Sitta ajitosa mgogoro wa Umeya Arusha

Mh S.Sitta akiwa ktk harambee Mjini Arusha.Ameombwa na kutafuta amani ktk mji wa Arusha kwa kuwapatanisha Mbunge Mh Lema na Meya wa Mji wa Arusha,na akachukuwa jukumu hilo kama ambavyo picha inavyojieleza.
Nawasilisha

Nilitaka kujua kidogo hapa.

Kwani Lema ni nani katika anga za sheria za nchi?

Kwani Meya asipotambuliwa na Lema lakini sheria za nchi zikimtambua inakuwaje?

 
Hilo pozi la Lemma nimelikubali ile mbaya.

Alafu huyo mayor anatia huruma balaa.
Wamama hawamkubali,
Wacha mungu hawamkubali,
Machalii hawamkubali,
Wazee hawamkubali.

Sijui sasa anan'gan'gania kuwaongoza nani?
 
Hilo pozi la Lemma nimelikubali ile mbaya.

Alafu huyo mayor anatia huruma balaa.
Wamama hawamkubali,
Wacha mungu hawamkubali,
Machalii hawamkubali,
Wazee hawamkubali.

Sijui sasa anan'gan'gania kuwaongoza nani?

Mkuu, kwa hiyo wewe unaangalia pozi la Lema tu, Huna haja ya kujua maendeleo ya wakazi wa Arusha?
 
Mkuu, kwa hiyo wewe unaangalia pozi la Lema tu, Huna haja ya kujua maendeleo ya wakazi wa Arusha?

Politicians hawawezi niletea maendelo yangu binafsi.
Huyo mayor anarepresent Babylon system ambayo inatunyonya kwa sasa. Na ndiyo sababu namchukia kama adui yangu.
Lemma an tu represent sisi ambao tuna struggle on the ground. Ndio maana na m support ingawa sifagilii siasa.
Hiyo kuhusu pozi ilikua on a lighter note!

BTW, R chuga ndio home town, kwa hiyo maendelo ya hapa yananihusu directly.
 
5th December 2011


headline_bullet.jpg
Lakini akishauri Chadema kipunguze ukorofi
headline_bullet.jpg
Lema, Meya wasalimiana kwa mara ya kwanza
headline_bullet.jpg
Mkuu wa Mkoa naye amtaka mbunge yaishe



Arusha(6).jpg

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (kulia) akipena mkono na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo, ikiwa ni mara ya kwanza tangu ulipoibuka mgogoro wa umeya jijini humo mwishoni mwa mwaka jana. Anayeshuhudia (katikati), ni Waziri wa Ushirikiano Afrika Mashariki, Samuel Sitta.


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amekubali kubebeshwa mzigo wa kuwa chachu ya kusuluhisha mgogoro wa umeya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Hata hivyo, Sitta ametoa ushauri binafsi kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupunguza ukorofi kupitia kwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

“Napenda kumwomba Lema na wenzake wa Chadema kidogo wapunguze ukorofi…watu vijijini kidogo wanashindwa kuwaelewa kwa sababu chama kinachotarajia kushika madaraka kidogo kiwe na muonekano wa kushika uongozi na sio kufanya maandamano kila siku, vinginevyo, mtaendelea kupata kura za mijini tu, huo ni ushauri wangu,” alisema Sitta jana mjini hapa wakati wa harambee maalum ya

kuchangia ujenzi wa Kanisa Kuu jipya la Kiaskofu katika Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu iliyoko katika Jiji la Arusha
Sitta alisema kuwa amekubali kuwa chachu ya kusaidia juhudi za upatanishi kutokana na suala hilo kuwa kwa Waziri Mkuu.
Mgogoro huo uliibuka baada ya Chadema kupinga matokeo ya umeya mwishoni mwa mwaka jana, kwa madai kuwa taratibu zilikiukwa

hadi sasa chama hicho hakijamtambua meya.
Madiwani wake watano waliomtambua meya huyo na kufikia mwafaka kwa kugawana nafasi za uongozi wa halmashauri ya Jiji hilo walivuliwa uongozi na Kamati Kuu.

LEMA, MEYA WASALIMIANA, WASHIKANA MIKONO


Kwa kuanzia, Sitta amewafanya mahasimu wakubwa katika mgogoro huo, Mbunge Lema na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo (CCM), kushikana mikono na kusalimiana.
Mahasimu hao kwa nyakati tofauti, walisema imekuwa ni mara ya kwanza kwao kupeana mikono tangu mgogoro wa umeya ulipozuka mwishoni mwa mwaka jana.

RC: SINA UGOMVI NA LEMA


Kabla ya kushikana mikono kati ya Mbunge na Meya, tendo hilo lilifanyika kati ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo na Lema, ambapo mkuu wa mkoa alisema tangu ateuliwa na Rais kushika wadhifa huo mkoani hapa hivi karibuni, jana ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kukaa jukwaa moja.

“Leo (jana) ni mara ya kwanza kwangu kukutana ‘live’ na Lema, namkaribisha ofisini kwangu tukapige maneno,” alisema na kuahidi kuchangia Sh. 500,000.

KAULI YA LEMA


Akikwepa kumtaja kwa cheo cha umeya, Lema, alisema hana ugomvi binafsi Lyimo kama diwani wa Kata ya Olorien, isipokuwa ugomvi wake ni mfumo uliomwingiza kuwa meya kwamba haukuwa halali.

KAULI YA MEYA


Kwa upande wake, Lyimo ambaye alitoa fedha taslimu Shilingi milioni moja, alisema anashukuru tukio hilo kuwakutanisha, na kwa mara ya kwanza wameweza kushikana mikono . Tumeshikana mikono leo licha ya mambo mengi mabaya ambayo amenifanyia, ninamsamehe na yote ninamwachia Mungu ndiye atakayeamua,” alisema Meya Lyimo.

Baada ya kusema hivyo, baadhi ya waumini walianza kuguna na wengine kuzomea kidogo kama ishara ya kutoridhika na kauli yake.
Mapema kabla ya kuwasimamisha Lema na Lyimo mbele ya jukwaa, Sitta alisema, “aliposimama hapa Lema, aliniomba nisaidie upatanishi wa umeya wa Arusha…tunaanza hii safari pamoja kwani Injili ya Mathayo imesema, ‘Heri waliowapatanishi….’ hivyo, nachukua fursa hii

kusema nitakuwa chachu ya kupatanisha mgogoro huu.” Kukubali kwake kunafuatia ombi la Lema, ambaye alichangia Shilingi milioni moja, alimuomba Sitta kusaidia kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.

“Najua mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa umeya Arusha yamefikia ngazi ya juu na sasa yapo kwa Waziri Mkuu, nakuomba Mheshimiwa Sitta usaidie kuhamasisha ili mazungumzo hayo yasaidie kupata muafaka ili tutakapoanza mwaka mpya tuanze na mambo mapya,” alisema Lema.

Alisema anapenda haki na ataendelea kuitafuta haki kwa sababu anachukia dhambi.“Naomba Mheshimiwa Sitta, harakisha ili mazungumzo ya kutafuta muafaka yafikie mwisho,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Lema aliwataka viongozi wa dini kuhakikisha kwamba madhabahu hayatumiki na watu wenye fedha kujipatia nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.

“Mimi ninapenda ukweli na haki kama viongozi wa dini hamtakuwa imara, watu wanaweza kutumia madhabahu kuingia kwenye nafasi za uongozi,” alisema na kuongeza: “Wapo watu wenye fedha nyingi sana wanaweza kutumia madhabahu ili waingie ikulu.”
Wakati wa kuanza kwa harambee hiyo, Sitta, ambaye ni Mbunge wa (Urambo Mashariki CCM), alikubali kubebeshwa mzigo huo.

SITTA: SIKUJA KUJISAFISHA


Aidha, alisema hatarajii kutumia jukwaa hilo kuomba radhi au kujisafisha kwa sababu hana sababu ya kufanya hivyo kwani yeye ni mwaminifu na wananchi wanatambua hilo.

“Wananchi mnawatambua viongozi wenu ambao ni waadilifu na pia mnawatambua wale wengine (hakuwataja), sitarajii kulitumia jukwaa hili kwa kufanya hivyo ingawa ninayo mambo mengi ya kisiasa ya kuzungumza,” alisema na kuongeza: “Wananchi mnatujua hata

tukisemaje.”Hata hivyo, wakati akiwatambulisha viongozi waliokuwa jukwaani, alipofika kwa Lema alisema huyu ni kijana machachari sana na kama alivyokuwa yeye (Sitta) enzi zake alikuwa machachari hivyo hivyo na akamtaka kuendelea kutetea haki.

Aliwataka Wakristu wenzake kujihadhari sana na dhambi ya unafiki na kusengenyana.
Wakati akisema hayo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyarandu alikuwa ndio ameingia muda sio mrefu na kukaa jukwaani hapo, na Sitta akasema Lema ni machachari kama alivyokuwa Nyarandu.

Alisema wao sasa ni wazee na hivyo wanajivunia kuwaachia vijana ambao ni waadilifu ili kuliongoza taifa na kulirejesha kama lilivyokuwa enzi za utawala wa Rais wa kwanza, Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Nyalandu ambaye alifika katika harambee hiyo alikuwa akitokea kwenye shughuli kama hiyo katika Kanisa la St. James ambako Waziri wa

Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alialikwa kuwa mgeni rasmi.
Nyalandu alichangia harambee hiyo Sh. milioni mbili na akaahidi kiasi kingine kilichosalia ili kifike Shilingi milioni 10 atawasilisha nyumbani kwa Sitta Dar es Salaam. Membe alitoa mchango wa Sh milioni moja na ulikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo, Valerian Shayo.

WATU MASHUHURI WACHANGIA


Katika harambee hiyo, familia ya Sitta ilitoa kiasi cha Shilingi milioni mbili; Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alitoa ahadi ya Shilingi milioni tano; Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, alitoa ahadi ya Shilingi 10 na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ahadi ya Shilingi milioni moja.

Wengine aliwataja kuwa ni wabunge kutoka Mkoa wa Tabora, Kigwangalah na Aden Rage wote walitoa ahadi ya Shilingi milioni moja kila mmoja wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu, alitoa ahadi ya Shilingi 500,000.
Wengine waliochangia ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi pamoja na wenzake Sh. milioni mbili, Jaji Mfawidhi wa Mahakama

Kuu Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere Sh. milioni tano; Elias Mshiru, Sh. milioni moja na Aloyce Gonzaga Sh. milioni moja na harambee ilikuwa ikiendelea hadi jioni.
Katika harambee hiyo, jumla ya Shilingi 143,418,500 zilipatikana fedha taslimu zikiwa Sh. 73,736,500 na ahadi Sh. 69,682,000.
Ujenzi wa kanisa hilo hadi kukamilika kwake mwaka 2013, unatarajiwa kutumia zaidi ya Sh. bilioni sita.

CHANZO: NIPASHE


 
Sitta anajiingiza kwenye huo mgogoro wa hao wachagga wawili (lema na lyimo) atauweza??????na kwanini wachagga hawagombanii kwao moshi wanaenda kugombania kwenye miji ya watu???
 
Nilitaka kujua kidogo hapa.

Kwani Lema ni nani katika anga za sheria za nchi?

Kwani Meya asipotambuliwa na Lema lakini sheria za nchi zikimtambua inakuwaje?


Kwani wewe ni nani katika siasa za Tanganyika? Wewe zungumzia mambo ya kwenu pemba siyo ya huku Tanganyika.
 
Ni waziri wa wizara inayoshughulikia mambo ya africa mashariki na sio mbunge wa afrika mashariki. Kuhusu kukutana na ku shake hands sio issue maana hata mugabe alikutana na bush, blair na wenzake kwenye maziko ya papa lakini haikuwa mwisho wa uhasama na chuki
 
Tuesday, 06 December 2011 20:44
Peter Saramba, Arusha

VIONGOZI wa dini mkoani Arusha, wamezitaka pande zinazovutana katika mgogoro wa kisiasa Manispaa ya Arusha, kutafakari kwa kina ili kutafuta njia muafaka na sahihi za kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa takriban mwaka mmoja sasa.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, walisema mgogoro huo haukisaidii chama chochote cha siasa, viongozi wake na hata wakazi wa Mkoa wa Arusha na Watanzania kwa ujumla.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Arusha, Thomas Laizer na mwenzake wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu, ambao tangu awali waliweka msimamo wapamoja kutaka viongozi wa vyama vya siasa na Serikali kutumia busara kumaliza mgogoro huo, jana walisema hakuna njia nyingine inayoweza kutumika kumaliza mgogoro huo wa umeya Arusha isipokuwa
majadiliano yenye nia njema.

Sauti hizo za viongozi hao wa dini, zimekuja siku mbili baada ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta kujitosa katika mgogoro huo akijaribu kutafuta suluhu na kufikia hatua ya kuwakutanisha mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na meya wa jiji hilo, Gaudence Lyimo.

Askofu Laizer
Askofu Laizer aliliambia gazeti hili kuwa njia bora ya kupata suluhu ya mgogoro huo, ni muafaka unaopasa kuweka mbele maslahi na faida ya jamii badala ya vyama na makundi ya watu wanaohusika katika mfafaruku huyo.

“Wapambanapo mafahari wawili, ziumiazo ni nyasi. Nyasi za Arusha ambao ni wananchi wameumia kweli kweli kutokana na mgogoro huu kwani hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana penye magomvi,” alisema Askofu Laizer.

Askofu Laizer alisema tangu kuibuka kwa mgogoro huo yeye na wenzake siku zote, wamekuwa wakifanya maombi maalumu ili suluhu ipatikane. Akaviasa vyama vya CCM na Chadema, kusikia sauti ya wengi wanaopinga vurugu hizo kwa kuwa ni sauti ya Mungu inayolilia amani Arusha.

“Hata kama wenzangu watapingana na msimamo wangu, mimi na kanisa langu tutaunga mkono juhudi zozote za kutafuta muafaka wa kweli Arusha kwa maslahi, faida na maendeleo ya umma wa Arusha,” alisema Askofu Laizer.

Askofu Lekulu
Kwa upande wake, Askofu Mkuu Lebulu, kupitia kwa msaidizi wake, Padri Simon Tengesi alisema:, "Kama ndugu wawili wamegombana ni busara wakakaa chini kwa pamoja na kufikia makubaliano kwa maslahi na manufaa ya
jamii”.

Pamoja na kupinga utaratibu wa uchaguzi uliowaweka pembeni madiwani wa Chadema, viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali Arusha pia walitangaza kutomtambua meya aliyechaguliwa, kutoka CCM, Lyimo.


Bavicha
Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la vijana la Chadema(Bavicha), John Heche alisisitiza kuwa njia pekee ya kupatikana kwa muafaka wa kweli na wa kudumu Arusha ni Serikali kukubali kwamba uchaguzi wa meya ulikiuka kanuni, taratibu na sheria na unapaswa kurudiwa upya hata kama meya wa sasa atasimama na kuibuka mshindi.


“CCM wanaogopa nini kurejea kwenye uchaguzi wakati wana madiwani wengi kuliko Chadema? Serikali iache kutumia mabavu kumng’ang’ania meya ambaye hakupatikana kwa njia halali kwani hawezi kutekeleza wajibu na majukumu yake kwa ufanisi kutokana na dhamira yake kumsuta,” alisema Heche

Heche alisema muafaka wa Arusha hauwezi kupatikana kwa njia ya vitisho vya vyombo vya dola wala hila za baadhi ya watu wachace kuweka mbele maslahi yao binafsi badala ya kujali mahitaji na maoni ya umma.

Heche alisistiza kwamba, kamwe chama chake hakiko tayari kufikia muafaka wa kugawana madaraka na CCM kama njia ya kumaliza mgogoro huo kwani hiyo
siyo moja ya ajenda zakeo.

Alitaja baadhi ya mambo ya msingi yanayostahili kushughlikiwa ili muafaka upatikane kuwa ni pamoja na uchaguzi kurudiwa, askari polisi waliohusika kuua na kujeruhi watu wasio na atia kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu na kesi iliyoko mahakamani dhidi ya viongozi wa chama hicho kuhusiana na tukio la Januari 5, mwaka huu kufutwa.

UVCCM
Mwenyekiti UVCCM Arusha, James Ole Millya alitaka vyama vyote kuepuka mtego wa kutaka kuonekana washindi katika mgogoro huo badala yake washindi wawe wananchi na umma wa Arusha unaoathirika sasa.

Baraza la madiwani la Manispaa ya Arusha, liligubikwa na mgogoro baada ya madiwani wa Chadema kupinga zoezi la uchaguzi uliomweka kwenye kiti cha umeya, Lyimo ambaye ni diwani wa Kata ya Olorien.

Januari 5, mwaka huu watu watatu walikufa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano yaliyoitishwa na Chadema kupinga uchaguzi.

 
Vuingozi wa dini tunawaheshimu lakini tunaomba nao wajiheshimu. Ni wazi kwamba ushauri wao mara nyingi ukiongozwa na maandiko matakatifu na misingi ya imani unalenga katika kuwatetea wanyonge, kujali utu na haki za watu, lakini wakati mwingine viongozi hao huogopa kufanya kazi yao kinabii. Wanashindwa kufanya kazi yao kinabii pale wanaposhindwa kumkemea mkosaji.

Katika mgogoro huu wa Arusha viongozi wa dini wanapotosha waamini wao na wanashindwa kuwaongoza kuzingatia haki. Viongozi wamekuwa wanafiki na wamekuwa wakishindwa kumweleza mkosaji kwamba katika jambo hili umekosea. Kwa unafiki wanawakutanisha Lema na Lyimo kama vile kuna ugomvi kati ya Lema na Lyimo, wakati wanajua kuwa Lyimo kachaguliwa kuwa Meya bila kufuata misingi ya haki. Kama wanashindwa kutetea haki hiyo amani wanayoidai itapatikanaje? Wakumbuke kuwa amani ni tunda la haki. Wakishindwa kumsaidia watu kupata haki yao wanawezaje kuwapatanisha?

Sasa hivi wameanza kuwaalika viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi katika makanisa yao ili wachangie michango mbalimbali wakijidai kuwa tuhuma zao hazijathibitika. Mfano; Lowasa alialikwa katika harambee ya ujenzi katika Parokia ya Nyakato kule Mwanza katika wiki chache zilizopita.Je kule kushakiwa hakutoshi na wao kushakia vile vile wema wa watu hao? Iweje viongozi hao hao wamekuwa wakiwafukuza katika hatua mbalimbali za malezi pale wanaposhakiwa, lakini leo wao wanakuwa wa kwanza kupokea fedha za mafisadi kwa vigezo vya kutothibitika. Hivi wakimaliza kupokea fedha zao na baada ya muda mfupi wakathibitika watazirudisha hizo fedha?

Chonde! Chonde! viongozi wetu wa imani msije mkaingia katika mtego wa wimbo la mafisadi kwa sababu ya umaskini wa waumini wenu. Kumbukeni mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka wananchi waliwafyeka watawala wao na viongozi wa dini. Viongozi wa dini waliingia katika mkumbo huo kwa sababu walishirikiana na watawala katika maovu. Hivyo, viongozi wa dini wawe makini katika kujiingiza katika mambo kama hayo ya Arusha. Wasipoonyesha kwamba ukweli ni upi na mwenye haki ni yupi basi wajue hawana mamlaka itokayo kwa Mungu kufanya hayo wanayofanya.
 
Back
Top Bottom