Sitta ajitosa mgogoro wa Umeya Arusha

hicho kichwa cha habari sijakielewa...! Kushikana mikono haimaanishi ndiyo mmepatana. Ikulu watu hawakuishia kushikana mikono tu...watu walichekeana kama ngedere na kuna wakati Mkulu mwenyewe alikuwa anatoa huduma za juice kama beki tatu....je walipatana?
 
si mara ya kwanza viongozi wa serikali kukataliwa na wananchi.Hata hapa Shinyanga kaimu mkuu wa mkoa pamoja na msaidizi meya walikwisha onja joto ya kuzomewa na kukataliwa na wananchi.Ni suala la maamuzi magumu unaachia ngazi taratiiibu
 
Juice za Machenza zilikuwepo na Kahawa na Kashata za Yemeni?
 
Yule kawekwa pale kwa masilahi ya wakubwa wake lakini kama ingekuwa ni kwa hiyari yake angesha ng'atuka...
 
Duh !! Kweli Arusha wameamua..

Mathayo 18:18
Amin,nawaambieni,yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.

Exegate kidogo hichi kifungu cha mandiko. Tunashindwa kuelewa kwamba ni nani hasa alifunga hapa duniani ni wana wa Arusha au ni serekali ya CCM. Iliyomteua diwani huyo kuwa meya wakitumia kivuli cha uchaguzi geresha, a.k.a usanii wa kishamba.
 
Duh !! Kweli Arusha wameamua..

Mathayo 18:18
Amin,nawaambieni,yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.

wewe! hili nalo neno!
 
Hiyo haki ambayo Lema ameiahidi mbele ya Lebulu si ni pamoja na uhalali wa Meya wa Arusha? Sasa wamepatana wapi hapo?
 
Lini?Kama ni Leo kumbuka ni Jumapili na Pale Kanisani kuna section ya Tutakiane Amani,Umeshawahi ona wanaotakiana amani?Nakuhakikishia ilikuwa ni sehemu ya Ibada Japo yaweza kuwa Imefanyika Nyumbani,Kumbuka askofu au Padre anaweza fanya Ibada popote.Hamna amani na MAGAMBA wewe,Mpaka waondoke Magogoni ndio tutajua Amani imepatikana!!!:poa
 
Back
Top Bottom