Sitta avunja kanuni kumhujumu Warioba. TBC wahusishwa, UKAWA waja juu

Zingine hofu tu bila kuwa na sababu za msingi mzee wa viwango ni mtu wa kuzingatia sheria na kanuni tatizo lenu bavicha mnataka kufanya mambo kwa nguvu kama mko kwenye mikutano ya siasa mambo hayaendi hivyo jamani.
yani we jamaa jinga sana na chama chako.si mlimkataa huyu sitta kwenye usipika eti hana uke? Leo amefaa vipi?
 
Jaji warioba afanyiwa njama; Hasira za kalenga zamshukia ndani ya Bunge,.Busara zake binafsi pamoja na busara za mwenyekiti sita zamuokoa. Bonge laahirishwa mpaka hapo itakavyotangwazwa tena.Hili bunge lina watu wenye akili za ajabu sana!

We gamba mbona unaandika takataka!!!
 
Wewe nae tumia akili hapo Kalenga inaingiaje??Hujasikia Sita amevunja kanuni!!Punguzeni ushabiki wa ajabu!!
Natania tu mkuu maana wanaozomea bungeni hawana hoja ya msingi.Utaratibu wa kutengua kanuni bungeni ili kuruhusu kitu fulani kutokana na mazingira ni utaratibuwa kawaida, na mtu mzima unayeaminiwa na umma kwenda bungeni kufanya kazi ya kuzomea maana yake nini? ndio maana mimi nimeamua kuingiza utani tu maana nimeona hamna la maana.
 
Cyo bure kuna mkakati wakuihujumu rasimu kutokana na asilimia80 ya maoni ya rasimu ni ya cdm kitu ambacho atari kwa ccm.
 
Sababu ni kwamba kanuni inamtaka Rais wa JMT kuzindua bunge ndipo M/kiti wa tume aje kuwasilisha rasimu ya katiba katika BMK. Kinyume na matarajio ya kanuni ambazo wao wenyewe wajumbe wa bunge hilo walizipitisha wiki iliyopita, Mh. SS kama M/kiti wa bunge hilo analazimisha kutengua kanuni ili Warioba awasilishe rasimu hiyo na ndipo Rais aje azindue bunge hilo. Kwa mujibu ya wabunge waliokuwa wanapiga kelele wanaotaka kanuni zifuatwe na siyo ivujwe kama Mh. SS anavyotaka.

Safi sana!kuvunja kanuni na sheria ni malezi ya ccm ndiyo maana hata takataka haziishi barabarani maana hakuna wa kumuongoza mwenzake
 
Jaji warioba afanyiwa njama; Hasira za kalenga zamshukia ndani ya Bunge,.Busara zake binafsi pamoja na busara za mwenyekiti sita zamuokoa. Bonge laahirishwa mpaka hapo itakavyotangwazwa tena.Hili bunge lina watu wenye akili za ajabu sana!
Nahisi haya ni maoni yako binafsi, na si lazima uwe ndio ukweli halisi.
 
Haya yalishaisha hakuna kanuni iliyovunjwa pengine hujafuatilia vizuri ila kilichofanyika ni kutengua kanuni ili mambo yaende vizuri.
Kuna wakati mnahitajika kutumia akili zetu kwa busara... Haya mambo ya kutetea visivyo halali haifai..
 
Katika hali isiyotarajiwa na wengi Wabunge wa Bunge maalum la katiba wamezomea jioni yaleo na kusababisha bunge maalumu la katiba kuhairishwa pale aliyekuwa Mwenyekiti wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi jaji Warioba kufika jioni ya leo nakutaka kuwasilisha rasimu ya katiba;iliyopelekea mwenyekiti wa bunge hilo Mh Sita kuhairisha bunge hilo baada ya yeye kushindwa kutumia njia ya kumfanya jaji Warioba kuendelea kuwasilisha rasimu hiyo. MUNGU SAIDIA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUPATE KATIBA MPYA

warioba charii
 
Kwakua hawa jamaa walijichagua wenyewe kwahio hawako accountable kwa mtu yoyote ndio maana lakini kama lile wazo la CHADEMA lingefanyiwa kazi leo hii tusingeona huu upuzzi wote huu. Ndio tuliyoyataka kuwachagua vilaza wengi waingie kwenye BUNGE hili ili kulinda maslahi ya Wapuuzi wachache
 
Jaji warioba afanyiwa njama; Hasira za kalenga zamshukia ndani ya Bunge,.Busara zake binafsi pamoja na busara za mwenyekiti sita zamuokoa. Bonge laahirishwa mpaka hapo itakavyotangwazwa tena.Hili bunge lina watu wenye akili za ajabu sana!

tulia braza,wacha uccm,ukweli unajulikana,kwamba kuna mchezo mchafu wa chama cha mapinduzi, kutokumpa jaji warioba muda wa kutosha kuondoa sumu ilio mwagwa na maccm kuhusu yeye na tume yake, ikiwa mwenyekiti wa bunge kavunja kanuni badala ya rais kufungua bunge, wamemtanguliza jaji warioba ili jk ajeamwage sumu ya kupotosha mazuri ya tume ya katiba, uhondioukweli,
 
Nahisi haya ni maoni yako binafsi, na si lazima uwe ndio ukweli halisi.
Natania mkuu, ishu ni kwamba kuna watu walikuwa wanamzomea Warioba ili ashindwa kuwasilisha hoja yake kwa hoja kwamba kanuni zilitaka Rais azindue bunge kwanza ndio Warioba awasilishe lakini kanuni zikatenguliwa ili warioba awasilishe kwanza.kwa hiyo wale ambao hawakuridhishwa na utenguzi wa kanuni; bila shaka ndio waliokuwa wanazomea.Hata hivyo utaratibu wa utenguaji wa kanuni ni wa kawaida ndio maana nimewashangaa waliokuwa wanazomea na nikaamua kuleta utani tu maana......!
 
Nilisema mapema kuwa sita ni mnafiki hapa jamvini mkampigia debe bila kujua ccm walimnyima uspika leo iweje wampendekeze na hilohilo jitu linataka urais mwakani litafanya liwezalo kujipendekeza mi nalichukia naomba liumwe ghafla likafie bondeni kama wengine lisicheze na katiba ya tanzania
Tumefika huko!!
 
Natania tu mkuu maana wanaozomea bungeni hawana hoja ya msingi.Utaratibu wa kutengua kanuni bungeni ili kuruhusu kitu fulani kutokana na mazingira ni utaratibuwa kawaida, na mtu mzima unayeaminiwa na umma kwenda bungeni kufanya kazi ya kuzomea maana yake nini? ndio maana mimi nimeamua kuingiza utani tu maana nimeona hamna la maana.
Pamoja mkuu.
 
Tatizo CCM wanaenda na upepo. Wakati wanapitisha kanuni ya Rais kuzindua bunge kwanza halafu Mwenyekiti wa Tume ndio kuiwasilisha rasimu baadaye, CCM waliunga mkono kwa wingi wao kwa kusema "Ndiooooooo". Sasa walikuwa wanaitikia ndioo bila kujua wanachokiunga mkono ni nini. Leo wanataka kuivunja kanuni waliyoipitisha wenyewe kwa kulazimisha Mwenyekiti wa Tume aanze kabla ya Rais (ili JK aje ajibu hotuba ya Warioba!!!). Sasa kama wajumbe wametumia wiki tatu wanatunga kanuni tu, iweje siku ya kwanza tu ya kuzitumia kanuni CCM wanataka zivunjwe? Hebu jiulize nia ya hawa watu ni nini hasa!
 
Back
Top Bottom