Mbunge Asya Sharif Omar: Kukaimisha Watimishi Muda Mrefu Kunaondoa Ufanisi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Mbunge Asya Sharif Omar: Kukaimisha Watimishi Muda Mrefu Kunaondoa Ufanisi

Mbunge Asya Sharif Omar amesema ipo changamoto kwa wizara ya Maji watumishi wake ngazi ya Wakurugenzi na wakuu wa vitengo kukaimishwa kwa muda mrefu katika nafasi walizopo.

Akichangia hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji ma Mazingira Bungeni Dodoma amesema kitendo cha kumkaimisha mtu muda mrefu kwenye nafasi anakosa amani na hawezi kuwa na maamuzi sahihi katika utekelezaji wa majukumu yake, jambo linaloweza kupelekea kushuka kwa ufanisi wa kazi.

Ameishauri Serikali kuzijaza nafasi za watumishi waliokaimishwa ili kuleta ufanisi katika utendaji wa majukumu yao katika wizara ya Maji kwa kuwa wapo watu wa kutosha wenye sifa.
 

Attachments

  • GF6oUaIW0AAKj07.jpg
    GF6oUaIW0AAKj07.jpg
    124.9 KB · Views: 2
Back
Top Bottom