja hasa kundi aliloliita kuwa ni 'genge' lililohusika na kampuni hewa ya Richmond.
Akijikita katika kuwaelezea watu hao, Sitta alisema: "Katika genge hili kuna watu watatu vinara. Wa kwanza ni mwanasiasa. Huyu kwa lugha ya kipolisi ni mhalifu sugu; amehusika katika uchotaji wa mabilioni kinyemela katika Commodity Import Support (CIS); amechota mabilioni kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT); na aliwahi nadhani mwaka 2004 kupewa tenda ya kuingiza mahindi kutoka nje ya nchi, na akapewa malipo ya awali na hakufanya kama ilivyotakiwa. Ni mhalifu sugu.
"Wa pili ni mwanasiasa ambaye amejipatia utajiri wa kupindukia katika hali ya maswali, yupo mwingine anajiita mfanyabiashara naye ameingia katika mkondo huo. Na kwa vigezo vya Tanzania hawa ni mabilionea.
"Tatizo hawa ni viongozi na wana-influence (nguvu kubwa ya ushawishi) na uhusiano mzuri na viongozi wengine wa kitaifa. Wamejenga mitandao ya kuiibia nchi, na wanafanikisha kazi hiyo kwa kutumia influence ya kisiasa na uhusiano kati yao na viongozi wa juu kutisha watendaji waaminifu serikalini.
"Kwa mfano, Richmond ambao ndiyo Dowans, walinunua mitambo mitatu, kwa Dola za Marekani milioni 30, wakapewa barua ya dhamana (letter of credit) na CRDB inayozidi dola milioni 30. Baadaye wakataka kuiuzia serikali mitambo hiyo kwa bilioni 69. Bunge tulitafiti bei hiyo kwa kuuliza inakouzwa na tukaambiwa mitambo mipya ni kati ya bilioni 25 na 30 na bei inaweza kupunguzwa. Tukazuia, wakachukia.
"Sasa watendaji dhaifu wamekuwa wakiwaogopa na hivyo kujikuta wakivunja sheria ili kuwaridhisha. Wamewekeza majengo katika mji wa Dubai, Afrika Kusini na Uingereza. Kinachotokea ni kwamba Bunge sasa linawanyima usingizi, linatibua mitandao yao ya wizi na ulaji, kwa hiyo lazima wawe na hasira.
"Bahati mbaya kwao, wamefuatilia rekodi yangu kiutendaji hawajakuta makosa yoyote na hivyo wamekosa pa kunibana nikiwa kama kiongozi wa Bunge linalowanyima usingizi. Wamegundua track record (utendaji kazi ) yangu ni excellent (nzuri sana). Nimekuwa Waziri wa Ujenzi na kufanikisha miradi mikubwa kama Kiwanja cha Ndege Dar es Salaam, ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma, ujenzi wa Daraja la Salender, Dar es Salaam (mwaka 1980), ujenzi wa barabara ya Makambako-Songea (1983).
"Nimesimamia ujenzi wa nyumba 252 kwa fedha za mkopo kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC) na NPF (sasa NSSF). Mwaka 1988 nimekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, 1990 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mwaka 1993 hadi 1995 nimekuwa Waziri wa Sheria na Katiba, 1996 hadi 2005 nimekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kote huko hakuna ufisadi hata wa senti moja. Track record yangu ni uadilifu mtupu, wamekosa kwa kunikamata, wanahangaika sasa kupotosha ukweli," alisema Sitta.
Akijibu tuhuma zinazomhusisha kutaka gari la thamani kubwa na nyumba ya kifahari, alisema angetamani atumie usafiri hata wa 'Suzuki Vitara' lakini yeye si mwamuzi, bali jukumu hilo ni la vyombo vya usalama vinavyoamua gari gani linunuliwe ili kukidhi vigezo vyao vya ulinzi wa viongozi wa kitaifa dhidi ya changamoto za kisasa za uhalifu.
Amesema yapo magari yasiyopenyeza risasi yanayotumiwa na viongozi ambayo yamenunuliwa kwa Sh bilioni 1.2, na mwamuzi si "anayeendeshwa" bali ni vyombo vya Usalama wa Taifa, ambavyo ni lazima vifanye kazi kwa ufanisi wakati wote.
Kuhusu suala la nyumba, alisema amekuwa akiishi katika ambayo ilikimbiwa na Naibu Waziri, Dk. Makongoro Mahanga, kutokana na nyumba hiyo kuwa na mfumo wa majitaka unaopumulia ndani, na nyumba hiyo ilikuwa katika eneo la makazi ya mawaziri, jijini Dar es Salaam.
Amesema ameishi katika nyumba hiyo kwa takriban miaka minne, na baada ya Rais Jakaya Kikwete kupata taarifa hizo aliagiza ahamishwe na atafutiwe nyumba yenye hadhi yake kama kiongozi wa mhimili wa taifa (Bunge).
Aliongeza Sitta katika majibu yake kuhusu masuala hayo matatu:
"Tuanze kuzungumzia hoja ya ununuzi wa gari. Eti Spika nataka gari la kifahari. Sihusiki kabisa katika utaratibu wa kununua magari ya viongozi wa kitaifa. Nchi inaendeshwa kwa taratibu maalumu si ovyo ovyo namna hiyo, kwamba viongozi wa kitaifa wanalala na kuamkia asubuhi na kuagiza nunua gari jipya.

"Utaratibu ni kwamba kwa viongozi wa kitaifa kama Spika na wengine, anayehusika katika ununuzi wa magari ni Katibu Mkuu Kiongozi, ambaye naye anazingatia maoni ya Usalama wa Taifa katika kufikia uamuzi.
"Sasa utashi wangu kama kiongozi unaweza kuwa nataka Suzuki Vitara, lakini Usalama wa Taifa wanaweza kwa kutumia vigezo vyao wakasema kiongozi fulani apate gari bullet proof (isiyopenya risasi) na iwe na mawasiliano ya kisasa ya simu za upepo na mambo mengine.
"Kwa hiyo ni lazima watapuuza hoja ya Suzuki ili kutimiza jukumu lao la kiusalama, na mifano ipo tayari hapa nchini kuna magari yamenunuliwa kwa Sh bilioni 1.2. Nasema uamuzi gari gani inunuliwe kwa wakati gani si wa anayeendeshwa (kiongozi).
"Halafu niwaeleze tu kwamba gari la kiongozi si mali yake binafsi ni mali ya umma. Mimi nimekuwa nikitumia gari lililokuwa likitumiwa na Pius Msekwa (Spika aliyemtangulia) kwa miaka minne sasa na utaratibu ni kuwa magari ya viongozi wa kitaifa hubadilishwa kila baada ya miaka mitatu," alisema Sitta.
Kuhusu kutaka nyumba ya kifahari, alisema awali alipangiwa kuishi katika eneo la makazi ya mawaziri lakini bila kujali kuwa ni kiongozi wa mhimili wa taifa kama ilivyo mihimili mingine miwili (Mahakama na Serikali), alikwenda kuishi huko.
"Nilikwenda kuishi katika nyumba iliyokimbiwa na Naibu Waziri, Dk. Makongoro Mahanga. Ni nyumba ambayo mfumo wake wa maji taka unapumulia ndani, nimekaa hapo kwa miaka minne, Rais Jakaya Kikwete alipata taarifa hizo.
"Aliagiza (Rais) niondolewe akizingatia nafasi yangu kama kiongozi wa mhimili wa dola. Maagizo hayo yakafanyiwa kazi na watu wa usalama nikapigiwa simu kiwanja kimepatikana na ujenzi unaendelea lakini nihamishwe nilipokuwa naishi na kukodiwa nyumba.
"Hiyo nyumba si dola 8,000 kwa mwezi ni dola 7,000. Izingatiwe kuwa nyumba inayojengwa si yangu binafsi ni mali ya Serikali, Spika mwingine atakuja kuishi humo pia. Na mambo haya yote chanzo chake ni uuzaji wa nyumba za Serikali, viongozi wengine na hata majaji, sasa wanaishi hotelini hata Kilimanjaro Kempinsk Hotel wapo, ni matokeo ya makosa yanayotokana na uamuzi wa uuzaji nyumba," alisema Sitta ambaye amekuwa akiwasema wabunge wenye kulalamalalama kuwa wana ngozi laini na kwamba wanahitaji kuwa na ngozi ngumu kwa kuwa mikwaruzo katika siasa ndiyo ada.
Kuhusu tuhuma inayohusu kununuliwa samani aghali, alisema nyumba aliyokodiwa wakati akisubiri inayojengwa haikuwa na samani yoyote, ikiwamo jenereta kwa ajili ya kuwashia taa za usalama (security light), kuendeshea vifaa mbalimbali vya umeme pamoja na ofisi yake ya nyumbani.
"Mimi sijui bei ya vifaa hivyo madukani, lakini jambo la uhakika ni kwamba taratibu za kiserikali kuhusu manunuzi zimefuatwa na mhusika ni state si mali ya Sitta binafsi, ni ya umma. Hilo gari, nyumba na vifaa vingine ni mali ya umma," alisema.
Katika siku za karibuni kumekuwapo taarifa zinazoihusisha Ofisi ya Bunge, Spika Sitta na ufisadi, lakini pia kumekuwapo na mashambulizi kuelekezwa kwa baadhi ya wabunge mmoja mmoja, hususan wale ambao wanajinadi kuwa vinara wa vita dhidi ya ufisadi.
Katika hatua nyingine, taarifa zinasema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inazichunguza kamati kadhaa za Bunge, ikiwa ni pamoja na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ambayo ilihusika kuibua sakata la Richmond na kuiumbua TAKUKURU yenyewe.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM), William Shelukindo na makamu wake, Dk. Harrison Mwakyembe, ilipendekeza kuchukuliwa hatua kwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk. Edward Hosea, na wasaidizi wake kutokana na kushindwa kubaini udhaifu mkubwa katika sakata la Richmond.

Kamati hiyo iliituhumu TAKUKURU kuisafisha kampuni ya Richmond iliyopaswa kuzalisha umeme wa dharura, na ikapendekeza hatua zichukuliwe dhidi ya watendaji waliohusika katika mchakato wa kutoa zabuni kwa kampuni hiyo.

Hatua ya sasa ya TAKUKURU kuchunguza kamati za Bunge inadaiwa ni ya kulenga kupunguza makali ya Bunge, kupitia kwa wabunge hao hususan kipindi hiki ambacho Bunge linaonekana kuwa moja ya taasisi zinazoungwa mkono na kubeba matumaini ya Watanzania wengi.

Kwa mujibu wa habari zilizotufikia, TAKUKURU wamejipanga kutumia fursa za kisheria walizonazo kufanikisha mpango huo ikiwa ni sehemu ya kujibu mapigo ya wabunge, na mbali na Kamati ya Shelukindo iliyoshupalia Richmond, nyingine ni za Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa mambo mbalimbali yameanza kuchunguzwa katika kamati hizo ikiwa ni pamoja na safari za wajumbe wa kamati hizo kwenye maeneo mbalimbali ya nchi na hususan malipo ya posho, yanayodaiwa kuwa yanalipwa zaidi ya mara moja, kinyume cha taratibu.

Raia Mwema ilizungumza na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila kuhusu suala hilo ana akasema ya kuwa hajapewa taarifa zozote kuhusu kuwapo kwa uchunguzi huo, lakini akaongeza ya kuwa TAKUKURU wanayo mamlaka kisheria kuendesha uchunguzi bila kutoa taarifa rasmi.
Wakati wa uchunguzi wa mchakato ulioipa zabuni ya kufua umeme wa dharura Richmond, TAKUKURU, kupitia kwa Mkurugenzi wake, Dk. Hosea, ilitoa taarifa ya uchunguzi kuhusu kashfa ya kuwapo kwa rushwa na upendeleo katika utoaji zabuni kwa Richmond, ikieleza kuwa hakukuwa na rushwa wala upendeleo.

Hata hivyo, ripoti hiyo ilibainika kupingana na uchunguzi wa sakata hilo uliofanywa na Kamati ya Teule ya Bunge, iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ambayo ilianisha kasoro kadhaa, zikiwamo za kuwapo mazingira ya rushwa.

Kutokana na tofauti hiyo, kamati hiyo ilipendekeza bungeni Dk. Hosea na watendaji wengine mbalimbali serikalini, ambao ilidai walihusika na upendeleo wa utoaji zabuni kwa Richmond wawajibishwe, na Bunge liliafiki mapendekezo hayo na kuyapitisha kama mojawapo ya maazimio yake kuhusu sakata hilo.

Kwa kuzingatia hali na hasa baada ya Serikali kutoa taarifa yake katika mkutano uliopita bungeni, taarifa ambayo ilikataliwa na Bunge, msimamo wa Bunge dhidi ya TAKUKURU na hususan mkurugenzi wa taasisi hiyo si mzuri na wabunge kupitia mijadala bungeni wamekuwa wakishinikiza wawajibishwe, ikiwa ni pamoja na kujiuzulu.

Katika taarifa yake kuhusu adhabu aliyopewa Dk. Hosea, Serikali kupitia kwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja ilisema mkurugenzi huo amepewa onyo kwa kutokuwa makini kuhusu Richmond, hatua ambayo inapingwa na wabunge.
hs3.gif
 
Nahisi Gen. Mwamnyange hana kashifa si achukue nchi au?
 
source????
 
Kweli nchi hii sisi imeoza. Hosea hajamaliza uchunguzi wa Kagoda, Rada, Meremeta, EPA, Ununuzi wa magari na helicopters za jeshi huyo kishatumwa kuwarukia akina Dr Slaa na Zitto!!!
 
Back
Top Bottom