Sitta ajitosa mgogoro wa Umeya Arusha

mpushi

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
280
76
Mh lema, mkuu wa mkoa Arusha na Meya wamekutana na kushikana mikono katika harambee ya kuchangia Cathedral la kanisa katoliki Arusha mjini. Hayo yametokea chini ya Baba Askofu Josephat Lebulu na Mh Samwel Sitta.

687qbr.jpg
 
source radio maria ipe credit. naamini haupo kanisani kwani usingeweza kutumia mtandao ama sivo
 
Lile zimwi la kutokukubalika kwa diwani wa kata ya Olorien kama Meya wa jiji la Arusha limeendelea kumwandama Diwani huyo leo baada ya kupata mapokezi hafifu kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa la Mt. Teresia jijini Arusha inayoongozwa na Mh. Samwel Sitta. Tofauti na wageni wengine waliokuwa wakishangiliwa kwa vigelegele na makofi wakati wa utambulisho, Mh. Gaudence Lyimo hakupata mapokezi hayo kutoka kwa waumini hao kama wenzake. Waumini walionyesha kupoa hadi alipotangazwa mgeni mwingine ndipo hali iliporudi kama awali.

Mbunge wa Arusha ameendelea kutomtambua "Meya" huyo kwa kumtambulisha kama diwani huku akimwomba Mh. Sitta kuongea na wakubwa wake ili wakamilishe haraka kuumaliza mgogoro uliopo kupitia kamati iliyoundwa na Pinda na Mbowe.

Ninachojiuliza ni kwamba, ni lini atapata hekima ya kujiuzulu hiyo nafasi ili apate tena heshima kwa jamii ya Arusha. Licha ya kampuni yake ya ujenzi kufanya miradi mingi ya kanisa hilo kabla ya mgogoro huo, waumini hao hawamdhamini tena kama awali. Poor him!
 
Mh S.Sitta akiwa ktk harambee Mjini Arusha.Ameombwa na kutafuta amani ktk mji wa Arusha kwa kuwapatanisha Mbunge Mh Lema na Meya wa Mji wa Arusha,na akachukuwa jukumu hilo kama ambavyo picha inavyojieleza.
Nawasilisha
 

Attachments

  • IMG-20111204-00132.jpg
    IMG-20111204-00132.jpg
    548.4 KB · Views: 303
Amani Arusha itapatikana kwa meya kujiuzulu na uchanguzi halali kufanyika na si kwa kushikana mikono.
 
Duh !! Kweli Arusha wameamua..

Mathayo 18:18
Amin,nawaambieni,yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
 
Hata katika karate, Wachina huwa wanasalimiana kwa kuinama kabla hawajaanza kuzichapa
 
Mbele ya Askofu mkuu Josephat Leburu, Mbunge wa Afrika mashariki Mh. Samweli Sitta .Mbunge Lema ashikana mikono na mkuu wa mkoa wa Arusha na Meya wa Arusha. Lema akihaidi hadharani hana chuki na mtu yeyote binafsi ila hata choka kupigania haki kama haki haita tendeka katika jamii. Amemwomba Mbunge huyo wa Afrika Mashariki kumaliza mgogoro huo mapema. Wadau toeni mchango wenu katika hili.
 
  • Thanks
Reactions: BMT
Sawa sawa kukosana na hawa magamba ni kwa ajili ya kupindisha haki, kitu ambacho mb Lema amehapa kukipigania mpaka mwisho. Hakuna kupatana hapo mpaka haki ieleweke! big up! Lema mapambano mpaka mwisho.
 
Back
Top Bottom